Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Mwongozo wa haraka wa kuanza kutumia programu ya Uber

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufanya mambo ya kawaida kwa haraka

Ijue programu ya Uber

Umesahau nenosiri lako? Unahitaji stakabadhi? Unahitaji usaidizi? Unaweza kutumia menyu kwenye sehemu ya juu kushoto mwa programu kutekeleza haya yote na zaidi.

Kudhibiti akaunti yako

Ikiwa umesahau nenosiri lako au umeshindwa kuingia kwenye akaunti yako, unaweza kupata usaidizi katika sehemu ya ‘Akaunti na Malipo’.

Tuko tayari kukusaidia wakati wowote

Sehemu ya usaidizi kwenye programu ina mbinu, mikakati na majibu yatakayokusaidia kutatua matatizo unayoweza kukumbana nayo kila siku.

Ukaguzi wa safari za awali

Tuko hapa kukusaidia ikiwa utakumbwa na tatizo safarini. Bonyeza 'Safari Zako' ili uombe kurejeshewa pesa, kulalamika unapotozwa ada ya ziada au kuripoti kuhusu matatizo mengine. Unaweza pia kukagua barabara yako, kuangalia bei, kupata stakabadhi na zaidi.

Njia za malipo

Ni rahisi kukagua, kuongeza na kuondoa njia za malipo kwenye sehemu ya ‘Malipo’. Unaweza pia kutumia vocha, kuponi za ofa na zaidi.

Zana zote za usalama katika sehemu pamoja

Fungua Kituo cha Usalama ndani ya programu ili upate maelezo kuhusu mambo tunayofanya kukulinda. Bonyeza aikoni ya ngao unapokwenda safari yako ijayo.

Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kulingana na nchi, eneo na jiji.