Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Bakshishi inayotolewa ndani ya App ya Uber

Bakshishi ni njia rahisi ya kutoa shukrani. Wasafiri wa Uber na wateja wa Uber Eats wanaweza kutoa bakshishi moja kwa moja katika App baada ya kila safari au baada ya kuletewa chakula.

Utaratibu wake

Ni rahisi sana

Ili uwe na safari njema isiyo na usumbufu, unaweza kuwapa madereva bakshishi wakati unaopenda hadi siku 30 baada ya safari.

Hakuna ada yoyote ya huduma inayotozwa

Bakshishi huwaendea madereva moja kwa moja; Uber haitozi ada ya huduma kwenye bakshishi.

Faragha

Kutoa bakshishi huhusishwa na safari yako, sio jina lako

Pata usafiri unaohitaji wakati wowote

Itisha usafiri, ingia na uende.

search
Weka mahali
Navigate right up
search
Weka mahali unakoenda
search
Weka mahali
Navigate right up
search
Weka mahali unakoenda

Maswali yanayoulizwa sana

  • Si lazima utoe bakshishi. Uko huru kutoa bakshishi na madereva wako huru kuikubali wakati wowote.

  • Njia rahisi ya kumpa dereva bakshishi ni kupitia App. Mwishoni mwa safari yako, utaombwa umtathmini dereva wako. Baada ya kumtathmini, utapewa chaguo la kutoa bakshishi. Unaweza kumpa dereva bakshishi kwa pesa taslimu.

  • Huenda utahitaji toleo jipya la App ili utumie kipengele cha kutoa bakshishi. Pia, huenda baadhi ya madereva hawatakubali bakshishi kupitia App. Unaweza kuwa katika eneo ambako huwezi kutoa bakshishi ndani ya App. Ukipenda, unaweza kumpa dereva wako bakshishi kwa kutumia pesa taslimu.

  • Bakshishi yote. Uber haitozi bakshishi ada zozote.

  • Unaweza kutumia Uber Cash na kadi za zawadi kutoa bakshishi. Hata hivyo, huwezi kutumia ofa kumpa dereva bakshishi.

  • Baada ya safari kukamilika, unaweza kutoa bakshishi ndani ya siku 30 katika App, kwenye riders.uber.com au kupitia stakabadhi ya safari tuliyokutumia kwa barua pepe.

  • Msafiri ambaye aliita gari kwanza ataweza kuchagua kiwango cha bakshishi katika safari. Ikiwa msafiri aliyeita gari kwanza ametoa bakshishi, haitachangiwa na wasafiri wengine.