Sajili, uhifadhi na uwazawadi wafanyakazi wako
Boresha huduma anayopata mfanyakazi kwa faida zinazoweza kubadilika na marupurupu yanayosaidia malengo ya kuajiri, uzalishaji na uhifadhi, yote katika sehemu moja.
Ajiri watu wenye vipaji bora ukitumia Uber for Business
Kwa kutumia tovuti yetu rahisi kutumia, unaweza kuwavutia wafanyakazi wapya kwa kiwango cha kimataifa huku ukiwafanya wafanyakazi waliopo wafurahi, washiriki na wajitolee, popote walipo.
Ajiri
Wape wanaotafuta kazi vocha za usafiri kwenda kwenye mahojiano, ukiwaonyesha kwamba wanathaminiwa na kuboresha uzoefu wao wa jumla.
Gundua hapa jinsi Shopify inavyotumia Uber for Business ili kuvutia vipaji bora.
Kuhifadhi
Haijalishi wafanyakazi wako wanafanya kazi wapi, unaweza kuwaonyesha kuwa unajali kwa kuwapa milo kupitia Uber Eats. Au toa safari za kwenda na kutoka ofisini, hafla za kazi na kadhalika.
Angalia hapa jinsi Terminus ilivyowasaidia wafanyakazi wake wakati wa COVID-19 kwa kuwapa ujira wa USD100 kila mwezi wazitumie kwenye Uber Eats.
Zawadi
Zawadi ndogo husaidia sana. Chochea uradhi wa mahali pa kazi kwa kutoa vocha za mlo kwa kazi nzuri. Au sherehekea mafanikio ya wafanyakazi ukitumia kadi za zawadi. Unaweza pia kutoa ujira wa kila mwezi kwa ajili ya milo na vitafunio.
Angalia hapa jinsi Riskalyze inavyotumia vocha za zawadi kuwatendea fadhila wateja na wafanyakazi.
Kurudi kazini
Iwe wafanyakazi wako wanarudi ofisini wakati wote au kwenye ratiba mseto, fanya mabadiliko (na safari) iwe rahisi kwa kutumia vocha za safari kwenye Uber.
Angalia hapa jinsi Eataly ilivyotumia Uber for Business kuwasaidia wafanyakazi kuhisi salama wanaposafiri kwenda kazini wakati wa janga la ugonjwa.
Hivi ndivyo inavyofanya kazi
Dashibodi ndiyo sehemu ambapo mambo yote hufanyika. Ni kituo chako cha kufikia na kufanya mipango mahususi ya usafiri, milo na kadhalika. Unaweza hata kupata ripoti za wakati halisi na habari za matumizi ya hivi karibuni.
Jiwekee vipimo
Weka vikomo vya safari na milo kulingana na siku, wakati, eneo na bajeti. Pia unaweza kuiruhusu timu yako iitoze akaunti moja ya kampuni au kadi za shirika.
Waalike wafanyakazi wanaostahiki
Wasajili wafanyakazi wako kwa kuwaalika wajiunge kwenye wasifu wa kampuni. Wanaweza kuunganisha wasifu wao binafsi wa Uber na wasifu wa kampuni wa Uber for Business kupitia barua pepe au ujumbe wa maandishi.
Anza safari
Wafanyakazi wanaweza kufurahia safari na milo kwa ajili ya usafirishaji kwa kubadilisha haraka wasifu wao wa kazini, huku ukisimamia maelezo kama vile matumizi na gharama kutoka kwenye dashibodi.
Fuatilia gharama
Sahau kuhusu kuhifadhi stakabadhi. Weka kila safari na mlo kiotomatiki kwenye mifumo ya kulipa inayoweza kukaguliwa kila wiki au kila mwezi kwa ajili ya ufuatiliaji rahisi wa bajeti.
Ongeza tija, usafiri na ustawi wa wafanyakazi wako
Chunguza nyenzo za ziada
Washukuru wafanyakazi wako popote wanapofanya kazi
Onyesha shukrani kwa timu zako ndani na nje ya ofisi kwa mawazo haya 5 ya ubunifu ya zawadi.
Fikiria upya jinsi wafanyakazi wako wanavyosafiri
Pata maelezo kuhusu jinsi mashirika yanavyoweza kugeuza jinsi timu zao zinavyosafiri kwenda kazini kwa kutumia machaguo yanayojali mazingira na yanayofaa bajeti.
Angalia jinsi kampuni moja inavyotumia Uber for Business
Pata maelezo kuhusu jinsi BetterHelp inavyotumia Uber for Business kuunda mipango ya milo ili kutoa marupurupu yenye thamani kwa wafanyakazi wa mbali kote ulimwenguni.
Simamia timu yako ukitumia Uber for Business
Hata ukichagua kuwazawadia wafanyakazi wako kwa njia gani, tunakushughulikia.
Muhtasari
Kutuhusu
Huduma
Huduma
Kulingana na matumizi
Kulingana na tasnia
Usaidizi kwa wateja
Usaidizi
Nyenzo
Pata maelezo