Ufikivu kwa kutumia Uber
Teknolojia yetu na usafiri unaotolewa na madereva umebadilisha usafiri wa watu wengi wenye ulemavu, na tumejitolea kuendeleza teknolojia zinazounga mkono uwezo wa kila mtu kusafiri katika jumuiya zake.
Wasafiri walio na ulemavu
Teknolojia ya Uber inasaidia kuongeza usafiri na kujitegemea kwa wasafiri walio na ulemavu, kupitia vipengele na uwezo kama ifuatavyo:
Malipo ya kielektroniki
Chaguo la malipo kiotomatiki ya Uber inarahihisha mchakato wa kulipa, hivyo kuwapunguzia wasafiri wasiwasi wa kuhesabu pesa na kulipa dereva moja kwa moja.
Usafiri unapohitajika
App ya Uber inarahisisha usafiri wa walio na ulemavu kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kubofya kitufe tu. Si lazima wapange safari kupitia mratibu au kuamua kutumie mbinu nyingine, isiyo rahisi, ya kupata usafiri.
Kujua nauli mapema
Uber hutumia kipengele cha kujua nauli mapema ili kuwajulisha wasafiri kiasi cha nauli kabla ya kuitisha usafiri. Jambo hili linawapa utulivu na kupunguza uwezekano wa kulaghaiwa.
Sera dhidi ya ubaguzi
Msafiri anakutanishwa kiotomatiki na dereva aliye karibu kwenye App ya Uber kila anapoitisha usafiri, hivyo basi kupunguza fursa ya ubaguzi, hali ambayo inaathiri usafiri salama na nafuu.
Sera za wanyama wa kutoa huduma
Kwa wasafiri walio na ulemavu wa kuona au wasioona vizuri, na huenda wanasafiri na wanyama wa kutoa huduma, Mwongozo wa Jumuiya ya Uberna Sera ya Wanyama wa Kutoa Huduma inawahitaji madereva kuzingatia sheria zote zinazohusu usafirishaji wa wanyama wa kutoa huduma.
Shiriki Muda Utakaowasili na eneo
Wasafiri wanaweza kuonesha ndugu na marafiki maelezo ya safari kwa urahisi, yakiwemo barabara mahususi na muda anaokadiriwa kuwasili, ili kupunguza wasiwasi. Marafiki au ndugu watapokea kiungo ambacho wanaweza kuona jina, picha na maelezo ya gari la dereva na kufuatilia mahali ambapo msafiri yuko katika ramani moja kwa moja hadi atakapowasili aendako. Haya yote yanafanyika bila kupakua App ya Uber.
Wasafiri wenye ulemavu wa kutembea
Tunatumia teknolojia kufanya safari ifanyike kwa urahisi zaidi na wasafiri wenye ulemavu wa kutembea, ikiwemo kupitia WAV (magari yanayoweza kupandwa kwa kutumia viti vya magurudumu).
Magari yenye vifaa
WAV ya Uber inawasaidia wasafiri wanaotumia viti vya magurudumu vyenye injini ambavyo haviwezi kukunjwa, kukutana na madereva katika magari yanayoweza kupandwa kwa kutumia viti vya magurudumu kwa kutumia lifti na njia za walemavu.
Hupatikana duniani kote
Tunatumia aina mbalimbali za WAV katika miji kote ulimwenguni (ikiwemo Bangalore, Boston, Chicago, London, Los Angeles, New York, Philadelphia, San Francisco, Toronto na Washington, DC) kuamua aina ya magari yanayoweza kupandwa kwa kutumia viti vya magurudumu na yanayowafaa wasafiri na madereva zaidi.
“Kwa kuanzisha [WAV], Uber inawapa watu wanaohitaji magari yanayoweza kupandwa kwa kutumia viti vya magurudumu fursa ya kuitisha safari inapohitajika kwa kubonyeza tu kitufe. Kama shirika linalofanya kazi kuboresha maisha kwa watu walio na ulemavu, ninapongeza Uber kwa kupanua chaguo kwa watu wanaohitaji magari yanayoweza kupandwa kwa kutumia viti vya magurudumu.”
