Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Tunajivunia zaidi ukituamini

Kanuni za Faragha za Uber

Unapotumia huduma za Uber, unakuwa na imani kwamba tutalinda data yako binafsi. Tumejizatiti kudumisha uaminifu huo na hiyo inaanza na kukusaidia kuelewa desturi zetu za faragha. Kanuni zetu za Faragha huweka msingi wa jinsi tunavyoshughulikia faragha hapa Uber.

Tunaifanyia data mambo yanayofaa.

Usimamizi wa data kwa kuwajibika ni sharti la uvumbuzi endelevu. Tunadumisha thamani ya data binafsi kwa ajili ya Uber na watumiaji wetu kwa kushughulikia data kulingana na matarajio ya watumiaji, tukiitunza ikiwa sahihi na iliyokamilika na kuiharibu ipasavyo pale inapokuwa haihitajiki tena. Hii huboresha huduma zetu, huwafanya watumiaji wetu watuamini na hututofautisha sokoni.

Tunaunda faragha kwenye bidhaa zetu kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Faragha ni kipengele muhimu cha kuunda bidhaa na huduma za kiwango cha kimataifa, kuanzia uanzishaji hadi uzinduzi na kuendelea. Kufanya ukaguzi wa faragha kwenye bidhaa, teknolojia na huduma mpya na zilizobadilishwa huhakikisha kwamba zinatimiza matarajio ya watumiaji na kuunda msingi wa kuwapa wateja huduma ya kipekee. Hii inaitwa "faragha kwa makusudi."

Tunakusanya tu kile tunachohitaji.

Tunazingatia lengo mahususi tunapokusanya, tunapotumia au kushughulikia data binafsi ambalo linalingana na malengo na maadili yetu. Tunakusanya na kutumia tu kiasi cha data binafsi tunayohitaji kwa makusudi halali na yaliyoidhinishwa.

Tuna uwazi kuhusu desturi zetu za data.

Tunasema waziwazi kuhusu data binafsi tunayokusanya na jinsi tunavyoitumia na kuishiriki. Tunafanya kile tunachosema.

Tunawapa watumiaji machaguo kuhusu data zao.

Tunawapa watumiaji machaguo dhahiri kuhusu faragha na vidhibiti vyao ambavyo ni rahisi kutumia ili waweze kusimamia data zao.

Tunalinda data binafsi.

Tunatoa ulinzi unaofaa ili kuzuia upotevu na matumizi yasiyoidhinishwa au ufichuaji wa data binafsi.

Dhibiti faragha yako

Tembelea Kituo cha Faragha ili kufanya maamuzi kuhusu jinsi tunavyotumia data yako, uchunguze bidhaa za faragha na kusimamia mipangilio yako ya faragha.

Jinsi tunavyotumia taarifa yako

Uber inaweka huduma za usafiri, usafirishaji wa chakula na huduma nyingine panapoweza kupatikana kwa urahisi. Kuelewa ni data gani tunayokusanya na jinsi tunavyoitumia kunapaswa kuwa jambo rahisi.

Angalizo letu la Faragha linaelezea kwa kina data tunayokusanya na jinsi tunavyoitumia ili kukupa huduma salama na ya kuaminika ya mtumiaji.

Tumefupisha maelezo haya katika chati zilizo hapa chini kwa kila aina ya watumiaji wa Uber, hususan Wasafiri, Wapokeaji wa Oda na Madereva/Wasafirishaji wa Bidhaa.

Chati hizi pia zinaonyesha msingi wa kisheria ambao Uber hutegemea kwa kila utumiaji wa data chini ya sheria za faragha kama vile Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa Data ya Muungano wa Ulaya.

Unaweza pia kupakua toleo lililopanuliwa la chati hii.

