Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Mikahawa ya muda huko Harlem, New York

Kusaidia mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi kuendelea kufanya kazi katika miezi ya majira ya baridi.

Mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi iliathiriwa vibaya na COVID-19. Ili kusaidia mikahawa na biashara zinazomilikiwa na Watu Weusi kuendelea kufanya kazi katika majira ya baridi ya mwaka 2020, tulishirikiana na Valerie Wilson wa Valinc PR, Nikoa Evans-Hendricks wa Harlem Park to Park na EatOkra ili kuunda mandhari ya kulia chakula kwenye sehemu ya nje katika kitongoji cha kihistoria cha Harlem, New York, Marekani. Likiwa katika eneo la Renaissance Pavilion katika Strivers’ Row, jengo hili lilikuwa na mikahawa 6 inayojitegemea kwa kutoa sehemu salama, yenye ukarimu na ya kirafiki ya kuweza kuketi nje.

Tunawezesha mikahawa ya muda na mandhari ya mikahawa ambayo yanaonyesha chakula chao cha kushangaza kwa wateja wapya, ili kuongeza uwepo wao kwenye tovuti yetu na kuhakikisha kuwa wanaendelea kusaidiwa kwa njia ambayo itawasaidia kushamiri.

Kila sehemu iliunganishwa na mchoro wa mmoja kati ya wasanii 6 waliopewa kazi ya kuchora ambao pia walifanya kazi kwenye mchoro wa ukutani wa Harlem Black Lives Matter katika majira ya joto ya mwaka 2020. Kikanza na mfumo wa hewa safi ulichangia starehe ya oda ya chakula cha kulia hapo kwa ajili ya mikahawa na biashara hizi.

  • Alibi Lounge

    Mojawapo ya baa chache za LGBTQ+ zinazomilikiwa na Watu Weusi huko New York inamilikiwa na kuendeshwa na Alexi Minko, mhamiaji Mweusi basha kutoka Gabon ambaye ameunda sehemu ya kufurahisha, ya kifahari, ya faragha na salama kwa ajili ya jumuiya ya LGBTQ+. Wote wanakaribishwa kwenye Alibi, ni maarufu jijini kwa ajili ya kokteli zake za kipekee ambazo zimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu.

  • Kiwanda cha Chokoleti cha Harlem

    Pipi za chokoleti, peremende, vipande vya chokoleti na kadhalika: Jessica Spaulding, mwanzilishi wa Kiwanda cha Chokoleti cha Harlem, hutengeneza pipi zinazohamasishwa na urithi tajiri wa kikabila wa jumuiya ya Harlem.

  • Ma Smith’s Dessert Café

    Duka hili la mikate linaloendeshwa na familia huchanganya keki tamu zilizotengenezwa nyumbani na vitindamlo na ukarimu wa kirafiki wa eneo la Kusini la Marekani. Mapochopocho ya zamani yanawekwa pamoja na vyakula vipya, ikiwemo keki ndogo za kahawia za mahameli.

  • Ruby’s Vintage

    Mkahawa huu maridadi na wa kuvutia wenye muundo wa kale uliopewa jina la mwigizaji na mwanaharakati wa haki za raia, Ruby Dee, hujivunia kuwa na muziki mtamu na mazungumzo mazuri.

  • Sexy Taco

    Nyongeza za kufurahisha kwenye mapishi ya Cal-Mex huandaliwa hapa. Wateja husafiri kutoka kote mjini kwa ajili ya burrito ya kipekee na margarita tamu.

  • The Row Harlem

    Chakula cha saa tano asubuhi cha samaki na uji wa unga wa mahindi, chakula cha jioni cha empanada ya uduvi, makaroni na jibini ya kamba na tambi ikiwa kando na kokteli moja au 2 baadaye—The Row hujishughulisha na chakula kinachotoka baharini kilichojaa ladha na kufanyiwa marekebisho yenye hisia nyingi.

1/6

Wamiliki wa mikahawa hii walielezea kuwa sehemu hiyo ilisaidia biashara zao kuendelea kufanya kazi katika wakati mgumu sana. "Uber Eats kweli imeweka kiwango cha jinsi mashirika na jumuiya zinavyoweza kushirikiana kuunda mikakati na suluhisho za kusaidia biashara ndogo ndogo," anasema Brian Washington-Palmer, mmiliki mwenza wa Ruby’s Vintage. "Lengo la mpango huu wa kitaifa kwenye mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi linaonyesha jinsi Uber Eats inavyoelewa mahitaji ya jumuiya inayoihudumia na athari ya janga la ugonjwa kwa jumuiya za Watu Weusi kihususa."

Tembelea mikahawa mizuri tunayosaidia huko Harlem.

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Biashara za Watu Weusi ni muhimu

Kusaidia biashara za Watu Weusi kote ulimwenguni.

Mikahawa ya muda huko Washington, DC

Kuiwezesha mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi kupanua biashara zake katika kitongoji kipya.