Fursa iko kila mahali
Tumia wakati wako vizuri unapoendesha gari kwenye mtandao mkubwa zaidi wa wasafiri.
Unapata pesa kwa muda wako
Weka ratiba yako mwenyewe
Wewe ndiye boss. Unaweza kutumia App ya Uber kuendesha gari wakati wowote, usiku au mchana. Badilisha kazi yako isihitilafiane na shughuli zako nyingine za maisha, sio kubadilisha maisha yako ili kutosheleza mahitaji ya kazi yako.
Unapata pesa bila masharti yoyote
Kadri unavyofanya safari nyingi ndivyo unavyopata pesa nyingi. Unaweza kupata nyingi zaidi mahitaji ya gari yakiongezeka.
App itakuongoza katika kila hatua
Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza simu yako tu. Utaongozwa hatua baada ya hatua, utapata mapendekezo yatakayokusaidia kupata pesa nyingi zaidi, na tuko hapa kukusaidia katika kila hatua usiku na mchana.
Anza sasa
Jisajili mtandaoni
Tuambie tu mji unaotaka kuendeshea gari na aina ya leseni uliyo nayo.' 'Tutakutumia barua pepe iliyo na hatua zinazofuata.
Angalia masharti ya kuendesha gari
Watu wengi wametimiza masharti ya kuendesha gari kwenye mfumo wa Uber. Yafuatayo ni mambo unayohitaji kujua ikiwa unaendesha gari mjini Dar es Salaam.
Pata gari
Ni gari gani linalokufaa? Hakikisha linatimiza masharti yetu nchini Tanzania. Pia, kumbuka kuwa utatengeneza pesa zaidi ikiwa bei zako ni nafuu.
Huduma za ziada
Huduma tunazokupatia nchini Tanzania
Pata usaidizi
Tushirikiane kurahisisha safari zote za Uber. Kurasa zetu za usaidizi zinaweza kukusaidia kufungua akaunti, kuanza kutumia programu, kubadilisha nauli na mengine.
Wasiliana nasi
Je, una swali lolote? Utajibiwa. Utahudumiwa kwa namna pekee katika Kituo cha Madereva wa Uber katika ofisi za Dar es Salaam.
Usalama barabarani
App ya Uber ina vipengele vingi vinavyosaidia kulinda usalama wako barabarani sambamba na kujiamini kabla ya safari, wakati wa safari na hata baada ya safari. Ukihitaji usaidizi wowote, Uber ina huduma inayopatikana usiku na mchana ili kukupa usaidizi unaohitaji.
Maswali yanayoulizwa sana
- Ninaweza kuendesha gari katika mfumo wa Uber jijini mwangu?
Uber inapatikana katika mamia ya miji kote ulimwenguni. Gusa hapa chini ili uone ikiwa huduma inapatikana katika mji wako.
- Masharti ya kuendesha gari katika Uber ni yapi?
Down Small Lazima uwe umefikisha umri unaotakikana ili kuendesha gari katika jiji lako, uwe na aina inayokubalika ya usafiri na uwasilishe hati zinazotakikana, ikiwa ni pamoja na leseni halali ya udereva.
- Je, mfumo wa Uber ni salama?
Down Small Tunathamini usalama wako zaidi. Uber ina Timu ya Usalama ya Kimataifa inayojitolea kuhakikisha kuwa tunazuia matukio hatari. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya usalama katika App, pamoja na vipengele vya ulinzi kama vile ufuatiliaji wa GPS na kuficha namba ya simu yako, kwa kufungua kiungo kilicho hapa chini.
- Je, ninatakiwa niwe na gari langu binafsi?
Down Small Ikiwa unataka kuendesha gari katika mfumo wa Uber lakini huna gari, unaweza kupata gari kutoka kwa mmoja wa washirika wetu wa magari au kutoka kwa mmiliki wa magari katika mojawapo ya masoko mahususi. Tafadhali kumbuka kuwa aina za magari zinaweza kutofautiana kulingana na jiji.
App ya Dereva
Ni rahisi kutumia na inaaminika. Programu hii iliundwa na madereva kwa ajili ya madereva. Inakuonesha kila kitu unachohitaji kujua ili uwe dereva ukitumia Uber.
Endesha gari kupitia App
Endesha gari kupitia App
Ofa hii si ahadi au hakikisho kuhusu mapato unayofaa kutarajia siku zijazo. Ofa hii inapatikana tu kwa madereva na wasafirishaji wapya wa chakula kwenye App ya Uber ambao (i) hawajawahi kujisajili hapo awali kuendesha gari au kusafirisha chakula kwa kutumia mfumo wa Uber; na (ii) wanaopokea ofa hii moja kwa moja kutoka kwa Uber na kuiona kwenye kifuatiliaji cha hakikisho katika App ya Uber Driver; (iii) wamepewa idhini ya kuendesha gari au kusafirisha bidhaa kwa kutumia Uber; na (iv) wanaokamilisha idadi ya safari watu au oda zinazoonekana kwenye kifuatiliaji cha hakikisho katika miji walikosajiliwa ndani ya siku zilizobainishwa za usajili. Huenda vigezo na masharti ya ofa kama vile idadi ya safari za watu au oda na zawadi, zikatofautiana kulingana na eneo. Ofa unayohakikishiwa na unayoona kwenye App inachukua nafasi ya pesa zozote ulizohakikishiwa na Uber hapo awali.
Mapato yanayotokana na safari zako (baada ya ada ya huduma na matozo mengine, kama vile ada za jiji au serikali za mitaa) yanahesabiwa katika kipato unachohakikishiwa; bakshishi na ofa zozote unazopata huongezwa kwenye kiasi hicho. Mapato yanayotokana na usafirishaji wa chakula (baada ya ada za huduma na tozo zingine, kama vile ada za jiji au serikali za mitaa) na ofa za Eats Boost hujumuishwa kwenye jumla ya ofa yako; bakshishi na ofa zozote za ziada unazopata huongezwa kwenye kiasi hicho.
Malipo yoyote unayodai yatawekwa kiotomatiki kwenye akaunti yako baada ya kukamilisha safari zinazotakiwa. Kila usafirishaji wa oda au wasafiri huhesabiwa mara moja kwenye idadi ya chini inayotakiwa. Usafirishaji ulioghairiwa wa watu au oda hauhesabiwi. Ofa hii inatumika tu kwa watu walioipokea kutoka Uber (kupitia barua pepe, tangazo, ukurasa wa wavuti au kiungo maalum cha mwaliko) na kutimiza masharti ya ustahiki. Uber ina haki ya kutolipa au kukata malipo ambayo inabaini au inaamini kwamba yalifanywa kimakosa, kwa ulaghai, kinyume cha sheria au yanayokiuka vigezo na masharti ya madereva au masharti haya. Ofa ni ya muda mfupi tu. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.
Kuhusu