Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Utaratibu wa nyongeza ya nauli

Pata maelezo kuhusu jinsi huduma ya ongezeko la nauli inavyosaidia kukutanisha wasafiri na madereva kwa haraka ili wafike wanakoenda.

Utaratibu wake

Idadi ya wasafiri huongezeka

Kuna nyakati ambapo watu wengi huitisha usafiri zaidi na kufanya magari yakose kutosha wasafiri wote. Kwa mfano, hali mbaya ya hewa, nyakati za shughuli nyingi na matukio mahususi, huenda yakasababisha watu wengi zaidi kuitisha usafiri wa Uber kwa wakati mmoja.

Nauli huongezeka

Katika hali ambapo kuna wasafiri wengi, nauli huenda zikaongezeka ili kuwasaidia wanaotaka kusafiri wapate gari. Mfumo huu unaitwa nyongeza ya nauli na unasaidia App ya Uber kuwa chaguo la kuaminika.

Wasafiri hulipa nauli ya juu au kusubiri hadi ipungue

Wakati wowote ada zinapoongezwa kwa sababu ya kuongezeka kwa nauli, App ya Uber huwafahamisha wasafiri. Baadhi ya wasafiri wataamua kulipa nauli hiyo ilhali wengine wataamua kusubiri kwa dakika kadhaa wakitarajia nauli ipungue.

Ni utaratibu gani unaotumika kukadiria ongezeko la nauli?

Nauli zinapoongezeka, kizidishaji cha viwango vya kawaida, kiasi cha ziada cha nyongeza, au nauli ya mapema ikiwa ni pamoja na kiasi cha nyongeza itaonekana kwenye kadi yako ya ofa. Hii itabadilika kutegemea jiji lako. Asilimia ya ada ya huduma ya Uber haibadiliki nauli inapoongezeka.

Kwa sababu tunabadilisha ada kulingana na idadi ya wasafiri moja kwa moja, nyongeza ya nauli inaweza kubadilika haraka. Nyongeza ya nauli pia ni mahususi katika maeneo tofauti mjini, kwa hivyo huenda nauli ikaongezeka katika baadhi ya maeneo na kukosa kuongezeka kwingine.

Jinsi ya kutambua nyongeza ya nauli katika App

Ikiwa nyongeza ya nauli inatumika katika mji wako idadi ya wasafiri inapoongezeka katika eneo mahususi, rangi katika eneo hilo itabadilika. Maeneo yenye rangi kwenye ramani huwa na rangi mbalimbali kuanzia chungwa hafifu hadi nyekundu iliyokolea. Maeneo yenye rangi ya chungwa hafifu huwakilisha fursa ndogondogo za mapato kutokana na nyongeza ya nauli, ilhali maeneo yenye rangi nyekundu huwakilisha kubwa zaidi.

Tunapojitahidi kuboresha soko, tunaweza kujaribu utendaji na bei kwa njia ambazo hazijaelezewa kwenye tovuti hii.