Huenda ukatatizika wakati wa kujisajili au kupokea taarifa kutoka kwa mwanatimu wa mauzo. Tafadhali angalia tena, kwa sababu upatikanaji wa bidhaa unaweza kubadilika.
Nunua kadi za zawadi kwa wingi kwa ajili ya wateja na wafanyakazi
Kadi za zawadi ni njia bora ya kuzawadi timu yako na kumshukuru kila mtu aliye muhimu kwenye biashara yako.
Linganisha kadi za zawadi na Vocha
Unaweza kulipia safari na vyakula kwa njia kadhaa. Gundua mbinu inayokufaa.
- Muhtasari
Kadi za zawadi: Unanunua vocha ya Uber ili kuwapa wafanyakazi au wateja wako waitumie wanavyotaka.
Vocha: Unasambaza vocha za Uber kwa wafanyakazi au wateja na kulipia tu safari zilizofanyika au vyakula vilivyoagizwa. Pia unadhibiti vigezo na unaweza kufuatilia jinsi salio linavyotumika.
- Inafanya kazi vipi?
Down Small Kadi za zawadi: Unaweza kuwatumia wapokeaji kadi za kidijitali kupitia ujumbe, barua pepe au chapisho—unaamua jinsi ya kusambaza. Unaweza kununua kadi halisi za zawadi kupitia timu yetu ya mauzo. Nunua kadi hapa.
Vocha: Unasambaza vocha za Uber kwa wapokeaji na kuweka vidhibiti kama vile tarehe za mwisho, vizuizi vya eneo na/au siku na wakati ambapo vocha hizo zinaweza kutumika. Wapokeaji wanaweza kuomba safari au milo kutoka kwenye programu yao ya Uber au Uber Eats na kutumia vocha katika ununuzi wao. Unaweza kujisajili hapa.
- Ninawezaje kulipa?
Down Small Kadi za zawadi: Unalipa kiasi kizima cha thamani ya kadi ya zawadi wakati wa ununuzi.
Vocha: Unalipa tu wakati mtumiaji anakomboa vocha na anaitumia katika safari au mlo. Kwa mfano, ukisambaza vocha zenye thamani ya USD100 na USD50 tu zitumike, utalipa USD50.
- Kwa kawaida, biashara hutumiaje bidhaa hizi?
Down Small Kadi za zawadi: Baadhi ya njia ambazo kampuni hutumia kadi za zawadi: kuwapa wafanyakazi zawadi za likizo au mwisho wa mwaka, zawadi za shirika au kushukuru wateja, tuzo au zawadi nyingine.
Vocha: Baadhi ya njia ambazo kampuni hutumia vocha ni pamoja na kununua vyakula kwa ajili ya wanaohudhuria hafla za mtandaoni, kulipia gharama za safari kwenye biashara zao ili kuvutia wateja zaidi na kuwapa wateja chakula cha bei nafuu kwa sababu ya ununuzi wao.
Unaweza kununua na kutumia kadi za zawadi kwa urahisi
Haina ada za huduma au tarehe ya mwisho wa matumizi
Hutalipa pesa za ziada na wapokeaji hawatatozwa.
Kadi halisi au za kidijitali
Toa kadi pepe kwa njia ya ujumbe, barua pepe, chapisho, au upokee kadi halisi ili uzisambaze.
Vocha za vyakula na safari
Wapokeaji huchagua jinsi ya kutumia vocha zao, kwenye usafiri na mikahawa katika maelfu ya miji.
Inapatikana katika sarafu nyingi
Kadi za zawadi zinaweza kutumiwa katika sarafu nyingi, hivyo basi kuzifanya kuwa bora kwa timu na wasafiri wa kimataifa.
Ugawaji rahisi na kwa wingi
Sambaza mwenyewe kupitia faili nyingi au utumie huduma yetu ya barua pepe ya kadi ya zawadi.
Wasiliana na timu ya mauzo
Je, unahitaji kununua bidhaa zinazozidi $5,000 kwa kutumia kadi za zawadi? Unatafuta usaidizi kuhusu oda za sarafu nyingi au unajaribu kununua kadi halisi? Timu yetu iko tayari kukusaidia kupanga na kusambaza oda yako.
Jinsi kampuni zinavyotumia kadi zetu za zawadi
Manufaa na motisha kwa wafanyakazi
Tambua wafanyakazi ambao wamefanya kazi nzuri— kuwapa motisha na utendaji.
Zawadi za wateja kwa ajili ya ununuzi
Weka ofa kwenye kampeni zako za masoko kwa kuwapa wateja wapya au waliopo kadi za zawadi.
