Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Chaguo za safari kwenye ukurasa huu ni mfano wa bidhaa za Uber na huenda baadhi ya bidhaa zisipatikane mahali ambapo unatumia App ya Uber. Ukiangalia ukurasa wa wavuti wa jiji uliko au uangalie kwenye App, utaona usafiri unaoweza kuitisha.

X small

UberX Share

Ukiwa na UberX Share, pata kila kitu unachopenda kuhusu UberX kwa bei nafuu zaidi— okoa hadi asilimia 20 unapounganishwa na msafiri njiani. Angalia sheria na masharti.*

search
Weka mahali
Navigate right up
search
Weka mahali unakoenda

Sababu ya kuenda kwa UberX Share

Okoa pesa

Ukiwa na UberX Share unaweza kuokoa hadi asilimia 20 unapokutanishwa na msafiri kwenye njia yako. Angalia masharti.*

Zingatia ratiba

UberX Share imeundwa ili kuongeza dakika zisizozidi 8 kwenye safari yako kwa wastani.

Kuwa na busara ya hali ya hewa

Lisaidie jiji lako kuepuka uchafuzi wa ziada na usafiri wa gari kwa kushiriki safari yako.

Imeundwa ili kukusaidia kuendelea kusonga mbele

Omba kiti kimoja pekee

Unaweza kuomba kiti kimoja tu na UberX Share. Ikiwa unasafiri na rafiki au kikundi cha marafiki, fikiria kuomba UberX au UberXL.

Tunasasisha sera yetu ya kuketi kwenye kiti cha mbele

Wasafiri hawatatakiwa tena kuketi kiti cha nyuma. Hata hivyo, ili kumpa dereva wako nafasi, tunaomba utumie kiti cha mbele tu ikiwa unakihitaji.

Kuwa msafiri wa nyota 5

Mwongozo wetu unakuomba uwatendee madereva na waendeshaji wenza kwa heshima, kufuata sheria na kusaidiana kulindana. Ukiukaji wa Mwongozo wetu wowote wa Jumuiya unaweza kusababisha kuondolewa kwa idhini yako ya kufikia akaunti zako za Uber.

Utaratibu wa UberX Share

1. Ombi

Fungua programu ya Uber, weka unakoenda, na usogeze chini hadi kwenye chaguo la usafiri la UberX Share.

2. Safari

Programu itajaribu kukutanisha gari lako na wasafiri wengine wanaoelekea mahali unakoenda. Okoa pesa zaidi ikiwa utakutanishwa na msafiri mwenza. Angalia masharti.*

3. Shuka

Ikiwa safari yako ilikuwa na nyota 5, unaweza kumshukuru dereva wako na kumpa bakshishi kwenye programu baada ya safari yako.

Maswali yanayoulizwa sana

  • Utasafiri na abiria mwingine mmoja tu wakati wowote kwenye safari yako. Ikiwa msafiri mwenza atashushwa mbele yako, kuna uwezekano programu itatafuta msafiri mwenza mwingine, lakini imeundwa kutafuta watu wanaokwenda upande wako ili kuepuka kuongeza zaidi ya dakika 8 kwenye safari.

  • UberX Share imeundwa ili kuongeza si zaidi ya dakika 8 kwenye safari yako (kumbuka: kwa sababu ya trafiki na ucheleweshaji mwingine unaowezekana, hatuwezi kukuhakikishia saa za kuwasili). Utaona wakati unaotarajiwa kuwasili katika programu unaposafiri.

  • Mpangilio wa kuwachukua na kuwashukisha wasifiri hutegemea eneo unakoenda kwenye barabara, wala si mpangilio wa aliyechukuliwa kwanza.

  • Programu inakulinganisha na wasafiri wanaoenda upande wako ili kusaidia kuhakikisha kuwa kuchukuliwa kokote kwa ziada hakutaongeza muda unaokadiriwa wa kuwasili kwa zaidi ya dakika 8.

  • Inategemea nafasi iliyo kwenye gari na idadi ya wasafiri. Ikiwa unasafiri na mizigo, tunapendekeza uombe usafiri wa UberX badala ya UberX Share.

Maelezo zaidi kutoka Uber

Safiri kwa gari unalotaka.

1/8

Nyenzo iliyo kwenye ukurasa huu wa wavuti ni kwa madhumuni ya taarifa pekee na huenda isitumike katika nchi, kanda au mji wako. Inaweza kubadilika na huenda tukaibadilisha bila kukuarifu.

Kila mtu anayetumia tovuti ya Uber anatakiwa kutii sheria na kanuni husika anapofanya hivyo.

*Ofa hii inatumika tu kwa wasafiri wanaoomba UberX Share na wanakutanishwa na msafiri mwenza. Kukutanishwa na msafiri mwenza kunategemea wakati wa siku, msongamano wa magari, idadi ya maombi ya safari na idadi ya madereva wanaopatikana katika eneo fulani. Wasafiri wanaotumia UberX Share wataokoa kima cha chini cha pesa na wanaweza kupata zaidi kulingana na muda na umbali wanaosafiri na msafiri mwenza. Angalia programu ili upate maelezo.