Tarehe ya mwisho kubadilishwa: 23/3/2022
Mwongozo wa Jumuiya ya Uber
UINGEREZA
Mwongozo wetu umebuniwa ili kusaidia kufanya kila huduma ya programu ya Uber kwenye simu, tovuti ya Uber na/au kiolesura kingine cha teknolojia ya Uber (“Mfumo wa Uber”) iwe salama, yenye heshima na chanya. Mwongozo unapaswa kuzingatiwa na kila mtu anayetumia Mfumo wa Uber, ikiwa ni pamoja na madereva, wasafiri, matarishi, watumiaji wa Uber Eats, wauzaji wa Uber Eats na biashara nchini Uingereza. Pia unajumuisha mawasiliano ambayo unaweza kuwa nayo na wafanyakazi na wakandarasi wa Uber, ikiwa ni pamoja na katika Vituo vya Madereva wa Uber, kupitia mifumo ya usaidizi mtandaoni au kupitia simu. Mwongozo huu si masharti ya kimkataba na tunaweza kubadilisha maudhui yake wakati wowote.
Mwongozo una muundo ufuatao:
● SEHEMU YA 1 - Madhumuni
● SEHEMU YA 2 - Mwongozo unaotumika kwa watumiaji wote wa Mfumo wa Uber
● SEHEMU YA 3 - Mwongozo wa ziada kwa wasafiri
● SEHEMU YA 4 - Mwongozo wa ziada kwa madereva
● SEHEMU YA 5 - Mwongozo wa ziada kwa matarishi
● SEHEMU YA 6 - Mwongozo wa ziada kwa wauzaji wanaotumia Uber Eats
● SEHEMU YA 7 - Mwongozo wa ziada kwa watumiaji wa Uber Eats
● SEHEMU YA 8 - Jinsi Uber inavyotekeleza mwongozo huu
Asante kwa kujiunga nasi katika kusaidia na kudumisha mazingira bora.
SEHEMU YA 1
Nini madhumuni ya Mwongozo huu?
Mwongozo ufuatao unafafanua kwa kina baadhi ya matendo ya ushirika mzuri tunayohimiza kwenye Mfumo wa Uber na pia matendo au hali zinazoweza kukufanya upoteze uwezo wa kutumia Mfumo wa Uber. Mwongozo ufuatao — ambao tutaubadilisha mara kwa mara — unatoa msingi wa tabia tunazotarajia kutoka kwa watu wote katika jumuiya ya Uber. Kutofuata mwongozo wetu wowote kunaweza kusababisha ukiukaji au kutotii masharti ya mkataba wako na Uber na kunaweza kufanya upoteze uwezo wa kutumia sehemu au Mfumo wote wa Uber. Tafadhali kumbuka kuangalia mwongozo huu kabla ya kutumia Mfumo wa Uber.
Katika hali fulani, mwongozo wetu unatumika katika matukio ya nje ya Mfumo wa Uber tukipata maelezo kuyahusu, ikiwa ni pamoja na wala si tu maelezo kutoka kwenye mifumo mingine au wadhibiti katika eneo uliko, wakati mienendo hiyo inaweza kuhatarisha usalama wa Mfumo wa Uber na watumiaji wake.
Mwongozo unaokufaa unategemea jinsi unavyotumia Mfumo wa Uber. Tafadhali chukua muda usome kwa makini sehemu zilizo hapa chini zinazokuhusu.
SEHEMU YA 2
Mwongozo wetu sote
Kila mtu anayetumia Mfumo wa Uber anatakiwa kufuata mwongozo wa jumla uliowekwa katika Sehemu hii (Sehemu ya 2). Pia kuna miongozo ya ziada katika Sehemu ya 3 hadi 7 hapa chini ambayo inaweza kutumika kulingana na jinsi unavyotumia Mfumo wa Uber. Tafadhali hakikisha kwamba unakagua sehemu hizi, kama inavyofaa.
Heshimu watu wote
Jumuiya yetu ni anuwai na kuna uwezekano mkubwa kwamba utakutana na watu ambao huenda hawafanani nawe au wana imani tofauti na yako. Tafadhali heshimu tofauti hizo. Mwongozo katika sehemu hii unasaidia kukuza mwingiliano mzuri na heshima wakati wa kila huduma.
Mtendee kila mtu katika jumuiya ya Uber jinsi ungependa kutendewa: kwa heshima. Hatua unazochukua unapotumia Mfumo wa Uber zinaweza kuathiri usalama na starehe ya wengine. Ni vyema kuwa na adabu. Ndiyo maana unatakiwa kufanya maamuzi yenye busara na kuwaheshimu watumiaji wengine wa Mfumo Uber na kutangamana na watu wengine kwenye Jumuiya ya Uber—jinsi tu ambavyo ungefanya ukiwa katika maeneo yoyote ya umma.
Tunaamini kwamba kila mtu anapaswa kufurahia na kuridhishwa anapotangamana na watu wengine katika jumuiya ya Uber. Ndiyo sababu tumeweka kanuni na sera zinazohusu kugusana kimwili, unyanyasaji wa ngono na matendo mabaya, vitisho na ujeuri, kuwasiliana baada ya huduma, ubaguzi na uharibifu wa mali.
Kugusana kimwili
Usimguse mtu usiyemfahamu au mtu yeyote ambaye umekutana naye tu wakati unatumia Mfumo wa Uber. Kuna matukio machache tu yanayoruhusiwa kwa watu wanaohitaji au kuomba usaidizi wa kimwili (kwa mfano, wasafiri wanaotumia Uber Assist au walio na mahitaji ya ufikivu ambao wanaweza kuhitaji usaidizi wa kuingia na kushuka kwenye gari) au wakati ambapo mgusano mdogo wa kimwili hauwezi kuepukika. Hairuhusiwi kamwe kumjeruhi au kupanga kumjeruhi mtu yeyote.
Unyanyasaji wa kingono na tabia mbaya
Sote tunathamini nafasi na faragha yetu binafsi. Ni sawa kuzungumza na watu wengine. Lakini tafadhali usitoe maoni kuhusu sura ya mtu au kuuliza kuhusu hali yake ya uhusiano. Unyanyasaji wa kingono na matendo yoyote mabaya ya kimapenzi ya aina yoyote ni marufuku. Ukatili na dhuluma za kingono huhusu kumgusa mtu kingono bila idhini yake ya wazi.
Faragha na nafasi ya kibinafsi inapaswa kuheshimiwa. Orodha ifuatayo inatoa mifano ya baadhi ya matendo yasiyofaa, lakini si kamili:
● Usiulize maswali ya kibinafsi (kwa mfano, kuhusu hali ya uhusiano au mwelekeo wa ngono)
● Usitoe maoni kuhusu sura (kwa mfano, maoni ya kudunisha au “ya kinaya”)
● Usitoe maoni au ishara dhahiri (kwa mfano, maneno, ujumbe au picha za kuchochea ngono)
● Usifanye utani (kwa mfano, kutania kwa ishara au kumkaribia mtu sana)
● Usioneshe vitu visivyofaa (kwa mfano, vitu au picha zinazochochea ngono)
● Usimwendee mtu na mawazo ya ngono asiyoyataka au kufanya vitendo vinavyochochea ngono (hata ikiwa unaweza kudhani kuwa vitendo vyako havina madhara), ikiwa ni pamoja na kukumbatiana, kumbusu, kupendekeza au kuacha tupu sehemu za mwili wako
● Usijihusishe katika tabia zozote za kimwili zisizohitajika ikiwa ni pamoja na kugusa, kufinya, kusukuma na kukamata
● Usiwahofishe wengine, ikiwa ni pamoja na kwa kuwakodolea macho au kuwaangalia kwa muda mrefu
● Uber ina sheria ya kutoonesha maudhui ya ngono, bila kujalisha kama unamfahamu mtu huyo au hata kwa idhini yake
Vitisho na matendo ya ujeuri
Matendo ya fujo, majibizano au unyanyasaji hayaruhusiwi. Usitumie lugha, ishara au kuchukua hatua ambazo zinaweza kumkosea mtu heshima, kumtisha au zisizomfaa. Kwa mfano, usioneshe picha dhahiri (kama vile zinazochochea ngono au ukatili wa kimwili) kwa watu wengine katika jumuiya ya Uber; hii ni pamoja na kuonesha picha hizo bila idhini kupitia mifumo ya huduma kwa wateja wa Uber mtandaoni au kuhusiana na Mfumo wa Uber. Unashauriwa kutojadili mada za kibinafsi ambazo zinaweza kusababisha upinzani, kama vile dini na imani za kisiasa.
