Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Tushirikiane kuimarisha usalama wa kila mtu

Kila mtu ana wajibu wa kutekeleza ili kuhakikisha mazingira salama. Ndiyo maana tuna viwango vya kuzingatia katika kutumia akaunti pamoja, umri wa mmiliki wa akaunti na mengineyo.

Kutumia akaunti pamoja

Hairuhusiwi kutumia akaunti pamoja na mtu mwingine, isipokuwa kama imekubaliwa moja kwa moja kwenye mwongozo, vigezo na masharti na sera zetu nyingine. Ili kutumia App ya Uber, unafaa kusajili na kuwa na akaunti yako mwenyewe inayofanya kazi. Hufai kuwaruhusu watu wengine kutumia akaunti yako na usiwahi kumpa mtu mwingine yeyote maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako.

  • Linda akaunti yako. Usimruhusu mtu mwingine aingie kwenye akaunti yako. Hatua ya kuitisha usafiri au usafirishaji wa chakula kwa niaba ya mtu mwingine ambaye amefikisha umri unaotakikana inaruhusiwa na hali hii haikiuki Mwongozo wa Jumuiya ya Uber.

  • Linda akaunti yako. Usiwahi kumruhusu mtu mwingine akubali maombi ya huduma kupitia App za Uber akitumia akaunti yako, isipokuwa iwe imekubaliwa moja kwa moja kwenye mwongozo wetu, vigezo na masharti au sera nyinginezo.

  • Linda akaunti yako. Usiwahi kumruhusu mtu mwingine akodishe skuta, baiskeli au baiskeli yenye injini akitumia akaunti yako, isipokuwa kama imekubaliwa moja kwa moja kwenye mwongozo, vigezo na masharti na sera zetu nyingine.

Watu walio chini ya umri wa miaka 18

Lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili uwe na akaunti ya msafiri, mtumiaji wa Uber Eats au JUMP. Watu walio na akaunti hawaruhusiwi kuitisha usafiri au kusafirisha chakula kwa ajili ya walio na umri wa chini ya miaka 18 bila kuambatana na mtu mzima wakati wa safari au wakati wa kupokea chakula. Watu walio na akaunti pia hawaruhusiwi kukodisha baiskeli au skuta kwa ajili ya mtu aliye na umri wa chini ya miaka 18. Kipengele hiki kitazingatiwa isipokuwa kama kuna maelekezo tofauti kwenye mwongozo yetu, sheria masharti au sera nyinginezo.

  • Ukigundua wakati wa kuchukua au kusafirisha kuwa msafiri wako au mtumiaji wa Uber Eats anaonekana kuwa na umri wa chini ya miaka 18, unaweza kukataa safari au usafirishaji na uripoti kwa Uber. Kumbuka kuwa ukikataa au kughairi safari kwa sababu hii, tathmini ya dereva au tarishi haitaathiriwa. Ni vyema pia kumjulisha msafiri au mtumiaji wa Uber Eats ni kwa nini huwezi kukubali safari au kusafirisha bidhaa, ili asishangae kuhusu kilichotokea.

  • Watu wazima hawaruhusiwi kuitisha usafiri kwa ajili ya mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 ambaye hataambatana na mtu mzima wakati wa safari.

  • Watu wazima hawaruhusiwi kuomba kusafirishwa kwa chakula kwa ajili ya mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 ambaye hataambatana na mtu mzima wakati wa kupokea chakula.

  • Watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kukodisha baiskeli, baiskeli yenye injini au skuta kwa kutumia App ya Uber isipokuwa kama kuna maelekezo tofauti kwenye mwongozo wetu, vigezo na masharti au sera nyinginezo.

Wasafiri wa ziada

Unapoendesha gari kwa kutumia App ya Uber, hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kwenye gari isipokuwa aliyeitisha usafiri pamoja na wageni wake. Unapotumia gari kusafirisha chakula kilichoagizwa kwa kutumia App ya Uber Eats, huruhusiwi kuwa na wasafiri wowote kwenye gari wakati ambao unasafirisha oda. Mmiliki wa akaunti atawajibikia matendo ya wasafiri wenzake wakati wote wa kusafiri kwenye Uber. Ukiitisha usafiri au kusafirishiwa chakula au kukodisha baiskeli, baiskeli yenye injini au skuta kwa niaba ya mtu mzima, utawajibikia matendo yake wakati wa safari au usafirishaji wa chakula.

Maelezo ya gari

Ili kurahisisha kuchukuliwa au kusafirisha chakula, App za Uber huwapa wasafiri na watumiaji wa Uber Eats taarifa za kuwatambulisha madereva na matarishi pamoja na magari yao, ikiwemo namba pleti, aina na muundo wa gari, picha ya wasifu na jina lake.

