Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi
Msaada na Taarifa kuhusu Virusi vya Korona (COVID-19)

The health and safety of the Uber community is always our priority. We are actively monitoring the coronavirus (COVID‑19) situation and are taking steps to help keep those that rely on our platform safe. Click here for more information.

X small

Tunakuletea Uber Pro

Uber Pro ni mpango mpya wa zawadi ambao unawatambua madereva bora, kukuwezesha kufikia malengo yako, iwe unaendesha au huendeshi gari.

Utaratibu wake

Pata pointi

Endesha gari ukitumia Uber ili upate pointi. Safari nyingine zinaweza zikakupa pointi zaidi. Angalia maelezo zaidi kwenye App ya Dereva.

Wape wasafiri huduma bora zaidi

Zaidi ya kupata pointi, ni sharti udumishe tathmini fulani ili upate zawadi za viwango vya Gold, Platinum na Diamond. Masharti hutofautiana kulingana na eneo. Tafadhali angalia App ya Dereva upate maelezo zaidi.

Pata zawadi

Kadri hadhi yako inapoimarika, ndivyo unavyopata zawadi zaidi. Hadhi yako huhesabiwa kulingana na pointi na ubora wa tathmini katika kipindi maalum cha miezi 3.

Pata zawadi haraka zaidi

Safari unazokamilisha katika saa mahususi kila siku hukupa pointi zaidi. Angalia App ya Dereva uone saa unazoweza kupata pointi haraka zaidi.

Huduma bora zaidi kwa wasafiri hukupa zawadi zaidi

Unapokea zawadi kulingana na jinsi unavyotumia App ya Uber. Ili ufikie hadhi ya Gold, Platinum na Diamond na uendelee kupokea zawadi, sharti upate pointi na udumishe tathmini fulani. Ili upate maelezo zaidi, bonyeza aikoni ya menyu katika App ya Dereva, kisha ubofye Uber Pro na kishale cha kulia karibu na sehemu ya juu ya skrini.

Pata pointi na ufurahie zawadi katiki vipindi maalum vya miezi 3

Utajipatia pointi katika vipindi maalum vya miezi 3. Pointi huwekwa upya baada ya kila kipindi.

Ukijipatia pointi za kutosha kufikia kiwango kinachofuata cha zawadi, utaanza kupokea zawadi mpya papo hapo. Ongeza kiwango cha tathmini zako na upunguze kiwango cha kughairi safari ili uweze kuendelea kufurahia zawadi hadi mwisho wa kipindi kijacho cha miezi 3.

Angalia vigezo na masharti.

Ili kukusaidia ushiriki katika mpango wa Uber Pro, Uber itachakata data fulani ya kibinafsi, kama inavyoelezwa kwa kina hapo juu, ili kuhesabu kiwango cha hadhi yako. Ukichagua kuruhusu zawadi unayopewa na washirika wengine, Uber itawatumia jina na maelezo ya anwani yako ili kuboresha mchakato wa usajili na kuthibitisha kiwango cha hadhi yako. Mshirika mwingine anaweza kukusanya data zaidi wakati wa usajili na kukujulisha baadaye.

Mshirika mwingine anayetoa zawadi atakuwa mdhibiti wa data yako ya binafsi anayopokea kutoka kwa Uber kwa niaba yako na inayokusanywa ili kukupa zawadi. Tunakuhimiza usome sera ya faragha. Uber itakuwa kampuni inayodhibiti data ya kibinafsi inayochakata ili kuhesabu kiwango cha hadhi yako na kukutumia taarifa kuhusu hadhi na zawadi. Ili uweze kupata maelezo zaidi kuhusu haki zako za faragha, tafadhali tembelea ukurasa huu wa tovuti ulio na maelezo zaidi na usome Sera yetu ya Faragha. Unaweza kujiondoa kwenye mpango huu. Unaweza kupata maelezo kamili kuhusu jinsi ya kufanya hivyo katika Vigezo na Masharti ya Uber Pro..