Mambo ya msingi
Mchakato wa kuwa dereva wa Uber nchini Tanzania
Uber ni njia ya kisasa ya kujiajiri na kupata pesa. Watu wengi wana sifa za kuwa madereva wa Uber. Hii hapa ni taarifa unayotakiwa kujua iwapo ungependa kuwa dereva wa Uber jijini Dar es Salaam.
Anza kazi
1. Jiandikishe mtandaoni
Tayari una anwani ya barua pepe na simu ya smartphone? Vizuri, sasa tupatie maelezo machache kuhusu wasifu wako na tutakusaidia katika mchakao wa kujiandikisha.
2. Pakia nyaraka zako
Muda wa kuhakiki nyaraka zako. Nyaraka tunazotaka uweke ni zifuatazo:
- Kadi ya gari ambayo muda wake haujaisha (La angalau abiria 5)
- Bima ya gari
- Kadi ya Usajili wa Gari kwa ajili ya Shughuli za Biashara
- Leseni ya dereva Class C, C1, C2, or C3
- Leseni ya Teksi au Magari a Watalii
- Picha ya dereva
- Lazima iwe ni picha ya mbele, iwe katikakati na ionyeshe uso wote wa dereva na mabega, na asivae miwani ya jua
- Sharti iwe ni picha ya dereva tu na kusiwe na chombo kingine kwenye ndani ya fremu ya picha, mwangaza wa kutosha, na ionekane vizuri. Huwezi kutumia picha ya leseni ya dereva au picha nyingine za albamu
3. Tafuta gari
Ni gari gani linanifaa zaidi? Hakikisha linatimiza masharti yetu tuliyoweka nchini Tanzania, na ukumbuke kwamba utapata pesa nyingi zaidi ikiwa ulaji wake wa mafuta ni mdogo.
4. Kutumia akaunti yako
Ikiwa umekamilisha utaratibu ulioorodheshwa hapo juu, hongera! Sasa kila kitu shwari na unaweza kutumia akaunti yako kupata pesa.
Pata maelezo zaidi kutoka Uber
Anza kutengeneza pesa kwa kuendesha gari ukitumia Uber ukiwa Tanzania
Taarifa inayopatikana kwenye ukurasa huu wa tovuti ni kwa madhumuni ya kutoa taarifa pekee na huenda isitumike katika nchi, eneo au miji ulipo. Inaweza kubadilika na huenda tukaibadilisha bila kukuarifu.
Kuhusu