Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Vocha: badilisha upendavyo, tuma, eneza furaha

Vocha huwa na manufaa makubwa, popote unapofanya kazi

Ibadilishe upendavyo ili ikufae

Chagua iwapo ungependa vocha zinazoweza kutumiwa unaposafiri ukitumia Uber, vyakula ukitumia Uber Eats au zote mbili. Weka vizuizi kama vile eneo na muda wa matumizi kisha ubadilishe vocha zako upendavyo kwa kuweka nembo na ujumbe wa kampuni yako.

Boresha gharama zako

Toa vocha ya kiasi chochote utakachochagua na utalipia tu kile kitumiwacho na wapokeaji. Hali hii husaidia kukupa ufuatiliaji bora na usimamizi wa gharama.

Wasambazie watu binafsi au vikundi kwa urahisi

Imetumwa moja kwa moja kutoka kwenye dashibodi yako, ni bora zaidi vocha zikitumwa kwa watu binafsi au kwa wingi kwenye vikundi. Wapokeaji hupokea kiungo cha kipekee au msimbo wa QR uliorahisi kutumia ili wapate vocha kwenye wasifu wao binafsi wa Uber.

Uangalizi wa kipengele

Ongeza picha kwenye vocha

Badilisha vocha ikufae kwa ajili ya matukio. Chagua kwenye uteuzi wa picha na video ili kuipa vocha yako mwonekano maalum na uweke sauti ya tukio lako.

Ongeza idadi ya wanaohudhuria matukio

Saidia kuboresha ushiriki kwa kutoa vocha za usafiri kwa sherehe za likizo, warsha au shughuli za kuimarisha ushirikiano wa wafanyakazi. Je, ungependa kutoa chakula cha mchana wakati wa matukio ya mtandaoni? Vocha zitakusaidia.

Watie wafanyikazi motisha

Watuze wafanyikazi bora kwa kufanya kazi nzuri au uipe timu nzima vocha ya kila mwezi ya safari na chakula. Iwapo ungependa kuajiri wafanyakazi wapya, kuwa bora zaidi kwa kugharamia safari za wanaotafuta kazi hadi kwenye kituo cha mahojiano. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Shopify hutumia vocha kuajiri.

Wavutie wateja

Toa vocha za usafiri usiolipishwa kwa wateja wenye magari katika duka lako, wasaidie wanaosafiri kwa njia ya ndege kufika wanakoenda wakati safari ya ndege imechelewa au uwape wageni katika hoteli safari za VIP, katika ziara yao mjini. Pata maelezo kuhusu JetBlue na westdrift huwafurahisha wateja wao na vocha.

Gundua mawazo zaidi kuhusu jinsi ya kuwashukuru wateja hapa.

Dhibiti yote kwenye dashibodi

  • Kuza ukitumia violezo

    Violezo hukuwezesha kubuni, kutuma na kutuma tena vocha zenye thamani na vizuizi sawa. Unaweza hata kufunga mipangilio ya violezo ili maelezo ya mpokeaji pekee yaweze kubadilishwa. Pata maelezo zaidi

  • Endelea kudhibiti mipangilio

    Weka vizuizi vyako mwenyewe kama vile pesa kwenye vocha; aina za vocha za thamani, asilimia ya ofa na mipangilio ya eneo, muda wa matumizi na mwisho wa matumizi.

  • Wekea vocha zako mapendeleo

    Weka nembo ya shirika lako na ujumbe maalum ili uwafurahishe wapokeaji.

  • Tuma kwa wingi

    Furahisha timu nzima au orodha nzima ya wateja wako kwa hatua chache tu. Unaweza hata kuratibu vocha zitumwe tarehe maalum.

  • Shiriki ukitumia misimbo ya QR

    Rahisisha jinsi unavyosambaza vocha kwa kutayarisha msimbo maalum wa QR unaoweza kuchanganuliwa na wapokeaji ili wautumie.

  • Fuatilia matumizi ya vocha

    Endelea kufuatilia kampeni yako ya vocha kwa kufuatilia hali ya utumiaji kwa kila mpokeaji kwenye Dashibodi ya Uber for Business.

1/6
1/3
1/2

Ni rahisi kuanza

Hatua ya 1: Fungua akaunti

Ingia au ufungue akaunti ya Uber ukitumia barua pepe yako ya kazini kisha ufuate maagizo ili ujisajili kwenye shirika lako katika Uber for Business. Thibitisha anwani ya barua pepe yako ya kazini utakapoombwa.

Hatua ya 2: Weka mbinu yako ya malipo

Chagua Mpango wa vocha, kisha uweke mipangilio ya mbinu ungependa kutumia kwenye malipo. Usijali, hutatozwa hadi wapokeaji watakapotumia vocha zao.

Hatua ya 3: Chagua vigezo

Tayarisha vocha na ubadilishe mipangilio kama vile thamani na maeneo yanayotimiza masharti, tarehe na saa upendevyo. Pata maelezo zaidi kuhusu vizuizi.

Hatua ya 4: Sambaza vocha

Tuma vocha ukitumia barua pepe, ujumbe, upakiaji wa CSV au URL au moja kwa moja katika programu ya Uber—yote kutoka kwenye dashibodi yako.

Hatua ya 5: Tumia

Vocha huwekwa kwenye wasifu binafsi wa Uber kisha hutumika kiotomatiki wakati wa kulipia safari zinazotimiza masharti au oda za Uber Eats. Pata maelezo zaidi

"Kazi yetu na Uber for Business inaonyesha lengo letu la kuongeza thamani zaidi kwa uzoefu wa wateja. Tunayo furaha kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma rahisi ya sehemu moja hadi nyingine.”

Andres Barry, Rais, JetBlue Travel Products

Weka mipango yako ya vocha kwa kutotoza ada ya kujisajili

Utatozwa tu wapokeaji wako watakapotumia vocha katika safari yao kwenye oda ya Uber au Uber Eats.

Sheria na masharti ya Uber yatatumika na yatatolewa baada ya usambazaji au kudai vocha.

Chagua lugha ambayo unapendelea

EnglishKiswahili

Chagua lugha ambayo unapendelea

EnglishKiswahili