Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kutayarisha gari lako

Kabla ya kuanza safari yako ya kwanza, haya ni baadhi ya mambo ambayo madereva wanapendekeza. Katika baadhi ya miji, hatua hizi zinahitajika kwa mujibu wa sheria.

Kujitayarisha kwa safari yako ya kwanza

Madereva wengi waliopata tathmini za juu zaidi wanasema kwamba hutayarisha zana hizi kwenye gari lao kabla ya kuendesha. Sheria na vikwazo vya eneo vinaweza kuzingatiwa.

1. Kipachiko cha simu cha kusogeza bila kugusa.

2. Kipokea sauti cha Bluetooth cha kupokea simu (inaporuhusiwa na sheria).

3. Chaja ya simu ili betri yako isiwahi kuishiwa na nishati unapoendesha gari.

4. Nembo ya Uber (pia inaitwa kibandiko au vazi la biashara), inahitajika katika baadhi ya miji.

Viinua mgongo

Tuliwaomba madereva vidokezo zaidi kuhusu kujitayarisha kuendesha gari.

Kudumisha usafi

Madereva wengi walisema gari safi ni muhimu kwa ajili ya kupata tathmini nzuri na pongezi.

Kuwa na mpango wa muziki

Madereva waliopewa tathmini za juu wametuambia wanazingatia aina na kiwango cha sauti cha muziki (iwe ni waliochagua au wa kituo cha redio) kinachoweza kufurahisha na kisiwasumbue wasafiri. Wasipokuwa na uhakika, huwauliza wasafiri ikiwa wana kituo wanachokipenda au kama wangependa kucheza muziki kupitia simu yao wenyewe.

Maswali yanayoulizwa sana

  • Je, unanuia kuendesha gari ukitumia programu ya Uber lakini bado hujajisajili? Anza kwa kupakua programu ya Dereva wa Uberkwenye Google Play au App Store (tafuta Dereva wa Uber). Kisha njoo hapa ufungue akaunti.

  • Miji mingi inafanya ukaguzi kabla ya kuendesha gari ukitumia Uber. Vigezo vya ukaguzi vinatofautiana kulingana na eneo lako. Ikiwa ungependa kujua mapema mahitaji ya mji wako, wasiliana na Uber Greenlight Hub iliyo karibu nawe kwa maelezo.

Taarifa inayopatikana kwenye ukurasa huu wa tovuti ni kwa madhumuni ya kutoa taarifa pekee na huenda isitumike katika nchi, eneo au miji ulipo. Inaweza kubadilika na huenda tukaibadilisha bila kukuarifu.