Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Wasifu wa Familia

Unaweza kuwalipia uwapendao na ufuatilie hali ya safari na muda watakaowasili kwa urahisi ukiwaalika kwenye Wasifu wa Familia.

search
Weka mahali
Navigate right up
search
Weka mahali unakoenda

Umuhimu wake

Andikisha akaunti nyingi

Mlezi wa mtoto wako. Msaidizi wako. Binamu yako wa pili. Tunaziita Wasifu za Familia, lakini unaweza kumwongeza mtu yeyote unayetaka.

Weka maelezo ya kadi ya benki

Hata kama ndugu na marafiki zako wanaweza kutumia Wasifu za Familia kuwa mbinu yao ya malipo, hawataona maelezo ya kadi yako ya mteja.

Jinsi inavyofanya kazi kwa mratibu wa Wasifu wa Familia.

Ongeza anwani

Bonyeza ili ufungue App, nenda kwenye menyu, chagua Mipangilio, sogeza chini ili Uweke familia yako, na uchague majina mwafaka ambayo ungependa kuongeza. Baada ya kuweka msafiri atakayetumia Wasifu wa Familia, atapokea ombi la mwaliko.

Tafadhali kumbuka: unapaswa kuwa na toleo jipya la App hii ili uweze kutumia Wasifu wa Familia

Wawezeshe unaowapenda waite magari.

Mwalikwa anapokubali mwaliko, anaweza kuanza kuita gari kupitia simu yake kwa kutumia Wasifu wa Familia kama mbinu yake ya malipo.

Tozwa kiotomatiki

Gharama ya safari hii itatozwa kwenye Wasifu wa Familia, na mratibu atapokea stakabadhi kwa kila safari.

Jinsi inavyofanya kazi kwa msafiri wa Wasifu wa Familia

Kubali mwaliko wa Wasifu wa Familia

Fungua mwaliko wa Wasifu wa Familia uliotumwa kupitia barua pepe kisha ukubali.

Tafadhali kumbuka: unapaswa kuwa na toleo jipya la programu hii ili uweze kutumia Wasifu wa Familia

Ufanye kuwa njia yako chaguomsingi ya kulipa

Chagua Wasifu wa Familia iwe njia yako chaguomsingi ya kulipa.

Lipa kwa Kutumia Wasifu wa Familia

Ita gari kwa njia ya kawaida ukitumia Wasifu za Familia kuwa mbinu yako ya malipo.

Maswali yanayoulizwa sana

    1. Nenda kwenye Mipangilio katika App.
    2. Sogeza chini kisha uchague Familia.
    3. Chini ya Mapendeleo, chaguaMalipo ya chaguomsingi.
    4. Unaweza kuchagua njia zilizopo za malipo au uweke njia nyingine ya malipo.
    1. Chagua Mipangilio kwenye menyu ya programu yako.
    2. Sogeza chini hadi kwenye Wasifu kisha ubonyeze upau wa Wasifu wa Familia.
    3. Sogeza chini, gusa kitufe cha Ondoka kwenye Wasifu, na uthibitishe.
    1. Chagua Mipangilio kwenye menyu ya programu yako.
    2. Sogeza chini hadi kwenye Wasifu kisha ubonyeze upau wa Wasifu wa Familia.
    3. Sogeza chini, kisha uguse ndugu unayetaka kumwondoa.
    4. ChaguaOndoa Ndugu na uthibitishe.
    1. Chagua Mipangilio kwenye menyu ya App yako.
    2. Sogeza chini hadi kwenye Wasifu kisha ubonyeze upau wa Wasifu wa Familia.
    3. Sogeza chini, bonyeza Futa Wasifu wa Familia, kisha uthibitishe.

Jisajili

Pakua App na uweke mipangilio ya akaunti yako ili uwe tayari wakati ujao utakapohitaji usafiri.

Onesha

Waalike marafiki watumie Uber na watapata punguzo kwenye safari yao ya kwanza.

Aina za usafiri hubadilika kulingana na jiji na eneo lako.