Sababu za kutumia UberXL kusafiri
Linaweza kubeba wasafiri 6 (au mizigo mingi) vizuri
Bei za kawaida
Magari na SUV yenye nafasi ya kutosha
Jinsi ya kusafiri kwa UberXL
1. Ombi
Fungua App na uweke mahali unakoenda katika kisanduku cha "Unaenda wapi?". Ukishathibitisha eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda, chagua UberXL kwenye sehemu ya chini ya skrini yako. Kisha, bonyezaThibitisha UberXL.
Baada ya kukutanishwa na dereva, utaona picha yake na maelezo ya gari, na unaweza kumfuatilia kwenye ramani anapokuja kukuchukua.
2. Safari
Hakikisha kwamba maelezo ya gari yanafanana na maelezo unayoona kwenye App kabla ya kusafiri kwa UberXL.
Dereva wako anajua unakoenda na ana maelekezo yatakayokufikisha kwa haraka, lakini unaweza kumwomba atumie barabara unayopenda.
3. Shuka
Malipo yatatozwa kiotomatiki kwa kutumia njia ya malipo uliyoweka kwenye akaunti yako, kwa hivyo unaweza ukashuka kwenye UberXL bila wasiwasi pindi unapofika uendako.
Kumbuka kumtathmini dereva wako ili Uber iendelee kuimarisha usalama kwa manufaa ya kila mtu.
Safiri vizuri kwa Uber Reserve
Kamilisha mipango yako leo kwa kuweka nafasi ya usafiri. Omba safari yako hadi siku 90 mapema ukitumia Uber Reserve, ili usiwe na wasiwasi kuhusu kufika huko.
Safari kote ulimwenguni
Kuna njia zaidi ya moja ya kusafiri ukitumia Uber, haijalishi mahali ulipo au unakokwenda baadaye. Angalia programu ili uone ni machaguo yapi ya safari yanayopatikana karibu nawe.*
Uber Electric
Safari zisizo na uzalishaji wa hewa chafu kwa kutumia magari ya umeme
UberX Share
Safiri pamoja na hadi msafiri mmoja kwa wakati mmoja
Uber Transit
Maelezo ya usafiri wa umma kwa wakati halisi kwenye programu ya Uber
Baiskeli
Baiskeli za umeme pale unapozihitaji ambazo hukuruhusu kwenda mbali zaidi
Uber Comfort
Magari mapya zaidi yaliyo na nafasi ya kutosha ya kuweka miguu
Uber Black SUV
Safari za starehe kwa watu 6 katika magari ya kifahari ya SUV
Nyenzo iliyo kwenye tovuti hii ni kwa madhumuni ya taarifa pekee na huenda isitumike katika nchi, eneo au mji ulipo. Inaweza kubadilika na huenda tukaibadilisha bila kukuarifu.
¹ Unapoomba safari ya Uber Reserve, bei ya safari unayoona itakuwa makadirio yanayojumuisha ada ya kuweka nafasi inayoweza kutofautiana kulingana na eneo la kuchukuliwa na/au siku na saa ya safari yako. Ada hii hulipwa na wasafiri kwa muda wa ziada ambao dereva wao anasubiri na umbali au muda anaotumia kusafiri hadi eneo la kuwachukua.
Kuhusu
Kuhusu