—Eric Lipp, Mkurugenzi Mtendaji, Shirika la Open Doors
“UberX imebadilisha maisha ya mamilioni ya watu wanaosafiri kote ulimwenguni, na ni-nafurahia kuona Uber ikitumia ubunifu huu kuwapa wateja chaguo na fursa zaidi…. WAV itawawezesha watu wanaohitaji magari yanayoweza kupandwa kwa kutumia viti vya magurudumu kupata usafiri wanapohitaji kwa kubofya tu kitufe.”
—Tony Coelho, Mwandishi-mwenza, Sheria ya Wamarekani walio na Ulemavu
“Ninaamini kuwa Uber imekuwa mfumo bora zaidi wa kuendeleza huduma ya usafiri kwa ajili yangu na watu wengine walio na ulemavu wa kuona katika karne hii.”
—Mike May, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, BVI Workforce Innovation Center, Envision Inc.
Wasafiri walio na matatizo au ulemavu wa kusikia
Kipengele cha sauti hakihitajiki katika utendakazi wa App ya Uber. Teknolojia ya usaidizi kama vile arifa za kuonekana na kutetemesha simu zinaweza kusaidia wasafiri walio na matatizo au ulemavu wa kusikia kutumia App ya Uber kwa urahisi, na vipengele kwenye App, kama vile vya kuweka mahali unakoenda, vinaweza kutekeleza mawasiliano yasiyo ya kimazungumzo kati ya msafiri na dereva.
Wasafiri wanaohitaji usaidizi
Katika Uber, tunajitahidi kuongeza upatikanaji wa huduma za usafiri kwa kila mtu, mahali popote. Assist imebuniwa kusaidia watu wanaohitaji usaidizi zaidi. Kupitia Assist, madereva wa ukadiriaji wa juu wanaweza kupokea mafunzo kutoka kwa mashirika mengine ili kuwasaidia wasafiri kuabiri magari. Assist sasa inapatikana katika zaidi ya miji 40 kote duniani.
Wateja wa Uber Eats walio na ulemavu
Wateja walio na ulemavu wa kuona
Kupitia iOS VoiceOver na Android TalkBack, App ya Uber Eats inawasaidia wateja wa Uber Eats walio na matatizo au ulemavu wa kuona, kuagiza chakula kwenye migahawa kwa kubonyeza tu kitufe. Angalia jinsi ya kutumia App ya Uber Eats kwa kutumia vipengele hivi vya ufikivu.
Wateja walio na matatizo au ulemavu wa kusikia
Kipengele cha sauti hakihitajiki katika utendakazi wa App ya Uber Eats. Teknolojia ya Usaidizi kama vile arifa za kuonekana na kutetemesha simu zinaweza kusaidia wasafiri walio na matatizo au ulemavu wa kusikia, kutumia App ya Uber kwa urahisi. Vipengele kwenye App, kama vile uwezo wa kuweka eneo la usafirishaji, vinaweza kutekeleza mawasiliano yasiyo ya kimazungumzo kati ya mteja na msafirishaji.
Madereva wenye ulemavu
Madereva wenye ulemavu wa kutembea
Uber inatoa fursa za kiuchumi kwa watu wenye ulemavu wa kutembea. Uber inawakaribisha madereva wanaotumia magari yanayoweza kudhibitiwa kwa mikono ili watumie mfumo wa Uber. Mtu yeyote anayefikisha umri wa kuendesha gari anaweza kujisajili kuendesha gari kwenye mfumo wa Uber.
