Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Maendeleo huleta haja ya uvumbuzi

Tunaongoza mipango ya kipekee na uhamasishaji katika zaidi ya nchi 50 kote ulimwenguni, mara nyingi tukishirikiana na wengine. Fahamu mfumo wetu wa duniani kote wa kuleta mabadiliko.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC)

Shirika la IFC limeshirikiana na Uber katika juhudi za kuongeza fursa kwa wanawake katika masoko yanayoibuka, ikijumuisha kuwakutanisha viongozi wa sekta binafsi ili kujadili masuala ya jinsia na kuchambua data ili kuelewa vyema zaidi kuhusu jinsi kusafiri kwa watu wengi katika gari moja kunavyoweza kuongeza fursa za kazi kwa wanawake na kurahisisha usafiri.

Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC)

Uber huipa IRC—shirika la kibinadamu la kimataifa linalosaidia watu wanaolazimika kukimbia maeneo yenye mizozo na migogoro—huduma salama na za kutegemewa za usafiri kupitia safari zisizo na malipo kwa wafanyakazi wa IRC na jumuiya zilizo katika mazingira magumu zinazohudumiwa na wafanyakazi hao. Safari kwenye Uber ni nyenzo muhimu kwa wakimbizi na watu waliohamishwa makwao ambao wanajenga maisha yao upya.

LISC

Mashirika ya LISC, Uber, PayPal Giving Fund na Walgreens yameungana kuunda Hazina ya Ufikiaji wa Chanjo, ambao ni mpango wa dola milioni 11 unaoshughulikia tatizo la ukosefu wa usawa katika huduma za afya na kuwezesha watu kupata usafiri wa kwenda kwenye maeneo ya chanjo kwa watu ambao hawawezi kujifikisha huko. Shirika la LISC litasimamia Hazina ya Ufikiaji wa Chanjo kwa kufanya kazi, kama lilivyofanya kwa miaka 40, kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii yasiyotengeneza faida na vikundi vingine ili kuanzisha na kuunga mkono mpango wa safari za bure.

Partners In Health

Uber inashirikiana na shirika la Partners In Health ili kutoa safari kwa jumuiya zisizo na ufikiaji wa kutosha wa huduma, ambazo zinahitaji chanjo za COVID-19 na kuhakikisha kuwa usafiri sio kikwazo kwa ufikiaji wa chanjo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)

Uber inashirikiana na Muungano wa Elimu ya Dunia wa UNESCO ili kuhakikisha kwamba walimu na familia zenye matatizo ya kifedha zinaweza kupata usafiri bila malipo wakati shule zitafunguliwa. Kama sehemu ya ushirikiano huo, Uber pia imesaidia kuwezesha uwasilishaji wa zaidi ya milo 400,000 isiyolipiwa na vifurushi vya chakula kwa familia huko Kolombia, Kosta Rika, Kenya, Meksiko, Panama na Uingereza.

World Central Kitchen (WCK)

Uber ilishirikiana na World Central Kitchen kuwezesha uwasilishaji wa milo 300,000 katika maeneo ya Washington, DC; Bronx, NY; na Newark, NJ, kwa jumuiya zilizokuwa hatarini ambazo zilikuwa zimezuiliwa nyumbani kwa sababu ya janga la ugonjwa.

Haya ni baadhi tu ya mashirika kutoka kote ulimwenguni ambayo tumeshirikiana nayo:

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Hatua tunazochukua

We focus on taking actions to have a positive 
impact in the world.

Safari milioni 10 za bila malipo, chakula na kusafirisha bidhaa

Ulimwengu uliposimama wakati wa wimbi la kwanza la janga la ugonjwa, tulijitokeza tukiwa na safari za bila malipo milioni 10, chakula na usafirishaji wa bidhaa.