Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Pongezi za dereva

Mshukuru dereva wako na uwasaidie wasafiri wengine kumfahamu kwa kumpa beji au hata kumtumia ujumbe mfupi wa shurkani.

Kagua pongezi

Nadhifu na Safi

Kwani kuna asiyependa gari safi? Kama dereva wako ametunza gari lake, usibanie, mpongeze.

Huduma Bora

Huduma bora hufurahiwa, lakini huduma murua inafaa pongezi.

Kuzidi Matarajio

Hii ni kwa ajili ya madereva wanaofanya zaidi ya walivyotarajiwa.

Gwiji wa Ramani

Kama dereva wako ni mjuzi wa barabara (anajua njia za mikato), usisite kumpongeza.

Maongezi Mazuri

Kuna nyakati ambapo ungependa kutulia kimya na wakati mwingine utake kupiga gumzo la kusisimua. Ikiwa dereva wako ana mazungumzo ya kuvutia, basi beji hii ni yake.

Huduma Bora

Kila mtu anapenda marupurupu. Inawezekana dereva wako anastahili beji hii kwa kukupatia ubani wa kutafuna, maji ya chupa, vitafunwa na mengineyo.

Shujaa wa Usiku wa Manane

Unaweza kutumia pongezi hii kwa kuwa na safari salama ya kuelekea nyumbani baada ya burudani ya usiku.

Muziki Mtamu

Anacheza muziki unaochangamsha safari. Ikiwa dereva wako anapiga muziki unaokuongoa, tumia beji hii kumjulisha.

Gari Zuri

Si lazima gari liwe la kifahari ndipo dereva apate pongezi hii. Unaweza kumpa dereva beji hii ikiwa gari lake ni safi, linavutia au kila kitu kiko shwari.

Dereva Mwenye Bashasha

Inapendeza kuzungumza naye? Ni mcheshi kwa ujumla? Cheka kisha umtumie pongezi.

Utaratibu wake

Fungua App yako

Baada ya safari, gusa ili ufungue App kisha umtathmini dereva kwa njia ya kawaida.

Pongeza dereva wako

Baada ya kutathmini safari yako, gusa ‘Pongeza dereva wako’, halafu uchague beji inayoendana na pongezi yako.

Hatua za ziada

Ikiwa ungependa kutoa zaidi ya pongezi, unaweza kumpa dereva bakshishi. Pata maelezo ya jinsi ya kumpa dereva bakshishi hapa.

Jisajili

Pakua App na uweke mipangilio ya akaunti yako ili uwe tayari wakati ujao utakapohitaji usafiri.

Onesha

Waalike marafiki watumie Uber na watapata punguzo kwenye safari yao ya kwanza.

Aina za usafiri hubadilika kulingana na jiji na eneo lako.