Haturuhusu tabia yoyote ya kutisha au ya ujeuri, ikiwa ni pamoja na kwa timu ya Usaidizi wa Uber au katika Kituo cha Madereva wa Uber.
Mawasiliano ya baada ya huduma
Mawasiliano yanapaswa kukomeshwa wakati huduma husika ya Mfumo wa Uber imekamilika, isipokuwa wakati wa kurejesha au kupokea kitu kilichopotea. Mawasiliano yasiyotakikana yanaweza kuonekana kama unyanyasaji na hujumuisha kumtumia ujumbe mfupi, kumpigia simu, kuwasiliana katika mitandao ya kijamii, kumtembelea au kujaribu kumtembelea mtu binafsi baada ya safari au baada ya kumpelekea oda. Usishiriki maelezo yoyote ya mawasiliano yasiyo ya lazima.
Ubaguzi
Unapaswa kuhisi kuwa upo salama, umeheshimiwa na kukaribishwa wakati wote. Ndiyo maana haturuhusu tabia au mienendo ya ubaguzi, ikijumuisha kwenye timu ya Huduma kwa Wateja wa Uber au katika Kituo cha Madereva wa Uber. Usimbague mtu kwa msingi wa sifa kama vile umri, rangi, ulemavu, utambulisho wa kijinsia, hali ya ndoa, asili ya kitaifa, ujauzito, dini, uraia, sura, rangi, dini au imani, msimamo wa kisiasa, mwelekeo wa kingono au sifa zozote zinazolindwa kwa mujibu wa sheria husika.
Kwa mfano, haikubaliki na ni kinyume cha sheria:
● Kukataa kutoa huduma kwa sababu ya sifa kama vile umri wa mtu, rangi, ulemavu, utambulisho wa kijinsia, hali ya ndoa, ujauzito au uzazi, asili ya kitaifa, sura, rangi, dini au imani, msimamo wa kisiasa, mwelekeo wa kingono au sifa nyingine zinazolindwa kwa mujibu wa sheria husika. Sheria husika zinaweza kumtaka/au kuruhusu utoaji wa huduma kwa, na pia kwa manufaa ya kundi mahususi la watu. Katika matukio hayo, huduma zinazotakiwa au kuruhusiwa kwa mujibu wa sheria na vigezo husika zinakubaliwa chini ya mwongozo huu.
● Kutathmini mtumiaji mwingine—iwe ni madereva, wasafiri, matarishi, watumiaji wa Uber Eats, wauzaji, migahawa au biashara—kulingana na sifa hizi.
● Ubaguzi kulingana na mahali msafiri anakoenda au mahali mtumiaji wa Uber Eats anapopelekewa chakula. Tunaelewa kuwa usafirishaji abiria au oda ni mojawapo tu ya shughuli muhimu katika mtindo wako wa maisha. Si kinyume cha mwongozo kukataa kusafirisha watu au oda iwapo shughuli hiyo haikufai. Huruhusiwi kukataa au kughairi, au kutumia vipengele vya Mfumo wa Uber kimakusudi kuzuia maombi ya kusafirisha watu au oda ili kuepuka eneo fulani kwa ajili ya tabia za watu au biashara zinazoendelezwa katika eneo hilo.
Pata maelezo zaidi kuhusu sera ya Uber Dhidi ya Ubaguzi hapa.
Pia tunataka kusaidia katika kuongeza upatikanaji wa aina za usafiri na huduma kwa watu wenye ulemavu ambao wanaweza kuhitaji msaada wa ziada. Ndiyo maana tuna maelezo kwa madereva, wasafiri na watumiaji wa Uber Eats kuhusu mada hii. Unaweza kwenda hapa kwa maelezo zaidi kuhusu ahadi ya Uber ya ufikivu.
Uharibifu wa mali
Huruhusiwi kamwe kuharibu mali. Mifano ni pamoja na kuharibu gari au chombo kingine cha usafiri ulichoitisha kupitia Mfumo wa Uber, kuvunja au kuharibu simu au tableti, kumwaga chakula au kinywaji kimakusudi ndani ya gari, kuvuta sigara kwenye gari, kuharibu eneo la muuzaji au kutapika kwa sababu ya ulevi au vinginevyo. Ukiharibu mali - haijmuishi uharibifu wa kawaida unaosababishwa na matumizi - utawajibikia gharama ya kusafisha na kukarabatii.
Tushirikiane kuimarisha usalama wa kila mtu
Timu yetu inajitahidi kila siku ili kumpa kila mmoja huduma salama. Usalama wako ni muhimu zaidi kwetu. Kila mtu ana wajibu wa kutekeleza ili kuhakikisha mazingira salama. Ndiyo maana tuna kanuni za kuzingatia wakati wa kutumia akaunti pamoja, umri wa mmiliki wa akaunti na mengineyo.
Kutumia akaunti pamoja
Huruhusiwi kutumia akaunti pamoja na mtu mwingine, isipokuwa kwa matarishi wanaotumia haki yao ya kubadilisha - angalia maelezo zaidi hapa. Ili utumie Mfumo wa Uber, unatakiwa kusajili na kuwa na akaunti yako mwenyewe inayofanya kazi. Usimruhusu mtu mwingine atumie akaunti yako na usioneshe mtu mwingine taarifa zako za binafsi unazotumia kwenye akaunti yako, ikiwa ni pamoja na wala si tu jina la mtumiaji, nenosiri au picha zako, ili kuingia kwenye Mfumo wa Uber.
Madereva wanakumbushwa kwamba ni sharti wafanye safari zote wenyewe kwa mujibu wa sheria za mahali walipo, takwa hili halina udhuru.
Watu walio chini ya umri wa miaka 18
Lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili uwe na akaunti ya Uber nchini Uingereza. Hii inamaanisha kuwa sharti uwe na umri wa angalau miaka 18 ili uendeshe gari bila kuambatana na mtu mzima. Mtu aliye na akaunti haruhusiwi kuitisha usafiri au kusafirisha chakula kwa ajili ya walio na umri wa chini ya miaka 18 bila kuambatana naye au na mtu mzima wakati wa safari au wakati wa kupokea chakula. Watoto pia hawaruhusiwi kuagiza chakula wenyewe kwa kutumia akaunti ya watu wazima ya Uber Eats. Masharti haya ya umri yanatumika isipokuwa vigezo na masharti yetu yabainishe vinginevyo.
