Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Fursa nyingine

Je, kuwa na historia ya uhalifu kunafaa kukuzuia usiajiriwe?

Tunaamini kwamba jibu ni hapana. Zaidi ya Wamarekani milioni 70 wana rekodi za uhalifu, hali inayoweza kufanya iwe vigumu kwao kuajiriwa na kujitengenezea hela. Uber ni miongoni mwa idadi inayoongezeka ya kampuni na watunga sera waliojitolea kuwapa watu fursa ya pili.

MCHANGO WETU

Kuunga mkono mipango inayobadilisha urudiaji wa makosa

Tunaunga mkono harakati zinazosaidia kutoa fursa kwa kila mtu anayetaka—na kustahiki—kupewa fursa ya pili maishani.

Uber imekuwa ikiondoa ‘visanduku vya kuteua makosa’ kila wakati

Waajiri wengi wana kisanduku cha kuteua kwenye fomu ya kuomba kazi, ambapo wanaotafuta kazi huulizwa iwapo wana historia ya uhalifu. Unapoomba kazi za shirika katika Uber, visanduku hivyo havipo. Kwa hakika, tunahimiza kampuni nyingine kurekebisha hatua zao za kuajiri ili kupunguza ubaguzi na kuhakikisha nafasi sawa kwa wanaoajiriwa.

Pia tumeahidi kusaidia

Mwaka 2016, tulitia saini ahadi ya White House Fair Chance Business Pledge, hivyo kujiunga na utawala wa Obama pamoja na kampuni nyingine zaidi ya 200 kutoka tasnia za teknolojia, mauzo ya rejareja na vyakula na vinywaji katika kuondoa vikwazo kwa watu walio na historia za uhalifu.

Masimulizi

Kosa moja halifai kumfanya mtu aadhibiwe maishani mwote. Katika Uber, tumejitolea kufanya kazi na jamii tunakohudumia ili kusaidia kuboresha fursa zetu kwa wanaozihitaji zaidi. Iwe ni kupata usafiri wa uhakika kutoka sehemu moja hadi nyingine mjini au uwezo wa kulipia bili mwisho wa mwezi, fursa hizo zinafaa kupatikana kwa kila mtu. Tumeshuhudia jinsi hali ya kupata fursa ilivyo muhimu kwa mtu na jinsi maisha ya mhusika yanavyoweza kubadilika kuwa mazuri.

Mama, bibi, mtetezi

Ingrid ni mama na bibi. Baada ya kufungwa kwa kosa lisilo la vurugu, aliachiliwa mapema na sasa anawasaidia wanaume na wanawake ambao walikuwa wamefungwa jela, waanze kujipatia riziki mjini Los Angeles. Pia anaendesha gari akitumia mfumo wa Uber.

”Ni rahisi sana kwangu kutaka kufanya kazi na kwa sababu nina watoto, kila wakati nina jambo la kufanya na watoto … na nina hakika kwamba bado ninaweza kukidhi mahitaji.”

Mjasiriamali wa kisasa

Darrington anafanya kazi ya kuuza mashamba na pia ni dereva wa Uber. Amekwenda maelfu ya safari na hupokea tathmini ya nyota nyingi kutoka kwa wasafiri. Ilimchukua miaka kupata leseni ya kufanya kazi katika sekta ya kuuza mashamba baada ya kufungwa gerezani. Darrington hayuko peke yake. Kote nchini Marekani, mamilioni ya watu wanahangaika kutokana na adhabu za makosa waliofanyia jamii zamani. Utafiti unaonesha kwamba hali ya kuwa na historia ya kuwahi kufungwa gerezani kwa sababu yoyote hupunguza uwezekano wa kupata kazi kwa asilimia 50.

"Unafaa kuwapa watu nafasi ya pili ili waweze kudhihirisha uwezo wao."

Kusaidia jamii

1/3