Huduma za teknolojia ya Uber
Tunabadilisha jinsi watu wanavyoweza kuitisha usafiri na tumeanza na usafiri wa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
App za Uber, bidhaa na huduma nyingine
Uber ni kampuni ya teknolojia ambayo dhamira yake ni kufikiria upya jinsi ya kufanya usafiri ulimwenguni uwe bora. Teknolojia yetu inatusaidia kubuni na kudumisha tovuti zilizo na sehemu nyingi zinazowakutanisha wateja wanaotafuta safari na watoa huduma za usafiri wanaojitegemea, pamoja na aina nyingine za usafiri, ikiwemo usafiri wa umma, baiskeli na skuta.
Pia tunawaunganisha wateja na migahawa, wauzaji wa vyakula na wauzaji wengine ili waweze kununua na kuuza milo, mboga na bidhaa nyinginezo, kisha tunawakutanisha na watoa huduma wanaojitegemea. Aidha, Uber huwaunganisha wasafirishaji na wachukuzi katika tasnia ya uchukuzi wa mizigo.
Teknolojia yetu huwasaidia watu kuungana na kusafiri katika zaidi ya nchi 70 na miji 10,000 kote ulimwenguni.
Kutumia Uber kupata hela
Fursa inapatikana kila mahali.
Tunakuza miji
Kusaidia kuboresha usafiri wa umma na upatikanaji wa huduma kwa wanaohitaji.
Tunasaidia biashara zipige hatua
Angalia jinsi Uber Freight na Uber for Business husaidia mashirika kote ulimwenguni.
Usafirishaji wa bidhaa wa siku hiyo hiyo
Suluhisho rahisi la kusafirisha bidhaa ambalo huruhusu watu kutuma bidhaa siku hiyo hiyo.
Chaguo maarufu zaidi za usafiri wa Uber
Itisha usafiri, ingia na uende.
Uber WAV
Usafiri katika magari yanayowezwa kupandwa kwa kutumia viti vya magurudumu
Usafirishaji wa chakula unapohitaji
Uber Eats
Agiza kutoka migahawa unayopenda, mtandaoni au ukitumia App ya Uber. Migahawa hiyo itatayarisha chakula ulichoagiza na mshirika wa Uber anayesafirisha chakula, aliyekaribu nawe, atakileta mahali ulipo.
Mikahawa
Uber Eats hukupa manufaa halisi kwenye mgahawa wako. Wakati chakula chako kinaangaziwa katika App, wateja wapya wanaweza kukiona na wateja wako wanaweza kukiagiza mara nyingi zaidi. Washirika wanaosafirisha chakula kwa kutumia App ya Uber husafirisha chakula kwa haraka na kukifikisha kikiwa freshi.
Tengeneza pesa ukitumia mfumo wa Uber
Endesha gari ukitumia Uber
Tumia wakati wako vizuri unapoendesha gari kwenye mtandao mkubwa zaidi wa wasafiri.
Safirisha ukitumia Uber
Tengeneza pesa kwa kusafirisha chakula ambacho watu hutamani, na vitu vingine kwa kutumia App ya Uber Eats—huku ukitembea jiji lako.
Tunakuza miji pamoja
Kusaidia kuboresha usafiri wa umma kwa watu wote
Uber imejitolea kusaidia miji kote ulimwenguni kufanya usafiri wa umma uwe rahisi, bora na unaozingatia usawa.
Kutoa uwezo wa kufikia huduma kwa wanaohitaji
Tumeshirikiana na mashirika ya huduma za afya ili kuwapa wanachama na wagonjwa uwezo wa kufikia huduma kwa kuwapa chaguo za kuratibu safari. Wataalamu wa huduma za afya wanaweza kuratibu usafiri kwa niaba ya wagonjwa na walezi wanaoenda au kutoka kwenye kituo cha matibabu kwa kutumia dashibodi moja.
Tunasaidia biashara zipige hatua
Uber Freight
Uber Freight ni programu isiyo na malipo inayowakutanisha wasafirishaji na matarishi. Matarishi hugusa kitufe ili waweke nafasi ya mizigo wanayotaka isafirishwe. Kwa kutumia kipengele cha nauli utakayolipa, wasafirishaji hujua pesa watakazolipwa.
Uber for Business
Iwe ni usafiri wa wafanyakazi au safari za wateja, Uber for Business hukupa njia rahisi ya kudhibiti mahitaji yako ya usafiri. Mfumo huu umeundwa kwa ajili ya huduma za kikazi. Unakuonyesha vyema shughuli za safari za wafanyakazi, una vipengele vya kutoza, kulipa na kuripoti kiotomatiki.
Nyenzo iliyo kwenye ukurasa huu wa tovuti ni kwa madhumuni ya taarifa pekee na huenda isitumike katika nchi, kanda au jiji lako. Inaweza kubadilika na huenda tukaibadilisha bila kukuarifu.
Kuhusu