Maelezo ya gari
Ili kurahisisha kuchukuliwa au kusafirisha chakula, Mfumo wa Uber huwapa wasafiri na watumiaji wa Uber Eats taarifa za kuwatambulisha madereva na matarishi pamoja na magari yao, taarifa hizo zinaweza kujumuisha namba pleti, aina na muundo wa gari, picha ya wasifu na jina lake. Maelezo yasiyo sahihi au ambayo muda wake umeisha huwakanganya wasafiri na wateja wa Uber Eats na yanaweza kuathiri vibaya huduma wanayopata katika Mfumo wa Uber. Madereva na matarishi pia hupewa taarifa za kuwatambulisha wasafiri na watumiaji wa Uber Eats kwa mujibu wa Sera ya Faraghaya Uber.
Madereva na matarishi sharti wakamilishe safari na kusafirisha mizigo kwa kutumia magari yaliyoidhinishwa tu (isipokuwa kwa wahudumu wanaofanya kazi kwa niaba ya wasafirishaji - angalia maelezo zaidi hapa). Ili tuweze kutoa maelezo sahihi, tujulishe maelezo ya gari lako (panapohitajika) na mabadiliko yoyote kwenye hati zako ambayo huenda yakasababisha tatizo, kama vile leseni ya udereva ambayo muda wake unakaribia kuisha.
Mikanda ya usalama
Kutumia mkanda wa usalama kunaweza kuwa njia bora zaidi ya kuokoa maisha na kupunguza majeraha yanayotokana na ajali za gari - ndiyo maana ni sharti la kisheria nchini Uingereza kujifunga mkanda wa usalama unapoendesha gari. Kila tarishi anayetumia gari, kila dereva, kila msafiri, hata aliye kwenye kiti cha nyuma, sharti afunge mkanda wa usalama kila wakati. Wasafiri wanapaswa kuitisha gari ambalo lina viti vya kutosha idadi yao na wasisafiri katika makundi makubwa yanayozidi idadi ya mikanda ya usalama kwenye gari. Ni lazima madereva wakatae safari kwenye Uber ikiwa hakuna viti au mikanda ya usalama kwenye gari kwa ajili ya kila msafiri.
Helmeti kwa ajili ya baiskeli, mopedi na skuta
Kwa usalama wako, unaposafiri kwa baiskeli, mopedi au skuta, hakikisha una helmeti inayokutosha vizuri. Helmeti inaweza kukulinda ukiivaa vizuri kulingana na maelekezo ya mtengenezaji, kwa mfano ifunike kipaji chako cha uso na uifungie chini ya kidevu chako.
Kuwa mwangalifu
Hatua ya kuwa barabarani ina maana kwamba una jukumu la kuhakikisha usalama wako na watu wengine. Hii inamaanisha kuwa mwangalifu barabarani na kupumzika vizuri, ili uweze kushughulikia hali yoyote kwa haraka. Tunakagua ripoti za ajali na mienendo isiyo salama ya kuendesha gari.
Usimamizi na utunzaji mzuri
Kwa mujibu wa vigezo vya mkataba wa Uber, madereva na matarishi wanatakiwa kukagua magari mara kwa mara na kuhakikisha kuwa yako katika hali nzuri, ikiwa ni pamoja na wala si tu breki, mikanda ya usalama na magurudumu. Hii inamaanisha kudumisha magari yao kulingana na viwango vya usalama na matengenezo vya sekta, na kufuatilia na kukarabati sehemu zozote ambazo zimebainishwa na mtengenezaji.
Kutumia barabara pamoja
Ili barabara ziwe salama, madereva na matarishi wanatakiwa kuwa na desturi salama, ambayo inajumuisha kuwajali watu wote, bila kujali jinsi wanavyosafiri.
Dharura za umma
Uber inaweza kuchukua hatua zaidi ili kujaribu kudumisha usalama wa Mfumo wa Uber wakati wa dharura za umma, ambayo ni pamoja na majanga ya asili, dharura za afya ya umma na mikasa ya umma.
Kwa mfano, Uber ikipokea habari kutoka kwa mamlaka ya afya ya umma kwamba mtu anayetumia Mfumo wa Uber anaweza kudhuru umma, tunaweza kusitisha akaunti ya mtu huyo hadi itakapokuwa salama kabla ya kumruhusu aendelee kutumia Mfumo wa Uber. Vivyo hivyo, tunaweza kuwazuia watu katika jiji au eneo zima wasitumie sehemu au Mfumo wote wa Uber au kuweka masharti mengine kwa mujibu wa mwongozo wa mamlaka wakati wa dharura ya afya ya umma, majanga ya kiasili au mikasa mingine ya umma. Au, wakati utumiaji wa Mfumo Uber unaweza kusababisha hatari.
Fuata sheria
Tumejitolea kufuata sheria zote zinazotumika na kuaminika na tunatarajia kila mtu anayetumia Mfumo wa Uber kutekeleza wajibu wake na kutii sheria na kanuni husika, pamoja na sheria na kanuni za viwanja vya ndege panapohitajika.
Tuna masharti kulingana na sheria na kanuni zinazotumika ambazo kila mtu anapaswa azifuate. Kwa mfano, kutumia Mfumo wa Uber kutekeleza uhalifu wowote— kama vile kusafirisha dawa za kulevya, utengenezaji wa pesa bandia, usafirishaji haramu wa dawa za kulevya au binadamu—au kukiuka sheria au kanuni nyingine yoyote, imepigwa marufuku kabisa.
Fuata sheria zote
Kila mtu ana wajibu wa kujua na kutii sheria zote husika, ikiwa ni pamoja na sheria na kanuni za viwanja vya ndege ukiwa katika uwanja wa ndege na sheria za barabara— ikiwa ni pamoja na kutii sheria za trafiki, alama na ishara—wakati wote unapotumia Mfumo wa Uber.
Leseni, vibali na hati nyingine zozote husika za kisheria zinazohitajika kwa madereva na matarishi sharti ziwe hazijaisha muda wa matumishi kila wakati na panapohitajika, zitolewe kwa Uber. Kwa mfano, madereva na matarishi wote wanaotumia magari wanatakiwa kisheria kuwa na leseni ya udereva, bima na hati ya usajili wa gari, vyote vilivyo halali. Hii pia inajumuisha kutimiza masharti ya kisheria ya kupata leseni ya kukodisha gari la binafsi au teksi katika eneo lako.
Tunakagua ripoti za ajali au matatizo ya trafiki ambayo huenda yametokea wakati wa kusafirisha watu au oda na ripoti nyingine, zikiwemo zile ambazo zinaweza kuonesha uendeshaji mbaya au usio salama. Sheria za mahali ulipo kuhusu maegesho zinaweza kupunguza mahali ambapo madereva na matarishi wanaweza kuegesha magari yao wanapochukua oda, kuwasilisha bidhaa au kusubiri wasafiri wafike au kushuka gari. Madereva na matarishi sharti watii sheria hizi. Kwa mfano, ni kinyume cha sheria kufunga njia za baiskeli au kufunga njia za walio na ulemavu.
Kwa wasafiri na watumiaji wa Uber Eats, mruhusu dereva au tarishi aendeshe gari. Kwa mfano, msafiri hapaswi kugusa usukani, au gia au vinundu, vitufe au vifaa vingine ambavyo vinatumika kuendesha gari. Kwa wasafiri na watumiaji wa Uber Eats, usimwombe dereva au tarishi aendeshe kwa kasi au asimame, ashukishe au aendeshe gari kinyume cha sheria.
Unapoendesha au kuegesha baiskeli, au mopedi zingatia kanuni na sheria za mahali ulipo. Kufuata sheria za barabarani kwa kawaida hukuhitaji uwapishe watu wanaotembea kwa miguu, kuendesha upande unaofaa, kuonyesha ishara ikiwa unanuia kupiga kona, na kusimama kabisa kwenye taa nyekundu na alama za kusimama.
