Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kuunda timu anuwai ili kuhudumia tovuti yenye uanuwai

Kwenye tovuti ya Uber, idadi kubwa ya watu tofauti hutangamana katika safari zetu milioni 19 kwa siku. Tunahitaji kuunda huduma zetu na kuendesha biashara yetu kwa njia ambayo inaonyesha jumuiya mbalimbali tunazohudumia. Hiyo inamaanisha kwamba ni muhimu kwa wafanyakazi wetu wa ndani kuonyesha uanuwai uliopo kwenye tovuti yetu na kwetu sisi kukuza mazingira ambapo uanuwai huo unastawi na mahali ambapo watu wanahisi kukubalika na wanaweza kuchangia mafanikio yetu ya pamoja.

Kwa kufanya mabadiliko ya hatua kwa hatua na endelevu kadiri muda unavyokwenda, Uber imeunda upya msingi kuanzia chini hadi juu na kubadilisha kabisa utamaduni wetu. Miaka mitano baadaye, tayari tunaona jinsi uanuwai unavyotufanya tuwe na nguvu na kutuwezesha kutengeneza mazingira yenye usawa na jumuishi ili kuuboresha ulimwengu.

Ahadi ya uongozi ya kuleta uanuwai

Tumejizatiti kuongeza uanuwai wa watu katika Uber na kuwa kampuni inayopinga ubaguzi wa rangi na mshirika kwa jumuiya tunazohudumia. Timu yetu ya Uongozi wa Utendaji inafanya sehemu yake ili kufanikisha jambo hili kupitia kuweka malengo kuhusu uwakilishi kwenye timu zao na kufuatilia maendeleo mara kwa mara. Mwaka 2020, pia tulitoa ahadi za umma za kupinga ubaguzi wa rangi ili kuongeza juhudi zetu kupitia huduma na ushirikiano wetu na kwa watumiaji wote kwenye tovuti yetu. Tunasimamia na kufuatilia ahadi hizi kikamilifu na tunaendelea kupiga hatua kwa zote.

“Tunajua kwamba maendeleo huchukua muda, lakini si ukosefu wa suluhisho ambao hupunguza kasi yetu; kampuni hupata changamoto za kufanya maendeleo wakati hazina ujasiri wa kujizatiti na kupinga ubaguzi wa rangi na tabia za ukuu wa Watu Weupe. Watu na kampuni hupoteza motisha wakati hawaoni mabadiliko ya haraka. Lakini mabadiliko ya polepole ni endelevu zaidi. Ukosefu wa usawa na ubaguzi wa rangi haukuibuka mara moja na hauwezi kurekebishwa kwa suluhisho rahisi. Kazi haikamiliki kamwe. Ninaamini kwamba tukiendelea kujizatiti, mabadiliko yatatokea. Uber sikuzote imekuwa na ujasiri wa kujizatiti kwa hatua endelevu na kulingana nami hayo ni mafanikio ya mwanzoni.”

Bo Young Lee, Ofisa Mkuu wa Uanuwai na Ujumuishaji

“Kama kampuni inayoendeleza usafiri, lengo letu ni kuhakikisha kwamba kila mtu anaweza kusafiri kwa uhuru na kwa njia salama zaidi, iwe kimwili, kiuchumi au kijamii. Ili kufanya hivyo, lazima tusaidie kupambana na ubaguzi wa rangi ambao unaendelea katika jamii na kuwa bingwa wa usawa, ndani na nje ya kampuni yetu.

“Jambo moja ni wazi kwetu: hatuwezi tu kutumaini kwamba huduma zetu pekee zitaboresha usawa na haki. Lazima tutumie upana wetu wa kimataifa, teknolojia yetu na takwimu zetu ili kusaidia kufanya mabadiliko, haraka—ili tuwe kampuni ya kupambana zaidi na ubaguzi wa rangi; kampuni na tovuti salama na jumuishi zaidi na mshirika mwaminifu kwa jumuiya zote tunazohudumia.”

