Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Linda usalama wako unaposafiri kupitia mfumo wa Uber

Vidokezo hivi vilivyotengenezwa kwa ushirikiano na jeshi la polisi vinafanikisha kila safari kuwa salama, kuanzia hatua ya kuhakikisha kuwa unaabiri gari sahihi hadi kujua unakoenda na wakati wa kuomba usaidizi.

Vidokezo vya kuimarisha usalama wa Uber

Tunawakagua madereva na kuboresha teknolojia yetu ili kuimarisha usalama wako. Lakini kuna pia hatua unazoweza kuchukua ili kuimarisha usalama. Vidokezo hivi vilibuniwa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuimarisha usalama wako unaposafiri kupitia Uber.

1. Itisha usafiri kwenye App

Punguza muda unaotumia simu nje ukimsubiri dereva. Badala yake, subiri ndani hadi App ioneshe kuwa dereva wako amewasili.

2. Kagua Gari Lako

Kila unaposafiri kwa Uber, tafadhali hakikisha unaabiri gari na dereva anayefaa kwa kulinganisha maelezo ya namba pleti, aina na muundo wa gari na picha ya dereva na maelezo yaliyo kwenye App yako. Unaweza tu kuitisha usafiri wa Uber kwenye App, kwa hivyo usiwahi kuabiri gari au kubebwa na dereva ambaye halingani na maelezo yaliyo kwenye App.

3. Muulize dereva athibitishe jina lako

Kando na hatua za Kukagua Usalama wa Safari, unaweza pia kumuuliza dereva kuthibitisha jina lako kabla ya kuabiri gari. Dereva anaona jina lako la kwanza kwenye App nawe unaona jina lake kwenye App yako. Ili kuambiana majina kwa njia salama, unaweza kuuliza, “Umekuja hapa kumchukua nani?” Huenda dereva pia akakuuliza kuthibitisha jina lake kwa ajili ya usalama wake.

4. Kalia kiti cha nyuma

Ikiwezekana, kalia kiti kiti cha nyuma, haswa unaposafiri peke yako. Hii inakuwezesha kushuka kwa usalama kwenye upande wowote wa gari ili kuepuka msongamano wa magari na inakupa wewe pamoja na dereva wako fursa ya kutulia vizuri.

5. Funga mikanda ya usalama kila wakati

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, hatua ya kufunga mikanda ya usalama ni njia bora zaidi ya kuokoa maisha na kupunguza majeraha yanayotokana na ajali za barabarani.

6. Waoneshe ndugu na marafiki maelezo ya safari

Ukiwa safarini, bonyeza ‘Onesha hali ya safari’ kwenye App ili umwoneshe ndugu au rafiki jina, picha, namba pleti na eneo la dereva wako. Atapokea SMS au arIfa ya programu inayofuatilia gari lako na Muda Utakaowasili.

7. Linda taarifa binafsi

Katika maeneo maalum, tunawekeza katika teknolojia ili kuweza kufumba namba yako ya simu unapompigia au kumtumia dereva wako ujumbe kupitia App.*

8. Fuata hisia zako

Amini hisia zako na ufanye uamuzi bora zaidi unapoitisha usafiri kwenye mfumo wa Uber. Ikiwa unahisi unahitaji usaidizi wa dharura, unaweza kupigia huduma ya usaidizi wa dharura kwa kutumia kitufe cha huduma za dharura kwenye App. Kila unapopigia simu huduma za dharura kwenye App ya Uber, App itakupa eneo halisi na maelezo ya safari unayoweza kuonesha mratibu.

Kumbuka, unaweza kutamatisha safari wakati wowote ukihisi kwamba huna usalama.

9. Kuwa na unyenyekevu na heshima

Kulingana na Mwongozo wa Jumuiya ya Uber, tafadhali waheshimu wasafiri wenzako, dereva na gari lake.

10. Toa maoni kuhusu safari yako

Baada ya kila safari, utaombwa uitathmini kwenye App. Maoni yako husaidia kuimarisha usalama na uthabiti wa Uber na kufanya huduma za Uber ziridhishe kila mtu. Ikiwa utakumbana na tatizo la kiusalama safarini, tafadhali ripoti kwa Uber. Timu yetu ya usaidizi itafuatilia wakati wowote.

Na ukumbuke, katika kila safari unaweza kubonyeza aikoni ya ngao kwenye App ili uweze kufikia Zana za Usalama wa Uber na kupata usaidizi kila unapohitaji.

Kuhakikisha safari salama kwa ajili ya kila mtu

Pata maelezo zaidi kuhusu usalama kwenye mfumo wa Uber

Usalama wa msafiri

Mamilioni ya watu huomba safari kila siku. Kila msafiri anaweza kufikia vipengele vya usalama vilivyo kwenye programu. Na kila safari ina timu ya usaidizi kwa wateja inayopatikana wakati wowote.

Ahadi yetu kuhusu usalama

Uber imejitolea kuhakikisha usalama wako. Pata maelezo kuhusu dhamira yetu na jinsi tunavyotumia vipengele kwenye App ya wasafiri na madereva na mengineyo.

*Kipengele hiki hakipatikani katika kila nchi. Kipengele hiki kisipofanya kazi, huenda namba za simu zikaonekana.