Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Fursa za kiuchumi

Je, kila mtu anaweza kuboresha mapato yake? Ndiyo.

Hata wakati ambapo kuna uhaba wa kazi na sekta zisizo thabiti, miji ambapo Uber inahudumu huwa na fursa za kujitengenezea mapato, kwa hivyo watu wanaweza kujikimu.

MCHANGO WETU

Kubuni fursa za kazi

Uber inawasaidia watu kupata nafuu katika gharama za kiuchumi kwa kuwapa fursa za kujitengenezea hela, kufanya kazi kwa muda unaowafaa na kuwapa nyenzo zinazowawezesha kupokea mapato zaidi.

Uber inakupa njia ya kuondoka kwenye vitongoji duni vya Ufaransa

Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa madereva wengi wanaotumia App ya Uber nchini Ufaransa, ambao hawakuwa na ajira awali, wanatoka sehemu duni zaidi za Paris, Uber ilitajwa na Financial Times kama “njia ya kuondoa watu kwenye kitongoji duni.” Isitoshe, katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2016, asilimia 25 ya fursa za kupata pesa katika eneo la Paris zilitokana na mifumo ya usafiri kama vile Uber.

Uber inaweza kuwa kitulizo kwa wafanyakazi wanaojitegemea

Utafiti uliofanywa na JPMorgan Chase Institute ulionesha kuwa wafanyakazi wanaojitegemea, wanaotumia mifumo kama Uber, waliweza kutumia mapato yaliyotokana na App, kujazia upungufu katika mapato yao.