Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Njia bora ya kufanya kazi

Kuwasaidia madereva na watu wanaosafirisha bidhaa kote ulimwenguni ili kuwasaidia kufanikisha malengo yao.

Huku athari za janga la COVID-19 zikishuhudiwa, ni madereva na watu wa kuwasilisha bidhaa ndio waliendeleza shughuli za ulimwengu. Huku wengi wetu tukishauriwa kukaa nyumbani na kupunguza utangamano na watu wengine, jukumu lao lilikuwa muhimu katika kutusaidia kupata bidhaa tulizohitaji au kufika kwenye maeneo muhimu ambayo tulihitaji kwenda.

Hapo awali kabla ya kipindi hiki cha janga la ugonjwa, haikuwa dhahiri jinsi madereva na watu wa kusafirisha bidhaa huwa muhimu kwa mifumo ya miji na jumuiya. Hawasafirishi watu, vyakula na bidhaa kutoka eneo moja hadi jingine tu—pia wanaleta mabadiliko katika maisha ya watu. Huenda walichukua muda kumsikiliza abiria ambaye alikuwa na siku mbaya au wakasimama kwenye lango la bustani wakati wa uwasilishaji wa chakula ili kuwa na gumzo muhimu na mzee mkazi wa eneo hilo.

Hii ndiyo sababu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wetu amesema kuwa wafanyakazi wa kazi za muda wanastahili maisha bora. Ndiyo sababu tumetangaza Ofa Bora kwa wale walio Ulaya. Ndiyo sababu tunashirikiana na vyuo vikuu ili kutoa programu za digrii bila malipo, kama zile tunazoshirikiana na ASU na Chuo Kikuu Huria. Pia ndiyo sababu tunafanya kadiri ya uwezo wetu kuwasaidia madereva na wafanyakazi wa kusafirisha bidhaa ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao kote ulimwenguni.

Kuendesha mchakato wenye usawa wa kuhamia kwenye matumizi ya magari ya umeme

Kando na huduma yetu ya Uber Green na ahadi yetu ya kutumia magari yasiyotoa hewa ya ukaa kufikia mwaka 2040, tunashirikiana na EVNoire na GRID Alternatives nchini Marekani ili kubuni mipango ya majaribio na kuhakikisha kwamba madereva wasio Weupe na wanaotoka jumuiya zilizotengwa wanaweza kupata magari ya umeme.

Kutoa mipango ya elimu ya kifedha kwa madereva na watu wanaowasilisha bidhaa

Ili kuwawezesha madereva na wafanyakazi wanaosafirisha bidhaa wafanikiwe, tunabuni mipango ya kusaidia kuboresha hali zao za kifedha na kuwaandaa kwa ajili ya mustakabali wa kazi. Katika Amerika ya Kati na ya Kusini, tulizindua Avanza kwa ushirikiano na IFC. Nchini Kenya, tulianzisha mpango waNavigate tukishirikiana na AMI. Pia tunafanya kazi na Operation HOPE ili kufanikisha mpango kama huo nchini Marekani.

Kutoa stadi na fursa za kibiashara barabarani na kwingineko

Madereva na watu wengi wanaosafirisha bidhaa ambao ni wajasiriamali wanajiunga na jukwaa letu. Nchini Uingereza, tunashirikiana na Enterprise Nation kuendesha mpango wa Kujenga Biashara ili kutoa mafunzo na ufadhili wa hadi £10,000 utakaotumika kuendeleza mawazo mapya ya kibiashara. Nchini Afrika Kusini, tunasaidia Lularides katika kutoa mafunzo ya kuendesha pikipiki kwa vijana kutoka jamii zilizotengwa ili waweze kujiunga na jukwaa la Uber Eats.

Kama sehemu ya ndoto yetu ya kufanya usafiri uwe sawa kwa wote, tumejitolea kutoa fursa nzuri kwa madereva na watu wanaosafirisha bidhaa ulimwenguni kote.

Pata maelezo zaidi kuhusu mtindo wetu mpya kwa ajili ya kazi zinazoendeshwa kupitia jukwaa.

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Biashara za Watu Weusi ni muhimu

Kusaidia biashara za Watu Weusi kote ulimwenguni.

Kuwashukuru madereva wote na watu wanaosafirisha bidhaa

Maelfu ya madereva na wafanyakazi wanaosafirisha bidhaa waliendelea kusafirisha bidhaa muhimu wakati wa janga la ugonjwa.