Njia bora ya kusimamia biashara yako
Tovuti mpya ya Mtoa Huduma ya Uber hutoa data ya haraka na ya kuaminika zaidi; vipengele vipya vya kukusaidia kukuza biashara yako na muundo ambao ni rahisi zaidi kutumia na kuelewa.
Mabadiliko shwari
Ikiwa tayari unatumia nyenzo nyingine za usimamizi wa msururu wa magari ya Uber kama vile Uber Fleet, tunataka kuhakikisha kwamba maswali yako yote yanajibiwa unapohamia kwenye Tovuti ya Mtoa Huduma. Kwa taarifa zaidi, tafadhali angalia maelekezo na maswali yanayoulizwa mara kwa mara hapa chini.
Nyenzo hii bado inatengenezwa
Toleo la Tovuti ya Mtoa Huduma unaloona sasa si la mwisho. Bado tunaongeza vipengele. Kwa wakati huu, bado unaweza kutumia nyenzo za zamani na kuhama kati ya zote mbili bila matatizo yoyote.
Huduma zinazorudufishwa
Tunapendekeza kwamba ujaribu Tovuti ya Mtoa Huduma ili ujifahamishe huduma mpya. Kumbuka: kila kitendo unachofanya kwenye tovuti moja (kama vile kuweka gari au hati) kitaonyeshwa kiotomatiki kwenye tovuti nyingine na kinyume chake, kwa hivyo hakuna haja ya kukifanya tena.
Vichupo vipya vya Malipo na Ripoti
Huduma hii mpya hukuruhusu kuelewa vyema mapato yako unapotumia Uber, kupatanisha malipo na madereva na kutazama miamala yote inayofanyika kwenye magari yako.
Ufikiaji rahisi, wakati wowote
Jinsi ya kuingia kwenye Tovuti mpya ya Mtoa Huduma
Kuna njia 2:
- Ikiwa wewe ni mtumiaji wa Uber Fleet (nyenzo yetu ya zamani ya usimamizi wa msururu wa magari), unaweza kubofya bango jekundu lililo juu yake.
- Au nenda moja kwa moja kwenye tovuti ukitumia kiungo hiki:
Kagua mapato na malipo katika Tovuti ya Mtoa Huduma
Sasa unaweza kutumia vichupo vya Malipo au Ripoti
Ukiwa kwenye Tovuti ya Mtoa Huduma, bofya kichupo cha Malipo kwenye upande wa juu wa ukurasa. Hapa ndipo utakapopata taarifa ya mapato na malipo yanayohusiana na akaunti yako.
Ikiwa unataka kupakua taarifa hii, unaweza kubofya kichupo cha Ripoti au kwenye ikoni ya wingu.
Kuelewa salio lako la sasa
Katika upande wa juu kushoto wa ukurasa, utaweza kuona salio lako lililokusanywa kuanzia mwanzoni mwa wiki hadi siku na wakati unapoangalia data. (kumbuka: kunaweza kuwa na ukawiaji wa data wa hadi saa 3).
Inawakilisha jumla ya mapato unayozalisha (ikiwa unaendesha gari na/au kusafirisha bidhaa) na/au watu wanaojipatia mapato kwenye msururu wako wa magari na tayari haijumuishi malipo, marejesho ya fedha, gharama na malipo yanayotumwa kwa wahusika wengine.
Mwishoni mwa wiki, salio la mwisho linapaswa kuwa sawa na lile linalohamishwa kwenye akaunti yako ya benki katika wiki inayofuata.
Kuelewa mchanganuo wa salio lako
Chini ya salio lako la sasa, unaweza kuangalia ni vitu vipi vilivyojumuishwa kwenye kiasi hiki.
Kidokezi: Ili kupata taarifa dhahiri zaidi, tunapendekeza uangalie tarehe kadhaa kuanzia Jumatatu.