  • Thibitisha usafiri kwa kutumia taarifa zilizo kwenye App yako kila wakati. Usiingie kwenye gari lililo na dereva ambaye halingani na taarifa za utambulisho ulizo nazo.

Mikanda ya usalama

Mikanda ya usalama inaweza kuwa njia bora zaidi ya kuokoa maisha na kupunguza majeraha yanayotokana na ajali za barabarani. Kila dereva, msafiri, hata walio kwenye viti vya nyuma au matarishi wanaotumia gari ni sharti wafunge mikanda ya usalama kila wakati. Ni sharti msafiri aitishe gari linalotosha watu wote anaosafiri nao, madereva wanafaa kukataa safari ikiwa hakuna mikanda ya usalama ya kutosha kwa ajili ya kila msafiri katika gari lake.

Helmeti kwa ajili ya baiskeli, baiskeli yenye injini na skuta

Kwa usalama wako, unaposafiri kwa baiskeli, baiskeli yenye injini au skuta, hakikisha una helmeti inayokutosha vizuri. Helmeti inaweza kukulinda ukiivaa vizuri kulingana na maelekezo ya mtengenezaji, kwa mfano ifunike kipaji chako cha uso na uifungie chini ya kidevu chako. Ni sharti uvae helmeti popote inapotakiwa kwa mujibu wa sheria husika.

Utumiaji wa kamera au vifaa vingine vya kurekodi video au sauti

Mtu yeyote anayetumia App ya Uber ana uhuru wa kurekodi sehemu ya safari au safari yote au hatua ya kusafirishiwa chakula kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kwa madhumuni ya kurekodi tatizo analotaka kuripoti kwa Uber au mamlaka husika. Sheria au kanuni husika zinaweza kumtaka mtu anayerekodi kwa kutumia kifaa amfahamishe na/au apate idhini ya anayerekodiwa. Tafadhali angalia sheria na kanuni za mahali ulipo ili uthibitishe kama masharti haya yapo.

Kusambaza picha, sauti au rekodi ya video ya mtu hakuruhusiwi.

Tahadhari

Hatua ya kuwa barabarani ina maana kwamba una jukumu la kuhakikisha usalama wako na watu wengine. Ni vyema kuwa makini barabarani, kupumzika vizuri na kuangalia hali zozote zinazoweza kuhitaji uchukue hatua za haraka. Huwa tunakagua ripoti kuhusu mienendo isiyo salama ya kuendesha gari.

Usimamizi na utunzaji mzuri

Madereva na matarishi wanatarajiwa kuyatunza magari yao vizuri ikiwemo breki, mikanda ya usalama na magurudumu. Hii ina maana kwamba unatakiwa kulitunza gari lako kuambatana na viwango vya usalama na matengenezo yanayoruhusiwa mbali na kutii sheria na kanuni husika za mahali ulipo.

Kutumia barabara pamoja

Hali ya kudumisha usalama barabarani inataka ufanye matendo salama, yanayojumuisha kuwajali wasafiri wote, bila kubagua njia wanazotumia kusafiri.

  • Kabla ya kushuka kwenye gari, hakikisha umeangalia nyuma ili uone kama kuna mwendesha baiskeli, gari, wanaotembea kwa miguu au skuta.

  • Wazingatie watu wengine wanaosafiri kwa pikipiki, baiskeli zenye injini au skuta au wanaokwenda kwa miguu. Pia kuwa makini na hali za barabara mbele yako.

Dharura za umma

Uber inaweza kuchukua hatua zaidi kujaribu kulinda usalama wa mfumo wetu wakati wa dharura, ikiwa ni pamoja na majanga ya asili, dharura za afya ya umma na hali ya matatizo ya umma.

Kwa mfano, ikiwa Uber itapokea ilani kutoka kwa mamlaka ya afya ya umma kwamba mtu anayetumia mfumo wa Uber anaweza kuathiri umma, tunaweza kuorodhesha akaunti ya mtu huyo hadi iwe salama kumruhusu mtu huyo kuanza kutumia mfumo wa Uber. Vivyo hivyo, tunaweza kuwazuia watu katika jiji au mkoa mzima kutumia sehemu au mfumo wote wa Uber ili kutii mwongozo wa mamlaka wakati wa dharura ya afya ya umma, janga la asili au hali nyingine ya shida ya umma, au wakati hali inaendelea upatikanaji wa jukwaa la Uber kunaweza kuwa hatari dhahiri na ya sasa.

Mwongozo wa ziada kwa Uber Eats

Pamoja na kufuata Mwongozo wa Jumuiya ya Uber, angalia vigezo vyetu vya oda na usafirishaji wa Uber Eats.

Angalia Miongozo zaidi ya Jumuiya

Heshimu watu wote

Fuata sheria

*Nyenzo hii inasimamiwa na mshirika mwingine na Uber haiwajibikii maudhui yake.