Pombe na dawa za kulevya
Huruhusiwi kutumia dawa za kulevya au kufungua chupa za pombe ukitumia Mfumo wa Uber.
Ikiwa wewe ni dereva, tarishi au msafiri wa chombo chenye magurudumu mawili, kwa mujibu wa sheria huwezi kuendesha usafiri huo ukiwa umelewa. Sheria haikuruhusu kuendesha gari, baiskeli au mopedi ukiwa umekunywa pombe, umetumia dawa za kulevya au vileo vingine ambavyo hupunguza uwezo wako wa kuendesha gari, baiskeli au mopedi kwa njia salama. Ukikumbana na msafiri aliyelewa kupita kiasi au mwenye vurugu, una haki ya kukataa safari kwa sababu ya usalama wako.
Ikiwa wewe ni msafiri na una sababu ya kuamini kuwa dereva wako ni mlevi au ametumia dawa za kulevya, mwambie aghairi safari hiyo mara moja. Kisha shuka na upige simu kwa mamlaka ya karibu au huduma za dharura. Ukishuka gari lako, tafadhali pia ripoti kuhusu tukio lako kwa Uber.
Marufuku ya bunduki na silaha
Wasafiri na wageni wao, na pia madereva na matarishi, hawaruhusiwi kuwa na bunduki na silaha wanapotumia Mfumo wa Uber, kwa mujibu wa sheria husika.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Sera yetu ya Kukataza Bunduki hapa.
Ulaghai
Hairuhusiwi kutoa maelezo ya uongo kwa makusudi au kutumia utambulisho wa mtu mwingine, kwa mfano wakati wa kuingia katika akaunti au kufanyiwa ukaguzi wa usalama. Ni muhimu kutoa maelezo sahihi unaporipoti matukio, kufungua na kutumia akaunti zako za Uber, kupinga matozo au ada na kuomba mikopo. Omba tu ada, matozo au kurejeshewa pesa unazostahiki, na utumie ofa na matangazo kama tu ilivyokusudiwa. Usifanye miamala isiyo sahihi kimakusudi.
Shughuli za ulaghai zinaweza pia kujumuisha, lakini si tu:
● kuongeza makusudi muda au umbali wa safari au wa usafirishaji wa bidhaa kwa sababu za ulaghai au vinginevyo;
● kukubali maombi ya usafiri, oda au kusafirisha bidhaa bila nia ya kukamilisha, ikiwa ni pamoja na kuwashawishi wasafiri au watumiaji wa Uber Eats waghairi kwa sababu za kilaghai;
● kufungua akaunti ghushi au za ziada kwa sababu za ulaghai;
● kudai ada au matozo ya kilaghai, kama vile ada za usafishaji zisizo za kweli;
● kuomba, kukubali au kukamilisha safari au usafirishaji wa bidhaa kwa uwongo au ulaghai kwa makusudi;
● kudai kuwa umekamilisha usafirishaji hata bila kuchukua mzigo;
● kuchukua mzigo halafu ukabaki nacho chote au sehemu yake, na kutosafirisha mzigo wote;
● vitendo vinavyokusudiwa kuvuruga au kudhibiti utendaji wa kawaida wa Mfumo wa Uber, ikiwa ni pamoja na kurekebisha mipangilio kwenye simu ili kuzuia utendaji bora wa mfumo na kipengele cha GPS;
● kutumia vibaya ofa na/au kutozitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa;
● kupinga ada au matozo kwa sababu za ulaghai au zisizo za kweli;
● kutoa madai ya uongo dhidi ya mwingine ili ujinufaishe kifedha (yaani kurejeshewa pesa);
● kumruhusu mtumiaji mwingine afikie akaunti yako kinyume cha sera yetu ya kushiriki akaunti; au
● kughushi hati, rekodi au data nyingine kwa sababu za ulaghai.
Kuitisha huduma nje ya mfumo na malipo ya pesa taslimu
Ili kuimarisha usalama wa kila huduma, ni sharti madereva wahakikishe wanazingatia masharti yao ya kisheria kuhusu kukubali safari nje ya mfumo na kukodishwa, jambo ambalo haliruhusiwi kwa madereva binafsi wa kukodisha. Wasafiri pia hawapaswi kulipia safari kwa pesa taslimu au kuitisha dereva moja kwa moja nje ya Mfumo wa Uber.
Shughuli zisizokubalika
Usitumie kamwe chapa ya biashara au hakimiliki ya Uber bila ruhusa. Ikiwa inahitajika kwa mujibu wa sheria za nchi husika au ikiwa unaruhusiwa na Uber kuonesha bidhaa zilizo na chapa ya Uber, madereva na matarishi wanapaswa kutumia tu bidhaa zenye chapa ya Uber ambazo zinapatikana kutoka kwa Uber au mshirika aliyeidhinishwa wa Uber. Madereva na matarishi hawapaswi kuonesha bidhaa zilizo na chapa ya Uber wakiwa nje ya Mfumo wa Uber. Huruhusiwi kutumia bidhaa zisizoruhusiwa au za watu wengine — kama vile taa, mabango, ishara au bidhaa kama hizo zikiwa na jina la Uber au alama ya biashara.
Matumizi ya Programu/Tovuti
Unapotumia Programu ya Uber na/au tovuti lazima:
● utumie programu, tovuti na nyenzo zozote zinazotolewa, kwa mujibu wa sheria ya hakimiliki na Masharti yetu ya Programu/Tovuti.
● usifanye, usiwezeshe, kuidhinisha au kuruhusu uvunaji wowote wa matini au data au kukomba wavuti kuhusiana na programu, tovuti au huduma zozote zinazotolewa kupitia, au kuhusiana na, programu na/au tovuti yetu (isipokuwa kama marufuku hiyo hairuhusiwi na sheria husika).
● usiingize bila kujua virusi, programu za trojani, vidudu, mabomu ya kimantiki au nyenzo nyinginezo ambazo ni hasidi au hatari kwa teknolojia kwenye programu na/au tovuti yetu. Hupaswi kujaribu kupata idhini ya kufikia programu na/au tovuti yetu, seva ambayo programu na/au tovuti yetu imehifadhiwa au seva yoyote, kompyuta au hifadhidata iliyounganishwa kwenye programu na/au tovuti yetu. Ni sharti usishambulie programu na/au tovuti yetu kwa kutumia shambulizi la kunyima huduma au usambaaji wa kunyima huduma.
● uunganishe tu kwenye programu na/au tovuti yetu kwa njia ya haki na ya kisheria, isiyo haribu sifa yetu au kutumia vibaya na kwa namna inayotii Vigezo na Masharti yetu ya Programu/Tovuti.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia programu na/au tovuti ya Uber, tafadhali angalia Vigezo na Masharti ya Programu au Tovuti yetu hapa.
Maoni yako ni muhimu sana
Ikiwa jambo litatokea, liwe zuri au baya, tunarahisisha mchakato ili uweze kutuambia moja kwa moja kwenye programu au kwa kuwasiliana na timu ya Huduma kwa Wateja wa Uber. Unaweza kubonyeza Usaidizi kwenye programu au utembelee help.uber.com ili timu yetu ya Usaidizi iweze kufuatilia. Ikiwa kuna dharura au ukipata hatari ya ghafla, julisha mamlaka ya eneo lako au huduma za dharura kabla ya kuarifu Uber. Timu yetu inaendelea kuboresha viwango vyetu na maoni yako yanatusaidia kuchukua hatua inayofaa na kudumisha ufaafu wa viwango vyetu kadri teknolojia yetu inavyoimarika.
