Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Tunajua kwamba, kwa karne nyingi, kuwa na uwezo wa kusafiri- kwenda kwenye maeneo salama, machaguo mazuri, huduma ya afya, fursa za kazi, haki sawa- haya hayatolewi kwa usawa. Leo kusafiri bado ni upendeleo, si haki.

Lakini haipaswi kuwa hivi. Tunaamini kwamba kusafiri kunaweza kusababisha mvurugo. Tangu Uber ianze, tumethibitisha hili mara kwa mara. Sasa, katikati ya janga la COVID na athari zake zinazozidisha ukosefu wa usawa duniani kote, ni muda sasa wa kuweka wazi ndoto yetu: kutoa fursa sawa ya kusafiri kwa wote.

Hii inarejelea dhamira yetu ya msingi: daima, bila kutulia tunatafakari upya jinsi ambavyo dunia inasafiri kwa mustakabali mzuri. Kwa kufanya hivyo, tunafanya kusafiri liwe jambo linalowezekana. Tunawawezesha watu kupata kazi wanayoweza kufanya wakiwa popote. Tunaziwezesha biashara kuwafikia wateja wapya. Tunasafirisha bidhaa muhimu kwa kutumia lori.

Wakati mwingine tumekosea. Lakini tumejizatiti kusonga mbele, katika mwelekeo mzuri kwa ajili ya watu na sayari. Tunaunda na kutekeleza mipango katika zaidi ya nchi 50 duniani kote, tukijenga uhusiano thabiti na jumuiya kupitia mtandao wetu wa matokeo ya kiulimwengu.

Ili kufanikisha ndoto yetu kubwa na kufanya kusafiri kuwe sawa kwa wote, kuna changamoto 4 za mtu binafsi, kijamii na kimazingira ambazo tunataka kuzishughulikia:

Uwezeshaji wa kiuchumi

Tunaamini katika kazi bora. Nchini Marekani tumeanzisha mbinu mpya kwenye kazi ya mtandaoni, ambayo urahisi wa kufanya kazi haupaswi kugharimu ulinzi ambao madereva na watu wanaosafirisha bidhaa wanatafuta. Hii inaonekana ulimwenguni kote, ikiwa ni pamoja na kampeni yetu yaMpango Bora barani Ulaya. Uber inawasaidia madereva na watu wanaosafirisha bidhaakufanikisha ndoto yao. Na tunawaheshimu kama Mashujaa wa Kila Siku.

Usalama

COVID-19 ilipojitokeza, sisi pia tulijitokeza. Tulionyesha mkazo wetu kuhusu usalama kwa kusafirisha vitu ambavyo ni muhimu. Tulitoa safari milioni 10 za bila malipo, vyakula na usafirishaji wa bidhaa kwa ajili ya wafanyakazi wa mstari wa mbele na jumuiya zilizo katika mazingira hatarishi. Hiyo ilijumuisha safari 50,000 za bila malipo kwa wale walio katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa nyumbani na unyanyasaji wa kijinsia. Kisha tukatoa safari nyingine milioni 10 za bila malipo au zilizowekewa punguzo ilikupata chanjo.

Uendelevu

Tuko njiani kuelekea kufikia uzalishaji sifuri wa hewa ya ukaa. Tumejitolea kuhakikisha kuwa, kufikia mwaka 2040, asilimia 100 ya safari duniani kote zinafanywa na magari yasiyozalisha hewa ya ukaa au kupitia vifaa vidogo vya usafiri na usafiri wa umma. Pia tumejizatiti kupunguza matumizi ya mara moja ya plastiki kwa kufanya vyombo vya chakula kuwa hiari kwenye Uber Eats. Tulizindua bidhaa za pikipiki za umeme nchini Kenya, kampeni za migahawa endelevu nchini Ufaransa na hata mkataba wa ununuzi wa nishati jadidifu na shamba la upepo huko Texas.

Usawa

Uber ni kampuni inayopinga ubaguzi. Tumetoa ahadi 14 (na zaidi kwa sasa) ambazo zinashughulikia hatua mbalimbali—kuanzia kuepusha jukwaa letu kuwa na ubaguzi hadi kusimamia usawa katika jumuiya yetu. Kama sehemu ya kusimamia usawa katika jumuiya, tulitenga Dola milioni 10 ili kusaidia biashara zinazomilikiwa na watu Weusi duniani kote. Pia tunasimama kwa umoja pamoja na jumuiya ya Kiasia na tunaweka mipango ili tutoe mafunzo ya kupinga ubaguzi. Na zaidi.

Pata maelezo zaidi kuhusu kile tunachofanya, kile tulichofanikiwa na kile ambacho tumejizatiti kufanya, kupitia visa tunavyoshiriki hapa.

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Hatua tunazochukua

We focus on taking actions to have a positive 
impact in the world.

Safari milioni 10 za bila malipo, chakula na kusafirisha bidhaa

Ulimwengu uliposimama wakati wa wimbi la kwanza la janga la ugonjwa, tulijitokeza tukiwa na safari za bila malipo milioni 10, chakula na usafirishaji wa bidhaa.

Usalama kwa wanawake

Kutoa safari 50,000 bila malipo na chakula kwa wale walio katika hatari ya kufanyiwa unyanyasaji na ukatili wakati wa janga la ugonjwa.