Madereva walio na matatizo au ulemavu wa kusikia
Uber inapanua fursa rahisi za kiuchumi kwa madereva walio na matatizo au ulemavu wa kusikia. Kila mwezi, maelfu ya madereva wa Uber walio na matatizo na ulemavu wa kusikia husafirisha watu wengi zaidi kuliko madereva wengine kwa wastani. Madereva walio na matatizo au ulemavu wa kusikia wamepata mamilioni ya pesa kwa kuwasafirisha watu katika jamii zao.
Mnamo Septemba 2016, Uber ilituzwa na Ruderman Family Foundation kuwa miongoni mwa kampuni 18 zinazoongoza katika kuwasaidia watu wenye ulemavu.
“Uber imejumuisha teknolojia ya ufikivu kwa Walio na matatizo na ulemavu wa kusikia katika App yao, hivyo basi kufanikisha ufikivu wa kiwango cha juu kwa jumuiya ya Watu Walio na Matatizo ya Kusikia, watengeneze pesa kwa kuendesha gari katika Uber. Ushirikiano huu na CSD utatoa fursa rahisi kwa madereva Wenye Ulemavu wa kusikia za kusafirisha watu. Ni fursa ya kukutanisha watu na kuzua mtazamo mpya wa uwezo na utu kwa Walio na Ulemavu wa Kusikia.”
—Chris Soukup, Afisa Mkuu Mtendaji, Communication Service for the Deaf
Bidhaa inaangazia madereva wenye ulemavu au matatizo ya kusikia
Isitoshe, tumeshirikiana na Communication Service for the Deaf, ambayo ni asasi kuu kabisa isiyo ya faida nchini Marekani, ili kuongeza fursa kwa wanaume na wanawake walio na ulemavu wa kusikia. Tumeshirikiana pia na wanachama wa jumuiya ya watu walio na ulemavu wa kusikia, ikiwemo National Association of the Deaf and Telecommunications for the Deaf and Hard of Hearing (TDI), ili kubuni na kutumia bidhaa nyingi za kuboresha huduma ya madereva, zikiwemo hizi:
Kuwezesha vipengele hivi kwenye App
Madereva wanaweza kujitambulisha kuwa na matatizo au ulemavu wa kusikia kwenye App ya Dereva, inayofungua vipengele vifuatavyo kwa madereva na wasafiri wao.
Ombi la usafiri linalomweka
App ya Madereva hutoa ishara inayomweka na arifa ya sauti ili kuashiria kwamba kuna ombi la usafiri. Hali hiyo huwarahisishia madereva kuona wakati kuna fursa ya kutoa huduma ya usafiri na kupata pesa.
Arifa kwa njia ya ujumbe pekee, badala ya kupiga simu
Msafiri hawezi kutumia kipengele cha kumpigia simu dereva mwenye ulemavu au matatizo ya kusikia. Badala yake, msafiri anaelekezwa kumtumia dereva ujumbe ikiwa angependa kuwasiliana naye. Si rahisi kughairi safari za madereva wanaotumia mipangilio hii ikiwa kuna simu ambayo haikujibiwa.
Ujumbe unaoonyesha msafiri anakoenda
App huweka arifa ya ziada ili kumuuliza msafiri abainishe kituo chake cha mwisho na kumfahamisha kwamba dereva ana ulemavu wa kusikia au ana matatizo ya kusikia. Dereva akiwasha mipangilio hii na akubali ombi la usafiri, msafiri ataona sehemu dhahiri kwenye skrini ya simu ikimuuliza ajaze sehemu anakoenda. Kisha App ya Uber itakuwa na maelekezo ya hatua kwa hatua baada ya safari kuanza.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu vipengele hivi,tazama video hii.
Tuko hapa kukusaidia
Usaidizi na huduma kwa wateja
Tembelea Kituo cha Usaidizi upate maelezo zaidi kuhusu akaunti yako ya Uber, kuona maswali yanayoulizwa sana, au kutoa maoni kuhusu usafiri wako wa hivi majuzi.
Nyenzo za madereva
Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu kuwasafirisha watu wenye ulemavu, angalia nyenzo za madereva.
Kuhusu