Jinsi ya kusoma jedwali hili
  • ✓ inamaanisha kwamba tunatumia data hii kote ulimwenguni
  • ✓* inamaanisha kwamba tunatumia data hii kote ulimwenguni, isipokuwa katika Maeneo ya Kiuchumi ya Ulaya, Uingereza au Uswizi
  • Umuhimu wa Mkataba (CN)
  • Sababu Halali (LI)
  • Inajumuisha jina la kwanza na la mwisho, barua pepe, nambari ya simu, jina la kuingia na nenosiri, anwani, picha ya wasifu, taarifa ya malipo au benki (ikiwemo taarifa inayohusiana na uthibitishaji wa malipo), mipangilio ya watumiaji na taarifa ya mpango wa uaminifu kwa washirika wa Uber. Kwa madereva na wasafirishaji wa bidhaa, hii pia inajumuisha taarifa ya gari au bima, taarifa ya mawasiliano ya dharura na ithibati za afya au uwezo wa kutoa huduma kwa kutumia programu za Uber.

  • Inajumuisha maelezo yaliyowasilishwa wakati wa mchakato wa kutuma ombi la dereva/msafirishaji, kama vile historia ya dereva au rekodi ya uhalifu (panaporuhusiwa na sheria), hali ya leseni, majina maarufu na anwani za awali, na haki ya kufanya kazi.

  • Inajumuisha kitambulisho kilichotolewa na serikali kama vile leseni ya udereva au pasipoti (ambayo inaweza kuwa na picha na nambari za utambulisho, tarehe ya kuzaliwa na jinsia) na picha zilizowasilishwa na mtumiaji kama vile picha za kujipiga na picha za wasifu.

  • Inajumuisha tarehe ya kuzaliwa/umri, jinsia, kazi (kuwezesha vipengele fulani au kutoa bidhaa au huduma zenye ukomo wa umri), kukusanya/kufafanua taarifa za jinsia ili kuteua mapendeleo ya dereva/msafiri na kikundi cha umri na idadi ya wanakaya (kupitia tafiti za mtumiaji).

  • Inajumuisha rekodi za gumzo na simu; ukadiriaji au maoni kwa watumiaji, migahawa au wauzaji; maudhui au rekodi (kama vile rekodi za sauti za ndani ya programu au kamera ya dashibodi) zinazotumwa ili kuwasiliana na Uber.

  • Inajumuisha nyakati na tarehe za safari zijazo za ndege, makazi au kuweka nafasi ya kukodi gari, kupitia kuweka mwenyewe au ufikiaji ulioidhinishwa wa uthibitisho wa barua pepe zinazohusiana na usafiri.

  • Ni pamoja na data sahihi au ya mahali tuliyokusanya kutoka kwenye simu za watumiaji.

  • Ni pamoja na aina ya huduma zilizoombwa au zinazotolewa, maelezo ya safari au oda (kama vile tarehe na saa, kuchukua na kushukisha anwani, umbali wa safari na bidhaa zilizoagizwa); na maelezo ya miamala ya malipo (kama vile jina la mgahawa au muuzaji na eneo, kiasi kilichotozwa na njia ya malipo).

  • Ni pamoja na tarehe na saa za kufikia, vipengele vya programu au kurasa zilizotazamwa, aina ya kivinjari, matukio ya programu kuacha kufanya kazi na shughuli nyingine za mfumo.

  • Ni pamoja na miundo ya maunzi, anwani ya IP ya simu au vitambulishi vingine vya kipekee, mifumo ya uendeshaji na matoleo, programu, lugha zinazopendelewa, vitambulishi vya matangazo, data ya mwendo wa simu na data ya mtandao wa simu.

  • Inajumuisha aina ya mawasiliano (simu, ujumbe wa maandishi au ujumbe wa ndani ya programu), tarehe/wakati na maudhui (kama vile rekodi za simu).

  • Inajumuisha kutoka au kuhusiana na:

    • Kupendekeza dereva
    • Maombi ya OBO (kwa niaba ya)
    • Madai au mizozo
    • Washirika wa biashara ya Uber ambao watumiaji hufungua au kufikia akaunti zao za Uber
    • Washirika wa biashara ya Uber kuhusiana na kadi za benki
    • Wauzaji wanaosaidia kuthibitisha watumiaji au kugundua ulaghai
    • Watoa huduma za bima, magari au fedha
    • Kampuni za usafiri za washirika
    • Vyanzo vinavyopatikana kwa umma
    • Watoa huduma za mauzo na/au wauzaji wa data
    • Maafisa wa kutekeleza sheria, wahudumu wa afya ya umma na mamlaka nyingine za serikali

Maswali kutoka kwa wateja wetu

  • Je, Uber hutumia vipi taarifa ya mahali nilipo?