Unaweza kuchagua kadiria huduma unayopata mwishoni mwa kila safari. Maoni ya kweli husaidia kuhakikisha kwamba kila mtu anawajibikia tabia yake na pia yanaweza kuboresha huduma kwa watumiaji wengine. Uwajibikaji huu husaidia kudumisha mazingira chanya, salama na yenye heshima.
Tathmini
Madereva, wasafiri, matarishi, watumiaji wa Uber Eats na wauzaji wana chaguo la kuwapa tathmini watumiaji wengine, na pia kutoa maoni kuhusu safari au usafirishaji wa mizigo. Mfumo huu wa maoni huboresha uwajibikaji na husaidia kudumisha mazingira ya heshima, usalama na uwazi kwa kila mtu. Madereva na matarishi wanaweza kuona tathmini zao za sasa kwenye programu. Wauzaji wanaweza kupata tathmini yao ya watumiaji na matarishi wa Uber Eats kwa kuingia katika akaunti ya Msimamizi wa Uber Eats. Wasafiri wanaweza kuona tathmini yao chini ya majina yao kwa kufungua programu na kugusa menyu.
Katika hali ambapo tathmini ya msafiri ni ya kiwango cha chini, tunaweza kuwasiliana na msafiri, na baadaye tunaweza kumsitisha au kumzuia kutumia akaunti ya Uber.
Kama ungependa kudumisha wastani wa tathmini za juu, ni muhimu uwe na nidhamu na heshima kwa watu wote unapotumia Mfumo wa Uber na kushirikiana na watu wengine katika jumuiya ya Uber. Kwa kawaida madereva na matarishi wanaotumia Mfumo wa Uber hutoa huduma bora kwa wasafiri na watumiaji wa Uber Eats, na wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wa Uber Eats wana nidhamu na heshima, kwa hivyo safari nyingi hufanyika vizuri. Uber inaweza kutoa maelezo ambayo yanaweza kukusaidia kuboresha tathmini yako mara kwa mara.
Kuwasiliana na Usaidizi wa Uber hakutasababisha kuondolewa kwa tathmini ya mtu binafsi. Tunajua kwamba wakati mwingine usafirishaji wa watu au oda hautekelezwi vizuri—ndiyo maana tathmini yako huwa wastani.
Kukubali Usafirishaji, oda na safari
Ikiwa wewe ni dereva au tarishi na hutaki kukubali maombi ya safari au kusafirisha bidhaa, unaweza kukataa ombi hilo, kulipuuza au kuondoka mtandaoni au kujiondoa kwenye akaunti. Si lazima ukubali idadi fulani ya chini ya safari au usafirishaji wa bidhaa. Ikiwa wewe ni muuzaji, tumia kipengele cha ‘Sitisha Oda Mpya’ au uondoe upatikanaji wa bidhaa mahususi. Hatua hii husaidia kuhakikisha kwamba mfumo unamnufaisha kila mtu.
Kwa matarishi, madereva na wauzaji, ukikataa maombi ya safari au oda mfululizo, teknolojia yetu inaweza kuchukulia kwamba hungependa kukubali safari au oda zaidi au umesahau kuondoka kwenye akaunti na huenda ukaondolewa kwa muda. Hata hivyo, una uhuru wa kuingia tena wakati wowote unapotaka kuanza kukagua maombi yoyote ya usafiri.
SEHEMU YA 3
Mwongozo wa ziada kwa wasafiri
Mbali na kufuata mwongozo wa jumla uliowekwa katika Sehemu ya 2, wasafiri wanaochagua kutumia Mfumo wa Uber sharti wafuate yafuatayo.
Tabia za wasafiri
Tafadhali jaribu kufika kwa wakati ili usafiri. Kwa kawaida, si vizuri kupiga kelele, kuapa au kufunga milango kwa nguvu. Na kwa kudumisha usafi—iwe ni kwa kuenda na takataka nyumbani au kupangusa kinywaji kilichomwagika, utasaidia kuhakikisha kwamba kila mtu anapata safari nzuri.
Mmiliki wa akaunti atawajibikia matendo ya wasafiri wenzake wakati wote wa kusafiri kwenye Uber. Ukiitisha usafiri kwa mtu mwingine mzima, utawajibikia tabia yake wakati wa safari.
Ada ya Kughairi Safari
Katika hali ambapo mmiliki wa akaunti ana haki ya kughairi ombi la usafiri, mmiliki wa akaunti anaweza kutozwa ada ya kughairi kulingana na sera yetu ya kughairi - inayopatikana hapa.
Uber pia inaweza kutoza ada ya kughairi katika hali ambapo inakataa maombi au kughairi baadhi ya huduma kwa sababu ina shaka kuhusu usahihi au usahihi wa ombi au kuhusu maelezo ya mawasiliano.
Viti vya watoto
Wasafiri wanatakiwa watii sheria husika wanaposafiri na watoto. Pale ambapo sheria inataka utumiaji wa kiti cha mtoto, ni jukumu la msafiri kutoa na kuweka kiti kinachofaa, isipokuwa kama mwongozo, vigezo na masharti au sera zetu zinasema vinginevyo. Watoto walio na umri wa chini ya miaka 12 wanapaswa kuketi kwenye viti vya nyuma.
Unapowachukua wasafiri walio na watoto wadogo, madereva wanaweza kuwapa muda zaidi kuweka kiti cha mtoto vizuri kabla ya kuanza kuendesha gari. Ikiwa msafiri hana kiti cha mtoto kinachofaa, ikiwa dereva hangependa msafiri aweke kiti cha mtoto kwenye gari lake, ikiwa mtoto haonekani kutimiza masharti ya kimo na uzani wa usalama wa kiti, au ikiwa dereva anahisi kwamba mtoto hawezi kubebwa kwa usalama, dereva anaweza kughairi safari ya Uber.
Ada ya Usafishaji
Wakati wa usafiri kwenye Uber, mmiliki wa akaunti atawajibikia ada zozote za ziada zinazoweza kutozwa pale ambapo mmiliki wa akaunti, mgeni wake au mtu mwingine ambaye mmiliki wa akaunti amemwitishia usafiri, amechafua mazingira au kuchafua gari, katika hali ambayo mmiliki wa akaunti anaweza kutozwa kwa uharibifu huo, pamoja na ada ya kusafisha. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu matozo na ada za usafishaji hapa.
Kukiuka Vigezo na Masharti ya Wasafiri na Mwongozo huu
Kukiuka Masharti ya Wasafiri au mwongozo huu unajumuisha tabia ambayo, kwa maoni yetu, inaweza kuathiri biashara au sifa yetu au kuharibu uhusiano na uaminifu kati yetu. Ifuatayo ni mifano ya mambo ambayo kwa kawaida huchukuliwa kuwa ukiukaji wa mwongozo huu na/au Masharti ya Msafiri:
● wizi au ulaghai;
● mashambulizi ya kimwili, uonevu, ukatili wa ngono au matendo mabaya ya kingono;
● uharibifu mbaya na wa makusudi wa mali; na
● ubaguzi kinyume cha sheria, udhalilishaji au unyanyasaji.
Orodha hii imekusudiwa kuwa mwongozo na si kamili.
SEHEMU YA 4
Mwongozo wa ziada kwa madereva
Mbali na kufuata mwongozo wa jumla uliowekwa katika Sehemu ya 2, madereva wanaochagua kutumia mfumo wa Uber sharti watii yafuatayo.
Wanyama wa kutoa huduma na vifaa vya usaidizi
Madereva wanaotumia Mfumo wa Uber wanapaswa kuzingatia sheria zote zinazosimamia usafirishaji wa watu walio na ulemavu, ikiwa ni pamoja na kusafirisha wanyama wa kutoa huduma na vifaa vya kuwasaidia (kama vile viti vya magurudumu). Madereva sharti pia watekeleze wajibu wowote uliowekwa na mamlaka kulingana na leseni zao za ukodishaji wa binafsi au wa teksi.
