Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Wasifu za madereva

Watu wengi wanaotumia mfumo wa Uber kuendesha gari wanaifurahia sana huduma hii. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu dereva wako kwenye wasifu wake, inayojumuisha maelezo ya uhalisia kama vile lugha anayozungumza, mambo anayopenda, na sababu za kuendesha gari.

search
Weka mahali
Navigate right up
search
Weka mahali unakoenda

Umuhimu wake

Wasifu wa dereva una maelezo ya kuvutia. Mbali na tathmini, beji za mafanikio na historia ya safari, unaweza kuangalia pongezi au ujumbe wa shukrani uliotolewa na wasafiri kama wewe. Utafurahia siku na safari yako mkijuana na dereva.

Utaratibu wake

Fungua App

Gusa ili ufungue App na uitishe usafiri kama kawaida.

Angalia wasifu wa dereva

Dereva akikubali safari yako, utaweza kutelezesha kidole chini hadi kwenye kadi inayofungua wasifu wa dereva.

Ongeza kwenye wasifu wa dereva

Kwa safari ulizozipa tathmini ya nyota 5, unaweza kutoa pongezi au ujumbe wa shukrani kwa dereva wako. Maoni haya huonyesha shukrani zako na huwasaidia wasafiri wenzako kupata maelezo kuhusu dereva wao.

Jisajili

Pakua App na uweke mipangilio ya akaunti yako ili uwe tayari wakati ujao utakapohitaji usafiri.

Aina za usafiri hubadilika kulingana na jiji na eneo lako.