Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Imarisha biashara yako kwa kutoa chakula kizuri

Wape wafanyakazi na wateja milo ya kampuni. Rahisisha usafirishaji wa chakula unaoweza kufanywa kuwa mahususi kwenye biashara yako, iwe unataka kutoa milo ofisini, kwa wanaofanya kazi wakiwa mbali au kwenye mkutano wa wateja.

Milo ya kazini inafaa kwa tukio lolote

Kutoa chakula ni njia mwafaka ya kuwatuza wafanyakazi na kuwahusisha wateja.

  • Milo ofisini

    Wape wafanyakazi chakula cha mchana cha ofisini. Waruhusu wafanyakazi wachague chakula kitamu huku wakifanya matumizi kulingana na bajeti na sera.

  • Milo baada ya saa za kazi

    Wape motisha wafanyakazi wako usiku wa manane kupitia milo wanayopenda. Weka vizuizi vya muda, siku, bajeti na bidhaa kupitia mpango wa mlo au kuwapa wafanyakazi vocha.

  • Milo nyumbani

    Wape malipo wafanyakazi wanaofanya kazi wakiwa mbali au wahimize wahudhurie hafla ya mtandaoni kwa kutumia vocha za mlo. Unaweza kuweka sheria kulingana na eneo, wakati na kadhalika.

  • Milo safarini

    Iwe ni kwa ajili ya wanatimu wa mauzo wanaosafiri au wafanyakazi katika maeneo ya wateja, unaweza kuweka mipango ya milo ili uhakikishe kwamba wanakula vizuri bila kujali mahali walipo.

  • Milo kama zawadi ya mfanyakazi

    Wafahamishe wafanyakazi wako kwamba unawathamini kwa kuwatumia vocha au kadi ya zawadi ya Uber* wanayoweza kutumia kwenye programu ya Uber Eats ili wafikishiwe milo.

1/5

Huduma rahisi ya kuagiza kutoka mwanzo hadi mwisho

  • Uteuzi wa mgahawa wa kimataifa

    Chagua kutoka kwa mgao wa mji wako wa washirika 825,000 na zaidi wa wauzaji wanaopatikana ulimwenguni kote kwenye Uber Eats.

  • Machaguo mbalimbali ya milo

    Chagua kutoka kwa vyakula anuwai na mapendeleo ya lishe, ikiwemo mboga na vyakula visivyo na gluteni.

  • Vichujio rahisi vya utafutaji

    Chuja kulingana na mapishi, muda wa kusafirisha, ukadiriaji, bei na kadhalika ili upate kile unachotafuta.

1/3

Kwa nini utumie Uber for Business? Ushahidi upo kwenye tovuti

Inapatikana ulimwenguni kote

Uber for Business inapatikana katika miji 6,000 na zaidi katika nchi 32, hivyo kufanya iwe rahisi kuongeza huduma za milo kwa wafanyakazi kwenye ofisi za sasa za kimataifa au kadiri unavyokua.

Tovuti moja ya milo na safari

Simamia safari na milo ya wafanyakazi kwa urahisi kwenye tovuti moja rahisi na uepuke kushughulikia mifumo mingi ya malipo, ankara za wauzaji na kadhalika.

Kuzingatia uendelevu

Iwe ni usafirishaji wa bidhaa kwa kutumia mbinu nyingi ili kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa, kuchagua kuwekewa vyombo ili kupunguza taka za plastiki au oda za kikundi ili kuboresha ufanisi, tunafanya kazi kwa kuzingatia uendelevu.

Njia nyingi za kuokoa pesa

Weka vikomo vya matumizi kwenye mipango ya milo au vocha za ofa (unalipia tu kiasi kilichotumika). Isitoshe, agiza kulingana na ukubwa wa kundi ili uepuke maagizo mengi. Zaidi ya hayo, jisajili kwenye Uber One ili uokoe pesa zaidi.

Anza kukuza biashara yako kupitia chakula kizuri

"Kuweza kuweka kadi moja ya kampuni kulikuwa kitulizo kikubwa, si tu kwa wafanyakazi lakini pia kwa watu wanaoidhinisha gharama."

Suzanna Hodder, Meneja wa Eneo la Kazi, BetterHelp

Chunguza nyenzo zaidi

Rahisisha mlo wa wafanyakazi kwa kutumia oda za kikundi

Angalia jinsi oda za kikundi kwa kutumia Uber Eats zinavyosaidia kurudisha urafiki mezani, iwe ni ofisini au nyumbani.