Madereva wanaotumia programu ya Dereva hawapaswi kumkataa msafiri aliye na mnyama wa kutoa huduma au kifaa cha kumsaidia (kama vile kiti cha magurudumu au mikongojo) kwa sababu ya mnyama wa kutoa huduma au vifaa vya kumsaidia - isipokuwa kama wana cheti halali cha udhuru kilichotolewa na mamlaka ya eneo husika. Kwa viti vya magurudumu visivyokunjika, ni lazima utumie magari yanayoweza kutumiwa na viti vya magurudumu. Kwa kawaida, sheria zinazotumika huwakataza madereva kuwanyima wasafiri huduma kwa sababu ya wanyama au vifaa vya kuwasaidia, na kuwabagua wasafiri walio na wanyama wa kutoa huduma au vifaa vya kuwasaidia, hata kama dereva ana imani tofauti ya kidini au anaogopa wanyama. Ukikataa msafiri kwa sababu ya mnyama wa kutoa huduma au vifaa vya kumsaidia, bila udhuru halali, huenda ukapoteza idhini ya kutumia Mfumo wa Uber na ripoti inaweza kupigwa kwa mamlaka ya kutoa leseni ya mahali ulipo.
Masharti ya usalama wa dereva
Wasafiri wa ziada na wasio na akaunti
Unapoendesha gari kwa kutumia programu ya Uber, hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kwenye gari isipokuwa aliyeitisha usafiri pamoja na wageni wake. Takwa hili linatumika isipokuwa vigezo na masharti yetu yanaposema vinginevyo.
Saa za kuendesha gari
Ukiwa dereva, ni wajibu wako kuchukua na kudhibiti mapumziko na vipindi vya kupumzika na kujiburudisha. Madereva pia wanatakiwa kutii sera ya Ukomo wa Saa za Kuendesha Gari (hapa).
Sera ya Afya na Usalama
Madereva wote wana wajibu wa kufanikisha mazingira salama ya kazi. Ni sharti ushughulikie afya na usalama wako na wa wengine ikiwa ni pamoja na wale unaokutana nao kwa sababu ya kutumia Mfumo wa Uber kama vile wasafiri na watumiaji wengine wa barabara.
Unapofanya safari katika Mfumo wa Uber ni lazima kila wakati:
● kuzingatia na kutii sheria za barabara na usalama zinazotumika katika barabara kuu
● uwe na afya njema ili uweze kuendesha gari
● ufuate maelekezo kuhusu utumiaji salama wa kifaa chochote unachotumia
● usijihusishe na tabia za kizembe, ikiwa ni pamoja na kuendesha gari kwa njia isiyo salama, kuendesha gari ambalo si salama, kufanya safari ukiwa umelewa pombe au dawa za kulevya, au kuchukua hatua inayodhuru au kutishia kuathiri usalama wa wasafiri, watumiaji wengine wa barabara au wahusika wengine.
Unapaswa kuripoti matatizo yoyote ya afya na usalama mara moja kwa timu ya Usaidizi wa Uber au katika Kituo cha Madereva wa Uber.
Lazima ushirikiane na Uber katika masuala ya afya na usalama, ikiwa ni pamoja na katika uchunguzi wa tukio lolote. Ajali na majeraha yote, hata yawe madogo, yanapaswa kuripotiwa kwa timu ya Usaidizi wa Uber au katika Kituo cha Madereva wa Uber.
Tutahakikisha kwamba una idhini ya kupata mafunzo ili ufanye kazi yako kwa ufanisi na usalama.
Kukosa kutii sera hii kunaweza kuchukuliwa kuwa ukiukaji wa mwongozo huu.
Utumiaji wa kamera za dashibodi au CCTV zinazorekodi video na/au sauti
Madereva wanaweza kuchagua kusakinisha na kutumia kamera ya dashibodi, ambayo inaweza kutumika kurekodi safari na kutoa ushahidi kwa Uber, mamlaka ya kutekeleza sheria au kampuni za bima endapo kutatokea hitilafu kwenye safari. Tafadhali kumbuka yafuatayo:
● Wasafiri wanaoabiri gari la usafiri wa pamoja lenye kamera ya dashibodi wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu jinsi video, picha au mazungumzo yaliyorekodiwa na kamera ya dashibodi yatakavyotumika. Baadhi ya mamlaka zinazotoa leseni haziruhusu utumiaji wa kamera ya dashibodi au CCTV, au zinahitaji, pamoja na mambo mengine, msafiri atoe idhini ya kurekodiwa. Tafadhali angalia hali ya sheria na kanuni husika nchini Uingereza ili uelewe majukumu yako.
● Madereva wanaweza kutuma rekodi kwa Uber kwa hiari yao. Huenda Uber ikakagua video zilizowasilishwa na kuchukua hatua kulingana na mwongozo huu na masharti ya mfumo.
Kuonesha au kutiririsha picha, sauti au rekodi ya video ya mtu kwenye mitandao ya kijamii au katika maeneo mengine ya kidijitali au ya umma, ni ukiukaji wa mwongozo wetu na unaweza kusababisha uchunguzi zaidi kutoka kwa timu yetu ya usalama.
Viti vya watoto
Madereva wanapaswa kutii sheria zinazohusika wakati wasafiri wanasafiri na watoto wachanga. Pale ambapo sheria inataka utumiaji wa kiti cha mtoto, ni jukumu la msafiri kuwa nacho na kuweka kiti kinachofaa, isipokuwa kama vigezo na masharti au sera zetu zinasema vinginevyo. Watoto walio na umri wa chini ya miaka 12 wanapaswa kuketi kwenye viti vya nyuma.
Unapowachukua wasafiri walio na watoto wadogo, madereva wanaweza kuwapa muda zaidi kuweka kiti cha mtoto vizuri kabla ya kuanza kuendesha gari. Ikiwa msafiri hana kiti cha mtoto kinachofaa, ikiwa dereva hangependa msafiri aweke kiti cha mtoto kwenye gari lake, ikiwa mtoto haonekani kutimiza masharti ya kimo na uzani wa usalama wa kiti, au ikiwa dereva anahisi kwamba mtoto hawezi kubebwa kwa usalama, dereva anaweza kughairi safari.
Sera ya kutoa taarifa
Tumejitolea kufanya biashara yetu kwa uaminifu na uadilifu. Ukiukaji wowote unaoshukiwa unapaswa kuripotiwa haraka iwezekanavyo. Madereva wanaweza kuripoti matatizo yoyote kuhusu ukiukaji kwa kufuata sera ya Kutoa Taarifa, ambayo inapatikana hapa.
Kukiuka Vigezo na Masharti ya Dereva na Mwongozo huu
Kukiuka Vigezo na Masharti ya Dereva au mwongozo huu unajumuisha tabia ambayo, kwa maoni yetu, inaweza kuathiri biashara au sifa yetu au kuharibu vibaya uhusiano na imani ya kikazi kati yetu. Ifuatayo ni mifano ya mambo ambayo kwa kawaida huonekana kuwa ukiukaji wa mwongozo huu na/au Vigezo na Masharti ya Dereva:
● wizi au ulaghai
● mashambulizi ya kimwili, uonevu, ukatili wa ngono au matendo mabaya ya kingono
● viwango vya juu vya kughairi
● uharibifu mbaya na wa makusudi wa mali
● matumizi mabaya ya mali au jina la Uber
● ubaguzi, udhalilishaji au unyanyasaji kinyume cha sheria
● kuiletea Uber sifa mbaya zaidi
● kukosa uwezo wa kufanya kazi kutokana na pombe au dawa za kulevya
● kusababisha hasara, uharibifu au jeraha kutokana na uzembe mkubwa
● ukiukaji wa wajibu wowote wa kisheria uliowekwa kwa ajili ya ukodishaji wa binafsi au kwa madereva wa teksi; na
● ukiukaji wa sheria za afya na usalama, ikiwemo kuendesha gari kwa namna hatari na mienendo mingine ambayo inahatarisha usalama wa wasafiri
Orodha hii imekusudiwa kuwa mwongozo na si kamili.
