Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Biashara za Watu Weusi ni muhimu

Kusaidia biashara za Watu Weusi kote ulimwenguni.

Uber imeshirikiana na mpishi bingwa mshindi wa tuzo, mmiliki wa mkahawa, mwandishi na mwanaharakati wa chakula Marcus Samuelsson ili kuisaidia mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi kupitia Mfuko wa Kuoanisha wa Biashara ya Watu Weusi ni Muhimu. Mfuko huu unaipatia ruzuku na usaidizi mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi ambayo imeathiriwa vibaya na janga la ugonjwa na ambayo kihistoria ina mitaji midogo.

Tunafurahi pia kusherehekea historia thabiti na ubunifu unaohusika kwenye chakula cha Watu Weusi na mfululizo mpya wa vipindi vya kidijitali kwa kushirikiana na Samuelsson na wapishi bingwa 4 na wamiliki wa mikahawa: Nina Compton, Kwame Onwuachi, Rodney Scott na Leticia Skai Young. Tunatumaini filamu hiyo si tu inahamasisha ulaji wa uzingativu bali pia inaruhusu watu kusikia baadhi ya hadithi nyingi ambazo bado hazijasimuliwa na wamiliki Weusi wa mikahawa.

Kwingineko kwenye programu ya Uber Eats, mipango kama vile Wiki ya Mikahawa ya Watu Weusi nchini Marekani imezisaidia biashara zinazomilikiwa na Watu Weusi zifikie kilele kwenye taarifa za Uber Eats, ikiwaruhusu wakazi kugundua mikahawa mipya ya mitaani. Nchini Uingereza, tumekamilisha utafiti tuliofanya na Be Inclusive Hospitality kwenye maisha halisi ya wamiliki wa mikahawa ya Watu Weusi na jamii za walio wachache ili kutambua jinsi tunavyoweza kuzisaidia jumuiya hizi.

Nchini Kanada, Uber imeshirikiana na Chama cha Wafanyabiashara Weusi wa Kanada ili kuzindua The Black Pages—orodha ya anwani ya kwanza ya kitaifa ya kidijitali kwa ajili ya biashara ndogo zinazomilikiwa na Watu Weusi kutoka pwani hadi pwani. Kujiunga na The Black Pages na kuitazama kunafanywa bila malipo, hii ikihakikisha kwamba Wakanada wana chanzo kimoja mtandaoni cha kusaidia kugundua na kuunga mkono mikahawa mipya inayomilikiwa na Watu Weusi, maduka ya rejareja, wachuuzi na wajasiriamali.

Mipango hii yote ni mwanzo tu wa ahadi ya muda mrefu ya kuangazia mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi nchini Marekani na ulimwenguni kote. Tutaenda kwenye miji mipya ili kuzipa usaidizi biashara hizi, tuzisaidie kupata ahueni kutokana na athari za janga la ugonjwa, tukijitahidi kuleta usawa wa rangi na kusaidia kuunda jumuiya zinazojumuisha zaidi.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu kazi yetu inayounga mkono biashara za Watu Weusi hapa.

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Mikahawa ya muda huko Washington, DC

Kuiwezesha mikahawa inayomilikiwa na Watu Weusi kupanua biashara zake katika kitongoji kipya.

Kuwashukuru madereva wote na watu wanaosafirisha bidhaa

Maelfu ya madereva na watu wanaosafirisha bidhaa waliendelea kusafirisha bidhaa muhimu wakati wa janga la ugonjwa.