Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Usalama kwa wanawake

Kutoa safari 50,000 bila malipo na chakula kwa wale walio katika hatari ya kufanyiwa unyanyasaji na ukatili wakati wa janga la ugonjwa.

Ripoti zimeonyesha kuwa ukatili dhidi ya wanawake uliongezeka kwa hadi asilimia 20 wakati wa janga la ugonjwa.

Tuliyaunga mkono mashirika ya kupambana na ukatili wa nyumbani na serikali za maeneo husika ulimwenguni kote ili kutoa zaidi ya safari 50,000 bila malipo kwa makazi na sehemu za usalama na zaidi ya milo 45,000 bila malipo kwa wale walio katika hatari.

Haya yote hayangewezekana bila ujuzi na utaalamu wa washirika wetu, ambao si tu wanatuelimisha, bali pia wanawasaidia bila kuchoka wale wanaoteseka. Ushirikiano mwingi kama huo upo ulimwenguni kote; hapa tunaangazia 3 kutoka Ufaransa, Uingereza na Brazili.

Collectif Féministe Contre le Viol (Ufaransa)

Uber ilitoa usafiri bila malipo ili kuwawezesha waathiriwa wa dhuluma ya kingono kupata msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia. Safari za kwenda kwenye miadi muhimu ya kisheria, kesi mahakamani na mikutano mingine huenda ilikuwa changamoto za kawaida kwa wanawake hawa kwa sababu ya gharama, umbali na mipango.

Hestia (Uingereza)

Tulitoa usafiri bila malipo pamoja na ufadhili kwa Hestia, mmojawapo wa watoa huduma wakubwa zaidi wa usaidizi kwa waathiriwa wa dhuluma za nyumbani huko London na Kusini Mashariki, Uingereza. Mwaka 2020, iliwasaidia wanawake na watoto 2,800 kupata ahueni kutokana na kiwewe cha dhuluma za nyumbani.

Instituto Avon (Brazili)

Tuliunga mkono uundaji wa Angela, roboti ya gumzo inayopatikana kupitia WhatsApp, iliyozinduliwa wakati wa janga la ugonjwa ili kuwaruhusu wanawake kuomba msaada kwa njia ya faragha. Aidha, kwa kutumia misimbo ya Uber Promo, wanaweza kutembea kwa uhuru zaidi ili kutafuta msaada.

Mifano iliyo hapo juu inawakilisha mashirika machache tu yanayoshughulikia matatizo ya ukatili dhidi ya wanawake nchini Ufaransa, Uingereza na Brazili na njia zetu bunifu za kufanya kazi pamoja.

Pata maelezo zaidi kuhusumipango yetu mipya kote ulimwenguni, ahadi zetu za usalama, Ripoti ya Usalama ya Marekani na kazi yetu nchini Brazili.

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Safari kwa ajili ya kwenda kupata chanjo

Kuanzia kwa walimu hadi wazee, tunasaidia kuhakikisha kuwa usafiri si kikwazo cha kupokea chanjo ya COVID-19.

Kutovumilia kabisa ubaguzi wa rangi

Ubaguzi wa rangi na ubaguzi hauna nafasi katika ulimwengu wetu—haya ndiyo tunayofanya ili kupambana nao.