Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Changia Nauli

Unaposafiri pamoja na marafiki au makundi ya watu, unaweza kuchangia nauli. Hamna haja ya kulipa kwa pesa taslimu. Iambie App ikufanyie hesabu kisha ikutumie bili.

Umuhimu wake

Safiri pamoja na marafiki

Ni bora zaidi mkiwa wasafiri wengi. Safiri pamoja na marafiki zako ili wachangie nauli.

Ruka sehemu ya malipo ya pesa taslimu

Gawa gharama ya safari moja kwa moja kupitia App. Ni rahisi na haina usumbufu wowote.

Utaratibu wake

Itisha usafiri

Gusa ili ufungue app na uitishe usafiri kama kawaida.

Tafadhali kumbuka: sharti uwe na toleo jipya la App ili utumie kipengele cha Kuchangia Nauli.

Changia

Baada ya kuitisha usafiri, telezesha kidole juu kutoka sehemu ya chini ya App yako, gusa njia ya kulipa uliyochagua, kisha uguse Changia Nauli.

Chagua marafiki zako

Weka majina au namba za simu za wasafiri wengine. Kila mtu utakayeongeza atatumiwa ombi la kukubali mwaliko wako.

Maswali yanayoulizwa sana

  • Ndiyo. Gharama ya safari inagawanywa kwa kiasi sawa miongoni mwa wasafiri wanaokubali mwaliko wa kuchangia nauli.

  • Ndiyo. Wakati wa kuchangia nauli, kila msafiri anayehusika hutozwa ada ya senti 25. Stakabadhi yako itaonesha ada yote ya nauli iliyochangwa na wasafiri wote.

  • Ikiwa msafiri hatakubali kuchangia nauli au hana njia halali ya kulipa, utatozwa ada yote.

  • Ikiwa unatumia Apple Pay lakini bado unataka kuchangia nauli, huenda ukahitaji kutumia njia nyingine ya kulipa. Unaweza kubadilisha utumie Apple Pay kwenye safari yako inayofuata.

Jisajili

Pakua App na uweke mipangilio ya akaunti yako ili uwe tayari wakati ujao utakapohitaji usafiri.

Onesha

Waalike marafiki watumie Uber na watapata punguzo kwenye safari yao ya kwanza.

Aina za usafiri hubadilika kulingana na jiji na eneo lako.

Ikiwa msafiri hatakubali kuchangia nauli au hana njia halali ya kulipa, utatozwa ada yote. Ofa zinazotumika kwenye akaunti yako zitatumika kwenye mgawo wa nauli yako pekee.

Huduma ya kuchangia nauli haipatikani katika aina zote za usafiri wa Uber. Tafadhali kumbuka kwamba huwezi kuchangia nauli baada ya safari kuisha.