SEHEMU YA 5
Mwongozo wa ziada kwa matarishi
Mbali na kufuata mwongozo wa jumla uliowekwa katika Sehemu ya 2, matarishi wanaochagua kutumia mfumo wa Uber Eats sharti wafuate mwongozo ulio hapa chini unaotumika kwa oda na usafirishaji wa Uber Eats.
Usafirishaji wa oda (taarifa kwa wasafirishaji)
Migahawa inaweza kutunga mwongozo maalum wa usafirishaji unaohimiza usalama wa chakula, kuzingatia mwongozo wa kanuni au kukidhi masharti ya lishe ya mtumiaji wa Uber Eats. Kwa mfano, wauzaji wanaweza kumwarifu tarishi ili asichanganye chakula halal na kisicho halal au oda zilizokusanywa kutoka kwa wauzaji tofauti wa Uber Eats. Matarishi wanapaswa kufuata mwongozo kama huo kutoka kwa wauzaji kila wakati.
Lazima tarishi atumie mfuko wa kuhifadhi ili kutoa huduma salama na safi ingawa matarishi hawalazimiki kutumia bidhaa zilizo na chapa ya Uber Eats. Matarishi lazima pia wadumishe usafi wa binafsi na wa vifaa ili kuhakikisha usalama wa chakula.
Matarishi wanapaswa kusafirisha oda kwa usalama na kulingana na viwango na sheria husika za usalama (ikiwemo usalama wa chakula). Kwa mfano, hawapaswi kuharibu au kufungua vifurushi wakati wa kusafirisha au hawapaswi kusafirisha chakula kilichomwagika au kilichoharibika.
Pombe na bidhaa zilizowekewa masharti
Ni kinyume cha sheria kumuuzia mtu yeyote aliye na umri wa chini ya miaka 18, au mtu yeyote aliyelewa bidhaa inayodhibitiwa. Matarishi wana jukumu la kufuata masharti ya usafirishaji wa pombe katika eneo husika, ambayo yanaweza kuwataka watumiaji wa Uber Eats kuonesha kitambulisho na kutompatia mtumiaji wa Uber Eats pombe ikiwa hajatimiza umri unaotakiwa kisheria au ikiwa anaonekana kuwa amelewa.
Haki ya kubadilisha / kutumia akaunti pamoja
Unaweza kuchagua kumwomba mtu mwingine asafirishe chakula kwa niaba yako wakati wowote unaposafirisha chakula. Ukiamua kufanya hivyo, kumbuka kwamba bado unawajibikia shughuli zote zinazofanywa kwenye akaunti yako, iwe ni wewe au mtu mwingine.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali rejelea sera ya kubadilishana hapa.
SEHEMU YA 6
Mwongozo wa ziada kwa wauzaji
Mbali na kufuata mwongozo wa jumla uliowekwa katika Sehemu ya 2, wauzaji wanaochagua kutumia mfumo wa Uber Eats sharti wafuate viwango vilivyo hapa chini vinavyotumika kwa ajili ya oda na usafirishaji wa Uber Eats pamoja na sera zetu za ziada zilizo hapa, ambazo zinaweza kubadilishwa mara kwa mara.
Jinsi ya kuandaa na kusafirisha oda vizuri
Wauzaji wanapaswa kutimiza masharti yote ya leseni na kanuni na sheria nyingine zozote zinazohusu vyakula na vileo—zikiwemo kanuni za usafi na usalama wa chakula—pamoja na mbinu bora zinazotumika katika sekta na sera za Uber. Muhimu zaidi, Wauzaji wanawajibika kuhakikisha kuwa bidhaa wanazouza ni salama na zinatii sheria na kanuni. Wauzaji ni sharti wawe na leseni na/au vibali halali panapohitajika kisheria na sharti wazingatie sera yetu ya tathmini ya usafi wa chakula.
Vyakula vingi vinavyopikwa huharibika haraka na vinaweza kusababisha magonjwa kama havitatunzwa vizuri. Vyakula kama hivi vinaweza kudhuru afya visipowekwa kwa muda na hali joto inayostahili kabla ya kuchukuliwa.
Ili kusaidia kuhakikisha kuwa chakula kinawafikia watumiaji wa Uber Eats kikiwa salama, wauzaji wanatakiwa wafungashe vizuri kabla ya usafirishaji. Wauzaji wanatarajiwa kuzingatia maelezo wanayopewa na watumiaji wa Uber Eats yanayohusu mizio ya chakula, vyakula visivyokubaliwa au masharti mengine ya lishe na wasikubali maombi ya oda ambayo hawawezi kuyatimiza. Wauzaji lazima wahakikishe kwamba wanatii sera ya Uber Eats ya mizio - hapa. Tafadhali angalia pia sehemu ya ‘utoaji wa taarifa’ hapa chini.
Utoaji wa taarifa
Una jukumu la kisheria la kuhakikisha kwamba maelezo fulani, ikiwa ni pamoja na lakini si tu, mizio na kiwango cha kalori, yanaoneshwa kwenye menyu katika programu ya Uber Eats. Ikiwa kuna masharti ya kisheria ya kutupatia taarifa kama hizo, ni lazima utupe maelezo haya kwa wakati unaofaa na uhakikishe kuwa ni sahihi na yanasasishwa mara kwa mara.
Ni muhimu pia utupe maelezo tunayoomba kuhusu biashara yako na utufahamishe kuhusu mabadiliko yoyote ya maelezo hayo kwa wakati unaofaa. Kwa mfano, tunafaa kujua ikiwa umiliki wa biashara yako umebadilika, ikiwa tathmini yako ya usafi wa chakula itabadilika au tunahitaji maelezo fulani kutoka kwako ili kutii kanuni za benki na malipo. Usipotupa maelezo tunayohitaji kuhusu biashara yako, hali hii inaweza kusababisha kufungwa kwa akaunti yako ya Muuzaji.
Jinsi ambavyo wauzaji wanaweza kudumisha mazingira salama ya kuchukua oda
Wauzaji na wafanyakazi wao wanatakiwa kufanya maamuzi bora na kuwajali matarishi ili kuwafanya wahisi vizuri, jinsi wanavyowachukulia wateja wao binafsi. Pia, wanapaswa kuwa na eneo salama la kuchukua oda; kwa mfano, wauzaji wanapaswa kujitahidi kuzuia matukio kwenye maeneo ya biashara ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa matarishi.
Kudumisha huduma bora kwa matarishi na watumiaji wa Uber Eats
Ni muhimu wauzaji waheshimu matarishi na watumiaji wa Uber Eats. Wauzaji wanapaswa kuwa makini ili kutayarisha na kuweka vyakula sahihi kwenye oda ya mteja wa Uber Eats. Mteja wa Uber Eats akipokea bidhaa zisizofaa, inaweza kusababisha huduma mbaya.
Kuchukua muda mrefu kuandaa chakula, muda mrefu kuchukua oda (muda anaochukua tarishi kuingia na kutoka kwenye eneo la mfanyabiashara akiwa na oda, ikiwa ni pamoja na muda wa kusubiri), muda wa chini wa mtandaoni (muda wa muuzaji kupatikana mtandaoni), kuchukua muda mrefu kabla ya kukubali oda na viwango vya juu vya kughairi pia huwapa huduma mbaya watumiaji na matarishi wa Uber Eats.
