Safari za kila siku kwenda kazini zimerahisishwa
Wafanyakazi wako hawapaswi kutatizika na usafiri wa kila siku. Wape safari za bila malipo kwenda kazini ili waweze kufika na kutoka ofisini kwa urahisi.
Mipango inayoweza kufanywa kuwa mahususi kwa ajili ya wafanyakazi wako
Safari ya kutoka sehemu moja hadi nyingine
Lipia gharama yote au sehemu ya safari za wafanyakazi wako ukitumia Uber. Tunakuletea hatua mpya za usalama za COVID-19 kwa ajili ya ustawi wa wafanyakazi wako.
Maili ya kwanza na ya mwisho
Wasaidie wafanyakazi wako kwenda na kutoka kwenye stesheni za magari ya umma. Walipie safari ili kuwasaidia kulipia gharama hiyo ya mwisho.
Safari za usiku wa manane
Wafikishe wafanyakazi wako nyumbani usiku kwa kulipia gharama ya safari kupitia Uber, bila kujali ni wakati gani wa usiku.
Wawezeshe wafanyakazi wako kusafiri leo
Fanya mpango wako uwe mahususi
Weka mpango wa usafiri unaowafaa wafanyakazi wako. Dhibiti kiasi cha gharama kitakacholipwa, nyakati wanazoweza kusafiri na aina ya gari wanayoweza kuomba.
Weka wafanyakazi wako
Waalike wafanyakazi wako wajiunge kwenye akaunti ya kampuni yako. Unaweza kuwaalika mmoja mmoja, kupakia faili la CSV au kuoanisha na mfumo wako wa usimamizi wa wafanyakazi.
Wawezeshe wafanyakazi kuomba safari
Wakati wowote wafanyakazi wako wanapohitaji kusafiri, wanaweza tu kubadilisha wasifu wao wa kazini na kuomba safari kwenye programu ya Uber.
Jinsi mpango wa safari unavyoweza kusaidia biashara yako
Safari zisizofadhaisha na za kuaminika
Kuanzia orodha kaguzi za usalama za COVID-19 hadi uchunguzi wa lazima wa rekodi ya uhalifu ya dereva, tumechukua hatua ili kuhakikisha kwamba tumeupa usalama kipaumbele.
Marupurupu yanayokutofautisha na watu wengine
Wavutie na udumishe wafanyakazi wenye tija kwa kuwapa safari kwa kutumia Uber kama sehemu ya faida zako za msafiri.
Nyenzo za kukusaidia kudhibiti gharama
Okoa pesa kwa maegesho na gharama za kila mwaka za usafiri. Ni rahisi kuweka vikomo vya mahali na wakati wa siku.
"Wakati ambapo machaguo ya usafiri wa kawaida hayakupatikana, Uber for Business ilitoa njia bora kwa wafanyakazi wanaotoa huduma muhimu kusafiri kwenda maeneo ya biashara ya Manhattan kila siku."
Stacey Cunningham, Rais, NYSE
Biashara yako inazidi kuimarika. Tuko hapa ili kukusaidia.
- Je, biashara inawezaje kuwapa wafanyakazi wake safari za bila malipo kwenda kazini?
Uber inaruhusu kampuni kufungua akaunti ya kampuni, kuunda mpango wa safari, kusimamia gharama za usafiri kwa ajili ya wafanyakazi wao. Kupitia mpango huu, biashara zinaweza kuwapa wafanyakazi wao safari za bila malipo kwenda kazini, mikutano au shughuli nyingine zinazohusiana na biashara.
- Je, Uber inapatikana usiku kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika zamu ya usiku?
Down Small Wafanyakazi wanaweza kuomba safari wakati wowote wa siku. Wasimamizi wanaweza kuanzisha mipango ya safari ndani ya dashibodi ya Uber for Business ili kufidia safari za usiku wa manane kwa wafanyakazi kwa kuweka muda, eneo na vizuizi vya matumizi.
- Je, inawezekana kuunganisha chaguo la safari katika mpango wetu wa faida za wafanyakazi na kuwapa wafanyakazi wanaostahiki safari za bila malipo?
Down Small Wasimamizi wanaweza kuanzisha mpango wa safari ndani ya dashibodi ya Uber for Business ili kutoa faida za sehemu ya safari au safari kamili. Msimamizi anaweza kuufanya mpango uwe mahususi kwa wafanyakazi fulani, nyakati za siku, kiasi cha matumizi na maeneo ili kuhakikisha kwamba faida inatumiwa kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
- Tunawezaje kuhakikisha kwamba wafanyakazi wetu wanatumia Uber kwa kuwajibika?
Down Small Njia mbili ambazo wasimamizi wanaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa ulaghai ni kwa kuweka vizuizi na kuangalia shughuli za wafanyakazi kwenye dashibodi ya Uber for Business.
- Tunaweza kufuatilia vipi safari za Uber ambazo wafanyakazi wetu huenda ili kusaidia kuhakikisha kwamba wanafika nyumbani salama?
Down Small Wasafiri wanaweza kupata taarifa muhimu ya usalama kwa urahisi, kupata usaidizi wa dharura na kuonyesha mahali walipo, hayo yote kutoka kwenye programu ya Uber. Wasimamizi pia wanaweza kuona safari za wafanyakazi kutoka kwenye dashibodi ya msimamizi. Isitoshe, Uber for Business imeunganishwa kwenye International SOS ili kuboresha mwonekano wa kampuni.
Gundua mengi zaidi kuhusu Uber for Business
Muhtasari
Kutuhusu
Huduma
Huduma
Kulingana na matumizi
Kulingana na tasnia
Usaidizi kwa wateja
Usaidizi
Nyenzo
Pata maelezo