Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Safari milioni 10 za bila malipo, chakula na kusafirisha bidhaa

Ulimwengu uliposimama wakati wa wimbi la kwanza la janga la ugonjwa, tulijitokeza tukiwa na safari za bila malipo milioni 10, chakula na usafirishaji wa bidhaa.

COVID-19 ilibadilisha kabisa maisha yetu yote pamoja na biashara yetu. Mnamo Machi 2020, Uber—kampuni inayowezesha usafiri—iliwaomba wasafiri kwenye tovuti yetu kuacha kusafiri. Tuliwahimiza wabaki nyumbani, ili tuweze kusaidia kusafirisha bidhaa muhimu: kusaidia kuwapeleka wahudumu wa dharura kazini, chakula kwa wazee na vifaa vya dharura kwa wahudumu wa mstari wa mbele, wote kama sehemu ya ahadi yetu ya kuchangia safari milioni 10 za bila malipo, chakula na kusafirisha bidhaa kwa wale wenye uhitaji kote ulimwenguni.

Miezi mitatu baadaye, safari hizo milioni 10 na usafirishaji wa bidhaa ulikuwa umetimizwa. Kwa sababu hiyo, madaktari wangeweza kufika kazini nchini India. Familia zilizo katika mazingira hatarishi zilipokea vifurushi vya chakula huko Meksiko. Na waathiriwa wa ukatili wa nyumbani wangeweza kusafiri kwenda kwenye makazi na sehemu salama. Kote ulimwenguni, Uber ilishirikiana na mashirika zaidi ya 200 katika nchi 54 ili kujitokeza kwa ajili ya wale ambao wanahitaji msaada. Hii ni mifano 3 tu ya uvumbuzi wetu, unaoendesha mtandao wetu wenye matokeo ulimwenguni kote:

Wakfu wa Bill na Melinda Gates (Afrika Kusini)

Uber ilisambaza zaidi ya maagizo milioni 1.4 ya dawa kwa wagonjwa wanaokaa nyumbani wakati wa janga, mpango ulioongozwa na Idara ya Afya ya Western Cape ikisaidiwa na Wakfu wa Bill na Melinda Gates.

NHS (Uingereza)

Tulitoa safari 300,000 za bila malipo na chakula kwa wafanyakazi wa NHS katika wimbi la kwanza la janga la ugonjwa wakati Uingereza ilikuwa imesitisha shughuli.

World Central Kitchen (Marekani)

Tuliwezesha usafirishaji wa milo zaidi ya 300,000 ikiwa bado moto huko Bronx, NY; Newark, NJ na Washington, DC, kwa jumuiya zilizokuwa hatarini ambapo watu walipaswa kukaa nyumbani kwa sababu ya janga la ugonjwa.

Safari na usafirishaji huu wote wa bidhaa usingewezekana bila mamilioni ya madereva na watu wanaosafirisha bidhaa kwenye tovuti ya Uber, ambao wenyewe walikuwa wafanyakazi wa mstari wa mbele, wakisaidia jumuiya zetu kuendelea na shughuli zake wakati wa janga hili lisilo na kifani. Na kipaumbele cha juu kilikuwa kufanya kila tuwezalo ili kuwaweka salama. Tukitambua hatari walizokabiliana nazo, tuliwekeza zaidi ya USD milioni 50 katika Vifaa vya Kujikinga (PPE) na tukaweka harakaSera ya bila barakoa, hakuna safari, tukitumia teknolojia yetu ili kusaidia kushurutisha uwajibikaji. Tulikuwa wa kwanza katika tasnia yetu kutoa msaada wa moja kwa moja wa kifedha kwa madereva na watu wanaosafirisha bidhaa ambao walipatikana kuwa na COVID-19 na tulifanikiwa kuwatetea madereva kujumuishwa katika hatua za serikali za kuimarisha uchumi.

Ingawa janga la ugonjwa liliharakisha kukuballika kwa usafirishaji wa chakula, bado ulikuwa wakati mgumu sana kwa mikahawa. Kwa kweli, madereva hawakuwa watu pekee ambao waliathiriwa kifedha na shida hiyo. Kwa kuwa mamilioni katika tasnia ya mikahawa waliathiriwa sana, tulitoa mchango wa USD milioni 6 kwa Mfuko wa Usaidizi kwa Wafanyakazi wa Mikahawa nchini Marekani, tukazindua kipengele cha mchango wa ndani ya programu ambacho kiliweka zaidi ya USD milioni 20 kwenye akaunti za benki za mikahawa na kutangaza ruzuku za USD milioni 4.5 kwa biashara za Marekani zilizokuwa zinapitia hali ngumu. Tuliweka pia vipengele vipya vya programu vilivyobuniwa kutosheleza mahitaji ya mikahawa yaliyokuwa yakibadilika kote ulimwenguni.

Pata maelezo zaidi kuhusu safari zetu milioni 10 za bila malipo na zilizo na punguzo kwa ajili ya kwenda kupatachanjo.

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Safari kwa ajili ya kwenda kupata chanjo

Kuanzia kwa walimu hadi wazee, tunasaidia kuhakikisha kuwa usafiri si kikwazo cha kupokea chanjo ya COVID-19.

Kutovumilia kabisa ubaguzi wa rangi

Ubaguzi wa rangi na ubaguzi hauna nafasi katika ulimwengu wetu—haya ndiyo tunayofanya ili kupambana nao.