Ongeza manufaa ya wafanyakazi wako ukitumia Uber One
Uanachama wa Uber One huboresha mpango wako wa manufaa ya mfanyakazi na biashara yako. Timu yako itafurahia marupurupu ya kipekee kwa usafiri wa biashara, milo, usafirishaji bidhaa na mengine mengi.
Kinachowafaa wafanyakazi wako
Kutoka kwenye ada zilizoondolewa za usafirishaji bidhaa hadi huduma inayolipishwa, ipe timu yako marupurupu ya tabaka la biashara ambayo ianaweza kupata tu kwa Uber One.
Ada ya Kusafirisha Bidhaa isiyo na Kikomo ya $0
Pata Ada ya Usafirishaji Bidhaa ya $0 kwa oda zinazotimiza masharti za vyakula, mboga mboga na pombe.* Tafuta aikoni ya Uber One kwenye programu.
Furahia punguzo la 5%
Pokea punguzo la asilimia 5 kwenye safari, usafirishaji bidhaa na oda za kuchukua zinazostahiki kwenye programu za Uber na Uber Eats.*
Huduma ya kipaumbele
Pata madereva waliokadiriwa juu zaidi kwa safari na Uber One Promise kwenye usafirishaji bidhaa—$5 kwa Uber Cash ikiwa makadirio yetu ya Kuwasili Hivi Karibuni si sahihi.*
Marupurupu ya kipekee
Furahia usaidizi wa wanachama wanaolipiwa, ofa na punguzo maalum, na huduma za kipekee zinazopatikana kwa wanachama wa Uber One pekee.
Boresha kwa urahisi Uber One kulingana na biashara yako
Hatua ya 1: Mpangilio wa kampuni
Shirikiana na timu yetu ya wataalamu kubinafsisha programu ya Uber One kwa ajili ya kampuni yako. Kisha wasimamizi wataweka dashibodi yao ili kuwezesha mialiko ya wafanyakazi kuwa ya kiotomatiki na kudhibiti programu kuanzia leo na kuendelea.
Hatua ya 2: Usajili wa wafanyakazi
Kila mfanyakazi atapokea mwaliko wa barua pepe wa kujiunga na programu. Ili kukubali, wafanyakazi watafuata kiungo kilicho kwenye barua pepe ili kupakua au kuingia katika programu yao ya Uber au Uber Eats kwenye simu au wavuti.
Hatua ya 3: Tayari. Chonjo. Nenda!
Baada ya kukubaliwa, wafanyakazi wataweza kufikia manufaa ya Uber One kwenye milo, safari zinazostahiki na zaidiyanayowekwa kwenye oda za biashara na za binafsi.
Kinachofaa biashara yako
Toa marupurupu ya wafanyakazi yenye ushindani
Tambulika kwa urahisi kwa waombaji kazi kwa kutoa marupurupu ya kulipia ambayo wafanyakazi wako watapenda, kwenye jukwaa linalofahamika.
Ongeza ushiriki wa wafanyakazi
Pata zaidi ya manufaa ya kimsingi kwa nyongeza zinazostahili kujivunia ambazo zitazifanya timu zako kuwa na furaha, ari na tija.
Toa manufaa rahisi kwa timu mseto
Toa marupurupu yanayofaa ya mbali, ana kwa ana na mseto ambayo yanayolingana na mahitaji yako katika mazingira ya kazi yanayobadilika kila wakati.
Chunguza nyenzo zaidi
Je, ungependa kuanzisha mipango ya usafiri na chakula kwa wafanyakazi wako? Fuata mwongozo wa hatua kwa hatua kuhusu jinsi ya kujisajili ili uendelee.
Angalia jinsi biashara kubwa na ndogo zinavyotumia mfumo wetu wa kimataifa kwa usimamizi wa safari za kampuni, vyakula na usafirishaji wa nchini.
Gundua jinsi kuwapatia wafanyakazi, wateja na watu wengine vyakula kunavyoweza kukusaidia na kuboresha mambo.
Maswali yaulizwayo mara kwa mara
- Wafanyakazi hukomboaje uanachama wao wa Uber One?
Mfanyakazi yeyote aliyeongezwa kwenye mpango atapokea barua pepe ili kudai uanachama wake wa Uber One. Mara tu mfanyakazi anapofungua akaunti ya Uber, anaweza kukomboa na kutumia uanachama wake kwenye wavuti au simu ya mkononi kupitia programu ya Uber au Uber Eats.
- Je, manufaa ya Uber One yanapatikana duniani kote?
Uber One kwa sasa inapatikana Marekani, kukiwa na mipango ya kupanuka duniani kote. Kufikia sasa, manufaa ya Uber One yanapatikana Marekani pekee na hayatatumika kwa maombi yoyote ya programu ya Uber yanayotumwa ukiwa nje ya nchi.
- Je, uanachama wa Uber One unatumika kwa oda na safari zote?
Manufaa ya Uber One yanapatikana kwa maduka yanayostahiki yaliyowekwa aikoni ya Uber One kwenye programu. Bei za wanachama zimehakikishwa kwa safari zote zinazotimiza masharti, bila kujumuisha safari zilizowekwa dakika 30 au zaidi mapema au safari za pamoja. Tazama sheria na masharti ya ziada ya uanachama hapa.
- Gharama ya Uber One ni ya kiasi gani?
Tunatoa vifurushi maalum vya uanachama vya Uber One vilivyopunguzwa bei kwa wateja wa Uber for Business. Wasiliana na timu yetu ya wataalam ili kubinafsisha programu ya Uber One kwa ajili ya kampuni yako.
- Je, kampuni yangu hutozwa vipi kwa uanachama wa Uber One?
Kampuni itatozwa tu kwa uanachama unaodaiwa na wafanyakazi na itatozwa kila mwezi kulingana na mpangilio wa dashibodi yake. Hakuna malipo ya mapema kwa uanachama wa Uber One.
*Manufaa yanapatikana tu kwenye maduka yanayotimiza masharti yaliyo na aikoni ya Uber One. Kima cha chini cha $15 katika maduka mengi, kima cha chini cha $30 kwenye oda za mbogamboga. Punguzo la asilimia 5 halitumiki kwenye oda za mbogamboga. Uber One Promise inategemea makadirio ya Muda wa Mwisho wa Kuwasili na hubainishwa baada ya kuweka oda yako. Ofa za Uber One hazipatikani kwa safari ulizoweka mapema kwa dakika 30 au zaidi au kwa safari za pamoja. Huenda ukatozwa ada na malipo mengine. Kodi na ada, iwapo zipo, hazitumiki kwenye viwango vya chini vya oda.
Lazima uwe na umri wa miaka 21 au zaidi ili kukubali kupokea pombe iliyosafirishwa. Manufaa yanaweza kutofautiana kulingana na sheria na kanuni za eneo na jimbo. Uber ina haki ya kupunguza manufaa kutokana na wasiwasi wowote wa jimbo, serikali za mtaa au udhibiti kuhusiana na utoaji wa manufaa fulani.
Akiba ya uanachama iliyotumika kupunguza ada za huduma. Huenda ukatozwa ada na malipo mengine. Angalia sheria na masharti hapa..
Muhtasari
Kutuhusu
Huduma
Huduma
Kulingana na matumizi
Kulingana na tasnia
Usaidizi kwa wateja
Usaidizi
Nyenzo
Pata maelezo