Ikiwa vipimo hivi, au vingine, ni vibaya zaidi kuliko wastani wa mji wa muuzaji, vinaweza kuathiri vibaya huduma za washirika wengine kwenye mfumo wa Uber Eats, kwa hivyo vipimo vya muuzaji vinapaswa kuwa angalau wastani wa mji wake. Ikiwa vipimo vya muuzaji viko chini ya kiwango cha chini zaidi, tutamjulisha.
Bidhaa zilizopigwa marufuku
Wauzaji wanaweza tu kutoa bidhaa za mauzo moja kwa moja kulingana na makubaliano yao na Uber. Huruhusiwi kuweka bidhaa maalum zinazodhibitiwa au zisizo halali, kulingana na sheria na kanuni husika, kwenye menyu ya Uber Eats ya muuzaji. Uber inaweza kuondoa—au vinginevyo kuzuia uwezo wa muuzaji kuchapisha kwenye—menyu ya Uber Eats ya muuzaji, bidhaa zozote ambazo Uber inachukulia kuwa zimepigwa marufuku au hazifai.
SEHEMU YA 7
Mwongozo wa ziada kwa watumiaji wa Uber Eats
Mbali na kufuata mwongozo wa jumla uliowekwa katika Sehemu ya 2, watumiaji wa Uber Eats wanaochagua kutumia mfumo wa Uber Eats sharti wafuate mwongozo ulio hapa chini unaotumika kwenye oda na usafirishaji wa Uber Eats.
Ukiomba kusafirishiwa chakula kwa niaba ya mtu mwingine mzima, utawajibikia tabia yake baada ya kupokea chakula hicho.
Bidhaa zenye masharti
Oda zote zilizo na bidhaa zenye masharti (kwa mfano, pombe au tumbaku) lazima zitii sheria na masharti yoyote ya usafirishaji wa nje duka na saa za huduma. Ni watumiaji wa Uber Eats walio na umri unaoruhusiwa kisheria kununua bidhaa zenye masharti au walio na umri wa juu, na wasio walevi ndio wanaoweza kuagiza na kupokea bidhaa zinazodhibitiwa, inapopatikana. Watumiaji wa Uber Eats wanaweza kuombwa wathibitishe umri na utambulisho, hatua inayoweza kujumuisha kuonesha kitambulisho chenye picha, kilichotolewa na serikali wakati pombe, tumbaku au bidhaa nyingine inayodhibitiwa inawasilishwa kwao. Ikiwa mtumiaji wa Uber Eats hana kitambulisho sahihi cha picha kilichotolewa na serikali anapoombwa, au anaonekana kuwa amelewa, hatakabidhiwa oda na inaweza kurudishwa kwa muuzaji kwa niaba ya mtumiaji wa Uber Eats kwa gharama ya mteja husika wa Uber Eats. Watumiaji wa Uber Eats hawawezi kuweka oda ya pombe ipelekwe kwenye sehemu ya umma ambapo haparuhusu vifaa vifunguliwe, au katika maeneo mengine yoyote ambayo hayaruhusu kubeba au kunywa pombe.
SEHEMU YA 8
Jinsi Uber inavyotekeleza mwongozo wetu
Kupoteza idhini ya kutumia Mfumo wa Uber kunaweza kuathiri maisha au biashara yako. Ndiyo maana tunaamini kwamba ni muhimu kuwa na sera zinazofafanua wazi matukio yanayoweza kufanya uzuiwe kutumia Mfumo wa Uber. Ukikiuka vigezo vyovyote vya mkataba wako na Uber, au vigezo na sera zozote husika, ikiwemo sehemu yoyote ya mwongozo huu au sera na viwango vya ziada ambavyo tunakujulisha mara kwa mara, unaweza kupoteza uwezo kiasi au wote wa kutumia Mfumo wa Uber. Ikiwa una zaidi ya akaunti moja za Uber, kama vile akaunti ya msafiri na ya dereva, ukiukaji wa mwongozo pia unaweza kusababisha upoteze uwezo wa kutumia akaunti zote za Uber. Ikiwa unaamini kwamba kuna hitilafu iliyofanya usiweze kutumia akaunti yako, unaweza kuwasiliana na timu ya Huduma kwa Wateja wa Uber.
Uber hupokea maoni kwa njia mbalimbali na ripoti za maoni zinazowasilishwa kwa timu yetu ya Huduma kwa Wateja ambazo zinaonesha kuwa huenda kuna ukiukaji wa mwongozo huu. Uber inaweza kufanya uchunguzi kupitia timu maalum, au ikihitajika, mashirika ya kutekeleza sheria. Tukifahamishwa kuhusu matendo yanayoweza kusababisha matatizo, tunaweza kuwasiliana nawe ili tuweze kuyachunguza.
Kupoteza idhini ya kutumia sehemu zote au sehemu ya Mfumo wa Uber kunaweza kutokana na ripoti za ukiukaji wa mwongozo huu na pia baadhi ya hatua unazoweza kuchukua nje ya Mfumo wa Uber. Uber inaweza kupokea taarifa kutoka kwenye mfumo mwingine na mamlaka katika eneo husika - ikiwa tutabaini kuwa kuna ripoti zinazotishia usalama wa jumuiya ya Uber, wafanyakazi wetu, wafanyakazi na wakandarasi, au kusababisha madhara kwa chapa, sifa au biashara ya Uber, basi ufikiaji wa programu ya Uber unaweza kudhibitiwa. Ikiwa matukio yaliyoripotiwa yalikuwa makubwa au ya kurudiwa, au ukikataa kushirikiana nasi, unaweza kupoteza uwezo wa kutumia Mfumo wa Uber. Matendo yoyote yanayohusisha ukatili, unyanyasaji wa ngono, udhalilishaji, ulaghai, ubaguzi, au shughuli za udanganyifu, haramu au zisizo salama unapotumia Mfumo wa Uber yanaweza kufanya upoteze uwezo wa kutumia Mfumo wa Uber. Vilevile, watekelezaji wa sheria wanapohusika, tutashirikiana nao katika uchunguzi kulingana na Mwongozo wetu wa Utekelezaji wa Sheria.
Tunaweza, kwa hiari yetu, kusimamisha akaunti yako au ‘kusitisha’ akaunti yako hadi tutakapokamilisha uchunguzi wetu.
Utoaji wa baadhi ya huduma, zikiwemo huduma za usafiri wa pamoja, kwenye Mfumo wa Uber unadhibitiwa nchini Uingereza. Ikiwa tutabaini kuwa akaunti yako ya dereva au tarishi haitii masharti husika au sheria, tunaweza kuondoa uwezo wako wa kutumia Mfumo wa Uber.
Mwishowe, madereva na matarishi wanaotaka kutumia Mfumo wa Uber wanaweza kufanyiwa uchunguzi, ikiwemo ukaguzi wa rekodi ya gari na uchunguzi wa tabia kama inavyotakiwa. Dereva au tarishi atapoteza uwezo wa kutumia akaunti zake za Uber ikiwa ukaguzi wa rekodi ya gari, historia ya uhalifu au ukaguzi mwingine utagundua ukiukaji wa mwongozo wa Uber au vigezo vingine vinavyotakiwa na wasimamizi wa eneo husika.
Maelezo zaidi kuhusu hali zinazoweza kusababisha akaunti ya dereva ifungwe yanapatikana katika Sehemu ya 3 ya mwongozo huu.
Chagua lugha ambayo unapendelea
About