Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Njia salama ya kusafirisha oda za Uber Eats

Mwongozo huu inarahisisha utaratibu wa kuandaa na kusafirisha chakula. Muongozo huu pia unasaidia kuimarisha uaminifu miongoni mwa madereva, wateja wa Uber Eats na wauzaji walio karibu nawe.

Jinsi ya kuandaa na kusafirisha oda vizuri

Wauzaji wanapaswa kutimiza masharti yote ya usajili, leseni na sheria nyingine zinazohusu vyakula, zikiwemo za usafi na usalama wa chakula, kanuni bora za sekta na sera za Uber. Ni lazima wauzaji wwe wamesajiliwa, wawe na leseni na/au vibali sahihi.

  • Vyakula vingi vinavyopikwa huharibika haraka na vinaweza kusababisha magonjwa kama havitatunzwa vizuri. Vyakula kama hivi vinaweza kudhuru afya visipowekwa kwa muda na hali joto inayostahili kabla ya kuchukuliwa. Ni muhimu kudumisha usafi wakati wote wa kuandaa oda.

    Ili kusaidia kuhakikisha kuwa chakula kinawafikia watumiaji wa Uber Eats kikiwa salama, tunakuhimiza ufungashe vizuri kabla ya kusafirisha.

    Unatarajiwa kuzingatia maelezo unayopewa na wateja wa Uber Eats yanayohusu mizio ya chakula, vyakula visivyokubaliwa au masharti mengine ya lishe na ukatae maombi ya oda ambayo hayatii. Unapaswa kutoa maelezo ya mizio na uweke lebo iliyoandikwa kwa oda zilizo na vyakula maalum vya mzio.

Usafirishaji mzuri wa oda

Wauzaji wanaweza kuwasiliana na madereva kuhusu mwongozo wa usafirishaji unaoboresha usalama wa chakula, kuzingatia mwongozo wa sheria, au kukidhi masharti ya lishe ya mtumiaji wa Uber Eats. Kwa mfano, wauzaji wanaweza kumwarifu dereca atenganishe vyakula Halal na visivyo Halal. Matarishi wanapaswa kufuata mwongozo kama huo kutoka kwa wauzaji kila wakati.

  • Lazima madereva watumie mfuko maalum ili kutoa huduma salama na safi. Matarishi hawalazimiki kutumia bidhaa za Uber Eats zilizowekewa chapa. Usafirishaji kwa kutumia baiskeli ni bora zaidi ukitumia mkoba maalum ili kulinda chakula dhidi ya kunesanesa na hali ya anga.

    Hupaswi kuharibu au kufungua kifungasha wakati wa usafirishaji. Kufanya hivi kunaweza kuathiri chakula, jambo ambalo huenda likaathiri pakubwa usalama wa chakula kwa watumiaji wa Uber Eats. Tafadhali dumisha usafi wa kibinafsi ili kuhakikisha usalama wa chakula.

Weka sehemu salama ya kuchukua vyakula

Wauzaji wanapaswa kubainisha eneo salama la kuchukua chakula ili matarishi wasisumbuke.

Usafirishaji wa pombe

Katika nchi ambapo usafirishaji wa pombe unaruhusiwa kwa mujibu wa sheria husika, ni lazima oda zote zilizo na pombe zizingatie vigezo na masharti yanayotumika ya usafirishaji wa pombe na saa za kazi. Watumiaji wa Uber Eats walio na umri unaoruhusiwa kununua pombe na ambao hawajalewa ndio tu wanaoweza kuagiza na kupokea oda za pombe inapohitajika. Matarishi wana jukumu la kufuata masharti ya usafirishaji wa pombe katika eneo husika, ambayo mara nyingi huhusisha kuwataka watumiaji wa Uber Eats kuonesha kitambulisho na kutompatia mtumiaji wa Uber Eats pombe ikiwa hajatimiza umri unaotakiwa kisheria au ikiwa anaonekana kuwa amelewa.

Angalia Miongozo zaidi ya Jumuiya

Heshimu watu wote

Tushirikiane kuimarisha usalama wa kila mtu

Fuata sheria