    Uber hukusaidia ufike mahali unakotaka kwenda. Hii inamaanisha kwamba maelezo ya eneo ni muhimu kwa huduma zetu. Tunayatumia ili kuwasaidia wasafiri na madereva wa Uber kukutana, kubaini barabara bora zaidi, kuwasaidia watumiaji kufuatilia safari zao na kuonesha marafiki zao muda watakaowasili, kubuni huduma na vipengele vipya, kuboresha usalama na ulinzi na makusudi mengine yaliyoelezwa kwenye Angalizo letu la Faragha.

  • Je, Uber huonesha mtu mwingine maelezo yangu?

    Baadhi ya bidhaa, huduma na vipengele vya Uber hujumuisha kushiriki taarifa na watumiaji wengine. Kwa mfano, unapoomba gari, dereva atajulishwa kuhusu maeneo yako ya kuchukuliwa na kushushwa. Tunaweza pia kushiriki taarifa yako ukituomba, kama vile wakati unapotaka kuwajulisha jamaa na marafiki kuhusu hali ya safari yako. Tunaweza pia kutuma taarifa yako kwa washirika wetu, kampuni tanzu na washirika wa kibiashara au kwa sababu za kisheria au iwapo kuna mzozo.

    Angalia Angalizo letu la Faragha kwa maelezo zaidi.

  • Je, maelezo yangu yatahifadhiwa kwa muda gani na Uber?

    Tunahifadhi maelezo ya wasifu wa mtumiaji na muamala kadiri unavyoendelea kutumia akaunti yako ya Uber. Uber huhifadhi maelezo ya gari na rekodi ya uhalifu ya madereva na washirika wanaosafirisha bidhaa (kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria) kwa muda wote wanaoendelea kutumia akaunti yao ya Uber.

  • Ni nini kitakachotendekea maelezo yangu ikiwa nitafuta akaunti yangu?

    Ukifuta akaunti yako, Uber itahifadhi data ya eneo, simu na utumiaji kwa muda wote inaoihitaji ili kutoa huduma na kutii sheria husika. Kwa mfano, tunahifadhi data kama hiyo kwa sababu ya usimamizi, kodi, bima, mashtaka na sababu nyingine za kisheria kwa muda usiopungua miaka 7. Tunaweza pia kutumia maelezo kama haya kwa sababu za kiusalama, kulinda akaunti, kuzuia na kugundua ulaghai na kwa ajili ya utafiti na maendeleo katika kipindi hiki cha uhifadhi.

  • Nitaombaje nakala ya data yangu?

    Unaweza kuomba nakala ya data yako hapa (unatakiwa kuingia katika akaunti). Kwa kawaida, mchakato wa kuunda kumbukumbu yako huchukua siku kadhaa. Unaweza kupata maelezo zaidi hapa kuhusu aina ya data inayojumuishwa.

  • Je, nitatumaje swali kwa Afisa wa Uber Anayesimamia Usalama wa Data (DPO), na jukumu lake ni lipi?

    Afisa wa Uber Anayesimamia Usalama wa Data ana jukumu la kutuongoza kutii sheria ya ulinzi wa data katika Muungano wa Ulaya. Yeye ndiye huwasiliana na wasimamizi wa faragha wa Ulaya na ndiye anayepokea maswali na dukuduku kuhusu faragha ya data kutoka kwa watumiaji wetu.

    Ikiwa una maswali mengine kuhusu data yako binafsi baada ya kusoma Maswali Yanayoulizwa Sana, unaweza kuwasiliana na Afisa wa Uber Anayesimamia Usalama wa Data kupitia fomu hii.

1/6

Ili kupata maelezo zaidi, rejelea Angalizo la Faragha la Uber