Dara Khosrowshahi, Afisa Mkuu Mtendaji

Wanaojiweza katika Uber

Jumuiya ya Uber ya walezi na wafanyakazi wenye ulemavu

Mwasia katika Uber

Jumuiya ya Waasia ya Uber

Watu Weusi katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wafanyakazi na washirika Weusi

Usawa katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya ujumuishaji wa kijamii na kiuchumi

Wahamiaji katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wahamiaji

Mchangamano wa Imani Mbalimbali katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya watu wa imani na tamaduni anuwai za kiroho

Los Ubers

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wafanyakazi na washirika wa Kihispania na Amerika Kusini

Wazazi katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wazazi na walezi

Watu wenye hekima katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wafanyakazi wa vizazi vyote

Wanajeshi waliostaafu katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wanajeshi waliostaafu

Wanawake katika Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wanawake

Ripoti za kila Mwaka za Watu na Utamaduni

Kila mwaka, tunachapisha Ripoti yetu ya Watu na Utamaduni ili kushiriki mtazamo wetu wa usimamizi wa mtaji wa binadamu; uanuwai, usawa, ujumuishaji na utamaduni. Tunashiriki takwimu zilizosasishwa za uwakilishi na kuonyesha jinsi tunavyoendelea dhidi ya malengo yetu. Ripoti hiyo ni sehemu muhimu ya mtazamo wetu wa kuongeza uwazi kuhusu takwimu za wafanyakazi wetu na mazoea ya mtaji wa binadamu. Tazama ukurasa wa Ripoti yetu ya Watu na Utamaduni kwa taarifa zaidi.

Kuwa mwajiri wa fursa sawa

Ripoti ya EEO-1, pia inajulikana kama ripoti ya taarifa ya mwajiri, imepewa mamlaka na serikali ya shirikisho ya Marekani na inahitaji kampuni kuripoti takwimu za ajira kulingana na mbari/kabila, jinsia na aina ya kazi.

Ripoti hii inatumiwa kuhakikisha uanuwai unaofaa na fursa sawa kwa wafanyakazi wetu wote—kimsingi ni mkakati wa wafanyakazi wa Uber nchini Marekani kwa wakati mahususi. Kukuza mahali pa kazi penye wafanyakazi wa aina mbalimbali husaidia biashara yetu kufikiria kwa makini kuhusu malengo yake kulingana na mkakati wetu mpana wa DEI. Tunachagua kufanya ripoti hii ipatikane kwa umma kama sehemu ya ahadi yetu inayoendelea ya kuongeza uwazi na maelezo ya kina kuhusu takwimu za kidemografia za wafanyakazi wetu.

1/3

Uber inajivunia kuwa mwajiri wa fursa sawa/anayepinga ubaguzi. Waombaji wote wa kazi wanaofuzu watazingatiwa kwa ajira bila kuzingatia jinsia, utambulisho wa kijinsia, mwelekeo wa kingono, mbari, rangi, dini, asili ya kitaifa, ulemavu, hadhi inayolindwa ya kustaafu kwa mwanajeshi, umri au sifa nyingine yoyote inayolindwa na sheria. Aidha, tunazingatia waombaji wa kazi wanaofuzu bila kujali historia ya uhalifu, sambamba na matakwa ya kisheria. Angalia pia nyongeza ya “Fursa Sawa ya Ajira ni Sheria”, “EEO ni Sheria” na “Sharti la Kutobagua Uwazi wa Malipo.” “Sharti la Kutobagua Uwazi wa Malipo.” Ikiwa una ulemavu au hitaji maalumu ambalo linahitaji kushughulikiwa, tafadhali tufahamishe kwa kujaza fomuhii

DEI na maisha katika Uber

Angalia ukurasa wetu wa kazi ili upate taarifa zaidi kuhusu jinsi ilivyo kufanya kazi kwenye Uber