Dumisha wafanyakazi bora kupitia mipango ya milo

Gundua jinsi mipango ya milo inavyoweza kusaidia kuwachangamsha wafanyakazi na kuongeza ushiriki, mlo mmoja baada ya mwingine.

Onekana kwa kutumia uanachama wa Uber One

Soma kuhusu jinsi uanachama wa Uber One huwezesha biashara yako na wafanyakazi wako kuokoa pesa na kuwapa marupurupu ya wanachama pekee.

Maswali yanayoulizwa sana

  • Machaguo ya kusafirisha chakula hadi ofisini kwako yanajumuisha kuweka oda za kikundi kwa ajili ya chakula cha mchana cha wafanyakazi au mpango wa mlo wenye vikomo vya matumizi na vizuizi vya mahali ili wafanyakazi waweze kuagiza kutoka Uber Eats wenyewe.

  • Unaweza kujiandikisha kwenye tovuti ya Uber for Business bila malipo. Shirika lako litatozwa kwa gharama zinazohusiana na kuagiza milo kwenye Uber Eats, kama kawaida.

    Unaweza kuanza leo kwa kujisajili ili ufikie dashibodi ya Uber for Business. Kujisajili kutahitaji kuthibitisha barua pepe yako ya kazini na kuweka mbinu ya malipo ili ukamilishe kusanidi akaunti (usiwe na wasiwasi, hutatozwa).

    Ikiwa biashara yako ina wafanyakazi zaidi ya 500, unaweza pia kuwasiliana na timu yetu ya mauzo ili kusaidia kukutayarisha kwa mahitaji zaidi yaliyo mahususi.

  • Mpango wa mlo unaweza kufanywa uwe mahususi ili kukidhi mahitaji ya biashara yako kwa kuweka sheria za matumizi kwa ajili ya muda, siku, vizuizi vya bidhaa, vikomo vya matumizi, eneo na kadhalika. Pata maelezo zaidi hapa.

  • Ndiyo. Mipango ya mlo kupitia dashibodi ya Uber for Business inaweza kufanywa iwe mahususi. Unaweza kuunda mipango mingi kadiri inavyohitajika ili kufanya iwe mahususi kwa ajili ya vikomo vya eneo na matumizi.

  • Biashara yenye ukubwa wowote inaweza kutumia huduma ya Uber Eats ili kusafirisha chakula katika ofisi yao.

  • Ili kuanzisha oda ya kikundi, chagua mgahawa kisha ubofye kitufe cha Oda ya Kikundi. Fanya mipangilio yako iwe mahususi, weka washiriki na uagize. Ili upate maelezo zaidi, tembelea ukurasa huu.

  • Ikiwa wewe ni mteja wa Uber for Business, wewe na wafanyakazi wako wote mnapata ufikiaji wa wahudumu wa usaidizi maalumu waliopewa ukadiriaji wa juu, wanaopatikana saa 24. Unaweza kuwasiliana na Kitengo cha Usaidizi kwa Wateja kupitia gumzo la moja kwa moja au usaidizi wa ndani ya programu. Nchini Marekani, usaidizi wa simu unapatikana kwa kupiga 800-253-9377.

  • Uber ina mipango mingi ya kuboresha vipimo vya uendelevu, ikiwemo:

    • Usafirishaji wa bidhaa kupitia mbinu nyingi: Matarishi wana chaguo la kusafirisha bidhaa kwa kutembea au kutumia baiskeli, skuta au magari yanayotumia umeme. Kupitia ushirikiano mbalimbali, Uber inafanya iwe rahisi kwa matarishi kufikia magari yanayotunza mazingira.

    • Oda za kikundi: Watumiaji wa Uber Eats wanaweza kuweka oda za kikundi pamoja na marafiki au wafanyakazi wenza ili kutumia tarishi mmoja kwenye agizo kutoka kwa mgahawa mmoja. Kuweka oda pamoja kunaboresha ufanisi na kupunguza usafiri unaorudiwa na uzalishaji wa hewa ya ukaa.

    • Kuchagua kuwekewa vyombo: Ili kupunguza taka za plastiki, watumiaji wa Uber Eats lazima waombe kuwekewa vyombo na mirija, kwa kuwa haijumuishwi tena kiotomatiki kwenye oda za milo.

    • Kuchukua oda kitongojini: Uber Eats huonyesha ramani ya kuchukua oda iliyo na migahawa mbalimbali ya kitongojini ambapo wateja wanaweza kuchagua kutembea na kuchukua oda zao ana kwa ana.

*Kadi za zawadi katika dola za Marekani hutolewa na The Bancorp Bank, N.A.

Chagua lugha ambayo unapendelea
EnglishKiswahili