Kuboresha huduma kwa wateja
Ongeza uaminifu wa mteja kwa kuwapa zawadi maalumu zinazowafanya kujua kuwa wanathaminiwa.
Vyakula vya matukio ya mtandaoni
Wape chakula cha kutosha wanaohudhuria mikutano, warsha na semina za mtandaoni.
Vifuta jasho vya majibu ya utafiti
Boresha viwango vya majibu na mawasiliano kupitia kifuta jasho cha Uber Cash au vocha ya Uber.
"Kupitia ushirikiano wetu na Uber Eats, si tu kwamba tuliweza kutoa kadi za zawadi za $100 kwa wafanyakazi wa Coca-Cola North America, lakini pia tuliweza kuboresha uchumi na sekta za kusafirisha chakula na mikahawa."
Brian Sappington, Afisa Mkuu wa Ushirikishi wa Kidijitali, Coca-Cola North America
“Kutokana na mabadiliko ya haraka ya COVID-19 yaliyosababisha kusitishwa kwa muda kwa ligi ya NBA, tumekuwa tukijaribu kuwasiliana na wanachama na washirika wetu waaminifu. Kutuma kadi za zawadi za Uber ni suluhisho bora na tunafurahi kuona jinsi ambavyo zimepokelewa vizuri.”
Brandon Schneider, Afisa Mkuu wa Mapato, Golden State Warriors
“Wakati wafanyakazi wetu wanafanyia kazi katika maeneo mbalimbali, nilitaka njia ya kuwasiliana nao na kuwashukuru kwa bidii yao. Kila mtu anafahamu Uber Eats na kadi za zawadi ni njia bora ya kumshukuru papo hapo.”
Ashton Lubman, Mshirika wa Kampuni, 1-800-GOT-JUNK?
Maswali yaulizwayo mara kwa mara
- Je, wapokeaji wanaweza kutumia kadi za zawadi kwenye kila huduma inayopatikana katika Uber?
Down Small Ndiyo, kadi za zawadi, pindi zinapotumika kwenye akaunti, huwa Uber Cash au vocha ya Uber katika sehemu ya Wallet ya programu na zinaweza kutumiwa kulipia safari za Uber au vyakula kwenye Uber Eats.
- Je, kadi za zawadi hulipia kodi na ada?
Down Small Ndiyo, kadi za zawadi za Uber zitalipia kodi, ada au bakshishi kwa muamala wowote wa Uber.
- Kadi za zawadi zinapatikana wapi?
Down Small Kadi za zawadi zinapatikana nchini Australia, Brazili, Kanada, India, Meksiko, Afrika Kusini, Uingereza na Marekani. Sarafu zinazotumika ni pamoja na AUD, BRL, CAD, INR, MXN, ZAF, GBP na USD.
- Je, kadi za zawadi ni halisi au ni za kidijitali?
Down Small Kadi za zawadi ni za kidijitali kama chaguo-msingi (si halisi). Kadi halisi za zawadi zinapatikana tu nchini Marekani na sharti zinunuliwe kupitia timu yetu ya mauzo.
- Ninawezaje kutoa kadi hizo za zawadi?
Down Small Wapokeaji wanaweza kupata kadi za kidijitali kupitia ujumbe, barua pepe au chapisho—unaamua jinsi ya kusambaza. Tunaweza kutekeleza majukumu mazito kumtumia mpokeaji namba ya zawadi kupitia barua pepe au unaweza kuchagua kupokea kadi halisi za zawadi ili uzisambaze mwenyewe.
- Ninawezaje kulipia kadi za zawadi?
Down Small Unaweza kuchagua kulipa kwa kutumia ACH/uhamishaji wa kielektroniki kati ya benki au kupitia kadi ya benki katika masoko maalumu. Huenda taasisi yako ya benki ikakutoza ada ya kuhamisha fedha kwa njia ya kielektroniki.
- Ni fedha gani zinazopatikana?
Down Small Kuna kima cha chini na cha juu cha kiasi cha kadi ya zawadi katika kila nchi. Tunaweza kutunga misimbo ya zawadi za kidijitali kwa kiasi kingi kizima katika sarafu zozote zinazotumika. Tafadhali jadili masharti ya sarafu na timu yetu ya mauzo.
Muhtasari
Kutuhusu
Huduma
Huduma
Kulingana na matumizi
Kulingana na tasnia
Usaidizi kwa wateja
Usaidizi
Nyenzo
Pata maelezo