Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Weka nafasi ya safari ukitumia Uber mapema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva

Kamilisha mipango yako leo kwa kuweka nafasi ya safari ukitumia Uber kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva. Omba safari hadi siku 90 kabla ya safari yako ya ndege, wakati wowote na siku yoyote ya mwaka.

Mahali unakoenda
Chagua tarehe na saa

Date format is yyyy/MM/dd. Press the down arrow or enter key to interact with the calendar and select a date. Press the escape button to close the calendar.

Selected date is 2023/10/01.

8:03 AM
open

Huenda huduma ya kuweka nafasi isipatikane katika eneo lako la kuchukuliwa

Omba safari kote ulimwenguni

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Njia za kusafiri katika eneo husika

 • Uber Pet

  1-4

  Ride with your pet

 • UberX

  1-4

  Safari za bei nafuu, kila siku

 • Black

  1-4

  High end cars

 • Starehe Electric

  1-4

  Electric cars with extra legroom

 • Raha

  1-4

  Magari mapya zaidi yaliyo na nafasi ya kutosha

 • Teksi

  1-4

  Teksi zisizohitaji kutafutwa

 • Gari aina ya Van

  1-6

  High end cars for 6

 • Kijani

  1-4

  Electric and hybrid vehicles

1/8

Chukua msafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva (GVA)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa GVA linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa Geneva moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la GVA kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Geneva, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Geneva zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli wa Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

 • Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Taarifa zaidi

 • Unaendesha gari ukitumia Uber?

  Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

 • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

  Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Gundua vitu vya kufanya katika vituo vya Uwanja wa Ndege wa Geneva

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva. Uwanja wa Ndege wa Geneva ni mojawapo ya viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi zaidi nchini Uswizi na huhudumia zaidi ya wasafiri milioni 17 kila mwaka.

Unahudumiwa na mojawapo ya wasafirishaji wakuu barani Ulaya na ndio njia rahisi kufika Geneva, maeneo ya karibu na vituo vingi na sehemu nyingi za kupumzika ya Ufaransa, Uswizi na kimataifa. Isitoshe, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva unapatikana takribani kilomita 4 (maili 2.5) kaskazini mwa mji wa Geneva, jambo linalofanya kuwa rahisi kuufikia kwa usafiri wa umma, magari au hata Uber. Magari huchukua takribani dakika 20, kutegemea hali ya foleni, ilhali safari fupi kwenye treni kwenda uwanja wa ndege kutoka katikati ya mji huchukua dakika 6 tu.

Vituo katika GVA

Uwanja wa Ndege wa Geneva una vituo viwili vikuu vya wasafiri: Kituo cha 1 na 2. Kituo cha 1 hutumika sana, kikilinganishwa na cha 2—ambacho ndicho kituo asili cha uwanja huu—kinatumika tu wakati wa msimu wa baridi. Kwa hivyo, kina huduma chache kikilinganishwa na Kituo cha 1, lakini kina kituo cha treni. Kituo cha 1 kimegawanywa katika vituo 5 vidogo: A, B, C, D na F.

Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Kuna migahawa mingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva, kuanzia migahawa midogo hadi hoteli za kifahari, baa na vyumba vya chai. Vyakula kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva vinamfaa kila mtu.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Unaweza kufikia maeneo mbalimbali kwenye uwanja wa ndege kwa miguu, isipokuwa Kituo cha 2, ambacho kiko kando na uwanja mkuu. Unaweza kusafiri kati ya vituo hivi 2 kwa basi.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Kuna maduka mengi ya kufanya ununuzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva, yenye bidhaa zisizolipishwa kodi pamoja na maduka mengi ya nchini na ya kimataifa. Kuna huduma 2 za VIP ambazo zinawawezesha wateja kufikia sebule na kuwaongoza katika sehemu za ukaguzi wa usalama. Huduma za siha bora zinapatikana kwenye uwanja wa ndege, huku kukiwa na vyumba vya kutafakari na vya kuoga. Isitoshe, wasafiri wanaweza kunufaika kwa kutumia maeneo 2 ya watoto kucheza, maeneo yaliyotengewa shughuli za biashara na vyumba vya mikutano.

Kubadilisha sarafu kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Kuna afisi kadhaa za kubadilisha sarafu katika maeneo ya wanaowasili na wanaoondoka kwenye uwanja wa ndege. Mitambo ya benki pia inapatikana kwenye uwanja wa ndege, mingi ikiwapa wasafiri fursa ya kutoa pesa katika sarafu mbalimbali.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa GVA

Takribani hoteli 10 zinapatikana karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva, jambo linazozifanya kuwa chaguo bora kwa wasafiri walio kwenye mapumziko ya muda mfupi na wanaowasili jioni. Utapata hoteli za gharama aina zote katikati mwa mji wa Geneva. Kuna pia chaguo za usafiri kwenda kwenye vituo vya kuteleza kwenye theluji na vyumba maalum katika eneo hilo, iwe nchini Ufaransa au Uswizi.

Maeneo ya kuzuru karibu na GVA

 • Jet d’Eau (Chemchemi ya Maji)
 • Ziwa la Geneva
 • Mont Salève
 • Old Town
 • Saint Pierre Cathedral (St. Peter’s Cathedral)

Pata maelezo zaidi kuhusu GVA hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa kila baada ya kipindi fulani. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au uendeshaji wake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji.