Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kuupa usalama kipaumbele unapoendesha gari ukitumia mfumo wa Uber

From picking up the right rider to knowing when to call for assistance, here are ways to help make every trip stress-free.

Looking for rider information? Switch to the rider safety page.

Vidokezo vya usalama kwa madereva

Tunabuni teknolojia yetu tukizingatia usalama wako. Lakini hatua unazoweza kuchukua zinaweza pia kusaidia kujilinda. Tulishauriana na vyombo vya usalama katika kuandaa vidokezo hivi vya kukusaidia kuwa salama unapoendesha gari ukitumia mfumo wa Uber.

1. Kuthibitisha msafiri wako

Wasafiri huelekezwa kukutana na wewe kwa kuthibitisha namba pleti, aina na muundo wa gari lako. Pia huhakikisha kwamba picha yako inafanana na iliyo kwenye App zao. Pia, unaweza kuwauliza wasafiri wakuthibitishie jina lako kabla ya kuabiri gari lako.

2. Kuwa makini unapoendesha gari

Unaweza kusaidia kudumisha usalama barabarani kwa kuwa makini, kuangalia barabara wakati wote na kupumzika ukiwa umechoka ili kuzuia kuendesha gari ukiwa unasisinzia. Kumbuka: kuandika SMS unapoendesha gari ni kinyume cha sheria katika majimbo na nchi nyingi. Madereva wengine hutumia kifaa cha kushikilia simu ili kuweka simu yao mahali ambapo wanaweza kuiona kwa urahisi, ili kupunguza usumbufu hatari. Katika baadhi ya miji, sheria zinahitaji kuwa na kifaa hicho.

3. Kulinda taarifa zako binafsi

Tunatumia teknolojia inayoficha namba yako ya simu unapompigia simu au kumwandikia ujumbe msafiri kwa kutumia App, kwa hivyo hataona namba yako ya simu.*

4. Kusambaza ujumbe wa kufunga mikanda ya viti

Katika maeneo mengi, madereva na wasafiri wanahitajika kujifunga mikanda kisheria. Pia ni njia bora zaidi ya kuokoa maisha na kupunguza majeraha yanayotokana na ajali za barabarani.

5. Kuwa mwangalifu kwa wanaotembea kwa miguu na wanaoendesha baiskeli

Sheria za barabara zinasema kuwa unapaswa kuwa makini kuhusu watu wanaotembea kwa miguu na wanaoendesha baiskeli. Kufanya hivyo ni muhimu hasa unapoegesha kando ili umshukishe au umchukue msafiri na unapoendesha gari usiku.

6. Kuwashusha wasafiri panaporuhusiwa

Kujua sheria za mahali ulipo kuhusu unakoweza kushukisha wasafiri kunaweza kukusaidia unapofika kwenye maeneo ya kupakia, magari yaliyoegeshwa na mengineyo.

7. Kufuata hisia zako

Amini hisia na uzoefu wako na ufanye uamuzi bora zaidi unapoendesha gari kwa kutumia mfumo wa Uber. Endapo utahisi kwamba upo katika hali ya dharura, unaweza kupata usaidizi wa haraka kwa kutumia kitufe cha dharura kwenye App yako. Kumbuka, unaweza kutamatisha safari wakati wowote ukihisi kwamba huna usalama.

8. Kuwa mwenye fadhili na heshima

Tumebuni Mwongozo wa Jumuiya ya Uber ili kufanya kila huduma iwe salama, iheshimike na ya manufaa. Ni wajibu wetu sote kufuata viwango hivi ili tusaidiane kujenga jumuiya salama na inayomjali kila mtu.

9. Kutupa maoni

Baada ya kila safari, una fursa ya kumtathmini msafiri wako kuanzia nyota 1 hadi 5 na utoe maoni yako kupitia sehemu ya Usaidizi kwenye App yako. Timu yetu ya kutoa usaidizi wakati wowote itakagua tukio husika.

Na ukumbuke, katika kila safari unaweza kubonyeza aikoni ya ngao kwenye App ili uweze kufikia Zana za Usalama wa Uber na kupata usaidizi kila unapohitaji.

Kuhakikisha safari salama kwa ajili ya kila mtu

Pata maelezo zaidi kuhusu usalama kwenye mfumo wa Uber

Uber imejitolea kulinda usalama wa madereva. Pata maelezo kuhusu jinsi usalama unadumishwa kupitia vipengele vya ndani ya App ya Uber Driver na huduma kwa madereva, ikijumuisha bima na usaidizi wa ndani ya App.

Uber imejitolea kuhakikisha usalama wa kila mtu. Pata maelezo zaidi, ikiwa ni pamoja na jinsi tunavyotumia vipengele kwenye App ya wasafiri na madereva na mengineyo.

Mamilioni ya watu huomba safari kila siku. Kila msafiri anaweza kufikia vipengele vya usalama vilivyo kwenye programu. Na kila safari ina timu ya usaidizi kwa wateja inayopatikana wakati wowote.

*Kipengele hiki kikikosa kufanya kazi, huenda namba za simu zikaonekana.