Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kutumia vocha kwenye Uber

Una bahati ikiwa umepokea vocha ya kutumia kulipia safari au chakula!

Utahitaji kufuata hatua chache rahisi ili kuhakikisha unapokea huduma bila matatizo.

Ungependa kutumia vocha katika biashara yako?

Hatua nne za kutumia vocha kulipia safari

Hatua za kufuata wakati uko tayari kusafiri

Ungependa kutumia vocha kulipia Uber Eats?

Vidokezo na mbinu za kutumia vocha kulipia safari

Nitatumia vocha yangu vipi?

Unaweza tu kutumia vocha katika kipindi na eneo mahususi, kulingana na aliyeitoa. Unaweza kuona maelezo haya baada ya kutumia vocha.

Vocha yangu iko wapi?

Vocha itaonekana kiotomatiki kwenye skrini ya ombi la usafiri katika sehemu ya chaguo za malipo. Utaweza pia kuona vocha yako kwa kubofya kwenye Mipangilio, Wallet na kusogeza chini kwenye sehemu ya Vocha.

Siko tayari kutumia vocha yangu.

Vocha yako itasalia kwenye akaunti yako hadi muda wake utakapoisha, lakini unaweza kuchagua unapotaka kuitumia kwa kuwasha na kuzima swichi yake. Baada ya kuweka maelezo ya mahali unakoenda, bonyeza tu vocha kwenye njia ya malipo ili uchague njia nyingine za malipo.

Je, vocha zitatumika katika wasifu wangu wa kazini?

Hapana. Kwa sasa, vocha hazitumiki kwenye wasifu wako wa kazini. Hakikisha unatumia wasifu mwingine wowote kando na huo ili uweza kutumia vocha.

Nina matatizo mengine.

Ikiwa una matatizo ya kudai vocha, tafadhali wasiliana na mtoa huduma ili uthibitishe kuwa vocha iko tayari kutumika. Kwa maswali mengine, tembelea sehemu ya usaidizi kwenye menyu ya App yako ya Uber.

Unatafuta vocha yako?

Ikiwa umeweka mahali unakoenda na bado huoni vocha yako, bonyeza kwenye njia ya malipo kisha usogeze chini ili uweke swichi ya vocha yako iwe “imewashwa”.

Ikiwa una Wasifu mbalimbali wa Safari, itabidi ubonyeze “badilisha” chini ya wasifu wako wa kibinafsi ili uone aina za malipo.

Chagua lugha ambayo unapendelea

Kiingereza, EnglishKiswahili, Kiswahili

Chagua lugha ambayo unapendelea

Kiingereza, EnglishKiswahili, Kiswahili