Dhana kuu utakazopata:
Salio kwenye akaunti unapoanza kipindi: Mapato ya msururu wako wa magari kutoka wiki iliyotangulia na kwa hivyo, ni kiasi unachoanza nacho katika wiki yako (tayari kimehamishiwa kwenye akaunti yako ya benki kutoka wiki iliyotangulia).
Jumla ya mapato: Ni mapato halisi unayozalisha (ikiwa unaendesha gari na/au kusafirisha bidhaa) na watu wanaojipatia mapato kwenye msururu wako wa magari, ada ya huduma ya Uber ikiwa tayari imeondolewa. Kwa kubofya kishale kilicho upande wa kulia, unaweza kuona mchanganuo wa mapato kwa kila kategoria na kuelewa pale ambapo mapato yanatoka (nauli ya safari, ofa, viinua mgongo au vifuta jasho). Mapunguzo ya kodi yanaweza kutumika hapa.
Marejesho ya fedha na gharama: Tozo za gharama mbalimbali zisizohusiana na safari, pamoja na malipo ya kufidia kodi.
Imelipwa kwa wahusika wengine: Makusanyo ya fedha yaliyokusanywa na madereva na amana zilizowekwa kwenye akaunti yako ya benki kwa ajili ya mapato ya wiki iliyotangulia.
Salio kwenye akaunti mwishoni mwa kipindi: Jumla ya mapato yaliyozalishwa na wewe na madereva, ukiondoa gharama zote zilizotajwa hapo awali. Hii inawakilisha kiasi cha mwisho ambacho msururu wako wa magari ulizalisha katika kipindi hicho na karibu sikuzote kitalingana na kiasi kinachowekwa kwenye akaunti yako katika wiki inayofuata.
Kumbuka: Salio la kwanza na la mwisho huripoti mapato yaliyozalishwa katika wiki iliyochaguliwa pekee, kuanzia Jumatatu saa 10:00 asubuhi na kumalizika Jumatatu inayofuata saa 10:00 asubuhi. Mapato kutokana na safari zilizokamilishwa kati ya saa 10:00 asubuhi na uhamisho wa benki yatajumuishwa katika kiasi Kilichohamishwa kwenda akaunti ya benki. Hii inamaanisha kwamba Salio la Kwanza na kiasi Kilichohamishwa kwenda akaunti ya benki huenda yasilingane kila wakati na tofauti unayoona ni sawa na "Salio la Kwanza" (+/-) mapato ya safari zilizokamilishwa kati ya saa 10:00 asubuhi na wakati wa kutuma malipo.
Kukagua taarifa za dereva
Kwa kubofya kitufe cha Lipa madereva kwenye upande wa juu kushoto wa ukurasa, utaelekezwa kwenye skrini ambapo utapata mchanganuo wa mapato kulingana na mtu anayejipatia mapato.
Zaidi ya hayo, ukibofya jina la yeyote kati ya watu wanaojipatia mapato, utaelekezwa kwenye ukurasa mpya ambapo utapata machaguo ya kuwasiliana na mtu huyo anayejipatia mapato (kupitia ujumbe, simu au barua pepe) na uangalie muhtasari wa mapato yake na kila muamala ambao ulifanywa kwenye akaunti hiyo
Kumbuka: Tovuti ya Mtoa Huduma kwa sasa haishughulikii uhamishaji wa pesa kwa madereva
Kufikia ripoti na data zinazopatikana
Aina za ripoti na taarifa zinazopatikana kwa kipindi kilichochaguliwa ni:
Shughuli ya Safari: Ina maelezo ya safari zilizokamilishwa na msururu wako wa magari, kama vile jina na taarifa ya mawasiliano ya dereva, gari, anwani, aina za huduma (safari au usafirishaji wa bidhaa) na hali ya safari (imekamilika, imeghairiwa, n.k.).
Shughuli ya Dereva: Ina safari zilizokamilika, muda wa mtandaoni na wakati wa safari kwa kila dereva.
Ubora wa Dereva: Ina jumla ya safari zilizokamilika, kiwango cha kukubali, kiwango cha kughairi na ukadiriaji wa nyota wa kila dereva.
