Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Tunakuletea programu mpya ya madereva, rafiki yako barabarani

Programu mpya ya Madereva itakusaidia kutengeneza hela zaidi kwa kukupa habari za papo hapo. Programu hii ni rahisi kutumia na utendakazi wake ni thabiti zaidi. Itakusaidia katika kila hatua —kama mshirika wa kweli.

Tazama Video

Tumeshirikiana na wewe kuiunda ili ikufae zaidi

Tumeshirikiana na madereva na washirika wanaosafirisha mizigo kote ulimwenguni katika kuunda programu mpya inayokusaidia kupiga hatua mbele. Ijaribu sasa.

Kwa madereva

Pata arifa kuhusu mahali pa kuendesha gari wakati kuna wasafiri wengi

Gusa sehemu zenye fursa kwenye ramani yako ili upate safari nyingi zaidi karibu nawe, kisha uulize programu ikuelekeze huko.

Kwa madereva na washirika wanaosafirisha mizigo

Fahamu hatua inayofuata

Upau wa hali kwenye sehemu ya chini ya skrini ya ramani utakujulisha ukiwa katika eneo lenye wasafiri wengi. Hivyo, unaweza kufanya uamuzi mwema kuhusu iwapo utapumzika au utaendelea kuendesha gari.

Kwa madereva na washirika wanaosafirisha mizigo

Fuatilia mapato yako kwa urahisi

Fuatilia kwa urahisi hatua unazopiga ili kutimiza malengo yako ya mapato ya kila siku na kila wiki. Unaweza pia kufikia muhtasari wa mapato yako kwa kugusa tu.

Jinsi ya kufuatilia mapato yako: gusa aikoni ya nauli kwenye skrini yako ya ramani, kisha utelezeshe kidole kulia na kushoto ili ukague mapato yako.

Kwa madereva na washirika wanaosafirisha mizigo

Panga siku yako kwa urahisi

Angalia mabadiliko ya saa kwa saa, weka mapendeleo na uangalie ofa—yote katika programu moja.

Jinsi ya kupata Zana ya Kupanga Safari: Gusa aikoni ya kishale kwenye kona ya chini ya kushoto ya skrini ya ramani. Kwa washirika wanaosafirisha mizigo, tutawaletea kipengele hiki hivi karibuni.

Kwa madereva na washirika wanaosafirisha mizigo

Unaweza ukategemea programu hii hata ukiwa nje ya mtandao

Je, muunganisho wa intaneti umekatika? Bado unaweza kuanzisha na kumaliza safari bila wasiwasi.

Kwa madereva na washirika wanaosafirisha mizigo

Usipitwe na lolote

Pata habari zote kwa kutumiwa ujumbe, iwe ni matukio yajayo, fursa za kujichumia hela au maelezo kuhusu akaunti yako na vipengele vipya.

Jinsi ya kupata Arifa: kila unapopokea ujumbe mpya, baji itaonekana kwenye picha yako katika kona ya kulia ya skrini ya ramani. Iguse ili usome ujumbe.

Kwa madereva na washirika wanaosafirisha mizigo

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia programu

Iwe ni safari yako ya kwanza au ya 100, sasa una nyenzo iliyojaa vidokezo na video zenye maelezo muhimu.

Jinsi ya kupata Maelezo ya Msingi kuhusu Programu ya Madereva: gusa picha kwenye kona ya kulia ya skrini ya ramani. Kisha juu ya ‘Akaunti’, gusa ‘Usaidizi’.

Utaratibu wa kutumia Uber

Kuingia mtandaoni

Uber inapatikana wakati wowote. Kwa hivyo, ukiwa tayari kuendesha gari au kusafirisha mizigo wakati wowote, fungua programu halafu uguse NENDA.

Kukubali maombi ya kusafirisha abiria na mizigo

Ukiwa mtandaoni, utaanza kupokea maombi ya usafiri katika eneo lako moja kwa moja. Simu yako italia. Telezesha kidole ili ukubali.

Maelekezo ya hatua kwa hatua

Programu hii hurahisisha hatua za kumpata mteja na kumfikisha anakoenda. Kwa hivyo, kazi yako itakuwa kumakinika barabarani tu.

Mapato ya kila safari

Angalia pesa ulizopata baada ya kila safari na ufuatilie hatua unazopiga ili utimize malengo ya mapato ya kila siku na kila wiki. Tutatuma mapato moja kwa moja kwenye akaunti yako ya benki kila wiki.

Mfumo wa kutathmini

Mfumo wa Uber unaowawezesha wahusika wote kutathminiana husaidia kudumisha huduma salama na inayoridhisha. Wasafiri, madereva na wateja wengine wataulizwa watoe maoni kuhusu kila safari.

App ya madereva

Anza kuendesha gari ukitumia mfumo wa Uber