Furahia programu ya Dereva kwenye skrini ya gari lako
Unganisha kwenye CarPlay au Android Auto na ufurahie uelekezaji wa hatua kwa hatua na ukubali safari kwenye skrini kubwa ili uweze kuendesha gari kwa urahisi.
Hivi ndivyo unavyoweza kufanya ukitumia skrini ya gari lako
Pata maeneo yenye wasafiri wengi
Pata mwonekano mzuri wa maeneo yenye wasafiri wengi kwa kutumia ramani ya kuonyesha maeneo yenye shughuli nyingi moja kwa moja kwenye skrini ya gari lako na kurahisisha kujua mahali pa kwenda ili kupata maombi ya safari.
Kubali maombi ya safari
Unaweza kuona na kukubali maombi ya kipekee na ya Rada ya Safari. Unapofanya hivyo, utaona maelezo ya safari kama vile nauli utakayolipa*, wakati wa kushushwa na umbali—kwenye skrini ya gari lako.
Vinjari bila wasiwasi
Fuata maelekezo ya hatua kwa hatua na uone majina ya barabara, ishara za kusimama na taa za barabarani kwenye skrini kubwa, ili uweze kufurahia huduma isiyo ya kugusa bila kukosa taarifa kuhusu barabara.
Ongeza uaminifu kwa wasafiri
Abiria wanaweza kuona barabara yao kwenye skrini kubwa huku ukiweka maelezo yako binafsi faragha kwenye simu yako.
“Hufanya kuona na kufuata maelekezo barabarani kuwa rahisi”
Marshall O. anapenda jinsi CarPlay inavyomsaidia “kutazamia zamu na mahali anakoenda” ili aweze kumakinika “barabarani.”
“Abiria wanapenda hivyo”
Daria R. anapenda “kutangamana zaidi na wateja wake” huku pia “akiona maelekezo kwa vizuri.”
“Programu ya Dereva kwenye CarPlay imeboresha hali yangu ya utumiaji”
Constance S. anasema ni “rahisi zaidi kuona maelekezo vizuri zaidi wakati taarifa zote ziko kwenye skrini ya CarPlay.”
Maelekezo rahisi ya kuweka mipangilio
- Unganisha simu yako ya Android au iPhone kwenye skrini ya gari lako bila waya au kwa kebo.
- Android Auto au CarPlay inapaswa kufunguka kiotomatiki baada ya simu yako kuoanishwa. Ikiwa haifanyi hivyo, fuata vidokezo kwenye skrini ili kuanza.
- Fungua programu ya Dereva kwenye simu yako, kisha tafuta na uchague programu ya Dereva kwenye skrini ya gari lako.
- Ramani ya Uber itakapofunguliwa, gusa Nenda Mtandaoni kwenye skrini ya gari lako ili uone maeneo yenye wasafiri wengi na uanze kukubali maombi.
Je, unajaribu kutumia mfumo wa usafiri kutoka kwenye skrini yako ya Tesla?
Furahia urambazaji ulio wazi na rahisi zaidi kwenye skrini kubwa ya Tesla yako na upunguze wasiwasi wa umbali kwa kutumia mfumo wa kulinganisha unaozingatia betri.
*Nauli utakayolipa, wakati wa kushusha abiria, na umbali huonekana kwenye Apple CarPlay na Android Auto katika masoko ambapo madereva na watoa huduma za usafirishaji wana uwezo wa kufikia maelezo haya kwa sasa.