Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tokyo Haneda (HND)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Haneda kwenda Tokyo Station au kutoka Shinjuku kurudi Hanenda.

4-3 Haneda-Kuko, 2-Chome, Ota-Ku, Tokyo 144, Japan
+81 3-5757-8111

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • Taxi

  1-4

  Get matched with a taxi nearby

 • Black

  1-4

  Premium rides for groups of up to 4

 • Black Van

  1-5

  Premium rides for groups of up to 5

1/3

Kupata usafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Haneda

Itisha gari ukiwa tayari kutoka nje.

Chagua aina ya gari linalofaa ukubwa wa kikundi chako na mizigo mnayohitaji kubebewa. Kisha, chagua eneo ambapo ungependa kuchukuliwa.

Ondoka kupitia ghorofa ya wanaowasili

Elekea katika eneo la kuchukuliwa ulilochagua kwenye programu.

Mtafute dereva wako

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Haneda

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Haneda na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Haneda

Ada

Ada ya kiwango cha juu cha ¥2,100 kila siku
Hazizidi ¥700 kila siku
Ada isiyopita ¥4,200 kila siku
Ada ya juu zaidi ya ¥1,050 kila siku; unapaswa kuonesha stakabadhi ya ulemavu
Ada haizidi ¥2,100 kila siku pamoja na ¥1,400 ya kuwekewa nafasi
Ada ya juu zaidi ya ¥4,200 kila siku pamoja na ¥2,800 ya kuweka nafasi
Ada hazipiti ¥1,050 kwa siku, pamoja na ada ya ¥700 ya kuweka nafasi; unatakiwa kuonesha cheti che walio na ulemavu
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 17 Desemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Haneda

Uwanja wa Ndege wa Haneda umegawanywa mara 3: Kituo cha Kimataifa na Vituo vya Nchini vya 1 na 2.

Usipitwe na lolote

Jinsi ya kuunganisha kwenye wifi ukiwa HND

Unaweza kuunganisha kwenye wifi bila malipo katika Uwanja wa Ndege wa Haneda. Chagua tu HANEDA-FREE-WIFIkwenye mitandao ya Wi-Fi, kisha ufungue kivinjari chako na ufuate maagizo yaliyopo.

Jipatie kadi ya SIM ya mahali ulipo

Unaweza kununua kadi ya SIM ya kulipia mapema kwenye sehemu ya wanaowasili katika Ghorofa ya 2 ya Kituo cha Wasafiri wa Kimataifa.

Kadi za SIM za Kulipia Mapema haziuzwi katika Vituo vya 1 na 2 vya Wasafiri wa Nchini.

Kadi za SIM za Kulipia Mapema zinazopatikana nchini Japani za wasio wenyeji wa Japani hutumika kwa mawasiliano ya data tu. Katika Sheria ya Japani, wasio wenyeji wa Japani hawawezi kununua kadi za SIM zinazoruhusu simu za sauti.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Haneda

Uwanja wa Ndege wa Haneda ndio wenye shughuli nyingi zaidi nchini Japani, huku ukihudumia eneo zima la Tokyo, ni moja kati ya viwanja 2 vya ndege muhimu sana jijini Tokyo. Haneda unaweza kufikika kwa urahisi zaidi ukilinganishwa na uwanja mwenza wa Narita, na uko umbali wa dakika 25 kwa gari kutoka katikati mwa Tokyo.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Haneda

Uwanja huu umegawanywa kati ya vituo vya kimataifa na vya nchini. Safari zote za kimataifa zipo katika Kituo cha Abiria cha Kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Haneda, huku safari za ndani ya nchi zikiwa katika Kituo cha 1 na Kituo cha 2.

Kituo cha 1 katika Uwanja wa Ndege wa Haneda

 • JAL
 • Japan Transocean Air
 • Skymark
 • Star Flyer (safari za kwenda viwanja vya ndege vya Kitakyushu na Fukuoka)

Kituo cha 2 katika Uwanja wa Ndege wa Haneda

 • AIRDO
 • ANA
 • Solaseed
 • Star Flyer (safari za kwenda viwanja vya ndege vya Yamaguchi-Ube na Kansai)

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Haneda

Uwanja wa ndege una mabasi yanayofanya kazi kati ya vituo vya safari za ndani ya nchi na Kituo kidogo cha Wasafiri wa Kimataifa kila baada ya dakika 4.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Haneda

Katika ukumbi wa Kituo cha Wasafiri wa Kimataifa, kuna huduma za kubadilisha fedha kwa saa 24 katika ghorofa za 2 na 3. Ofisi nyingine 2 zipo katika sehemu ya kuondoka kwa safari za kimataifa.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Haneda

Iwe unahitaji hoteli kwa sababu unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, unaweza kwenda kwenye hoteli ya uwanja wa ndege na kuna zaidi ya hoteli 30 na maeneo ya kulala karibu.

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Haneda (HND) hapa.

Facebook

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.