Mpangilio wa Malipo: Ina maelezo ya salio la akaunti yako katika kiwango cha msururu wa magari, ikiwemo mapato na makusanyo.
Malipo ya Dereva: Ina maelezo yoyote yanayohusiana na malipo ya kila dereva katika kipindi kilichobainishwa.
Muamala wa Malipo: Ina miamala yoyote inayohusiana na malipo katika kipindi kilichobainishwa.
Maswali yanayoulizwa sana
Kwa nini siwezi kufikia huduma ya zamani ya malipo tena?
Huduma ya malipo ya Tovuti ya Mtoa Huduma inatekelezwa na chanzo cha data cha kasi na sahihi zaidi. Data na ripoti katika nyenzo ya awali ya Uber Fleet inaweza kucheleweshwa kwa hadi saa 3-6. Katika Tovuti mpya ya Mtoa Huduma, data ya mapato karibu kila mara huripotiwa ndani ya saa moja (kumbuka: inaweza kuchukua hadi saa 3).
Je, ninawezaje kutazama mapato yangu ya kila wiki kwenye Tovuti mpya ya Mtoa Huduma?
Data za mapato ya kila wiki (ikiwemo fedha zinazotumwa kwa njia ya benki) zinapatikana katika kichupo cha Malipo pia kwenye ripoti ya Mpangilio wa Malipo katika kichupo cha Ripoti.
Kwa nini mapato katika nyenzo ya zamani yanaonekana tofauti yakilinganishwa na nyenzo mpya hata ingawa salio langu la mwisho ni lile lile?
Katika nyenzo ya zamani ya Uber Fleet, jumla ya mapato yako yalijumuisha ada ya huduma ya Uber, ambayo ilitolewa kwenye sehemu ya Malipo na Makusanyo. Katika jumla ya mapato yako sasa, inakuja ikiwa ada ya huduma ya Uber tayari imeondolewa. Ndiyo maana unaona utofauti katika nambari.
Nitapataje data ya kulipa madereva wangu?
Kubofya Lipa madereva katika kichupo cha Malipo hukuonyesha salio la kiwango cha dereva kwa kipindi fulani. Tumia hii ili kufuatilia mapato ya dereva na kusimamia malipo yako. Unaweza pia kutumia ripoti za Malipo ya Dereva kutoka kwenye kichupo cha Ripoti ili kupata taarifa hiyo hiyo. Bado unahitaji kuwalipa madereva nje ya tovuti (malipo ya moja kwa moja kwa madereva bado hayashughulikiwi).
Je, ni lazima nisajili tena taarifa zangu za benki na kodi (ikiwa zinatumika katika nchi yangu)?
Hapana. Taarifa zako zote za benki na kodi zitahamishwa kiotomatiki hadi kwenye Tovuti mpya ya Mtoa Huduma.
Je, kuna tatizo nikiweka dereva au gari kwenye tovuti moja tu?
Hapana, kila kitu unachotekeleza kwenye tovuti moja huonyeshwa kiotomatiki kwenye tovuti nyingine, kwa hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi au kurudufisha juhudi zozote.
Majina kwenye safuwima mpya ya Ripoti hayalingani na ya zamani; jambo hilo linatarajiwa?
Ndiyo, zinalingana na jinsi Uber inavyopanga taarifa ya malipo katika mifumo yetu na jinsi data ya malipo inavyoonyeshwa kwenye tovuti nyingine kama vile programu ya Dereva au Fleet.
Je, ninaweza kuona wapi ankara kwenye Tovuti mpya ya Mtoa Huduma?
Ankara bado hazipatikani kwenye Tovuti mpya ya Mtoa Huduma (zitapatikana hivi karibuni). Itabidi uendelee kutumia http://partners.uber.com ili kuangalia na kupakua ankara kwa muda.
Je, malipo ya kila wiki yameratibiwa kutumwa saa gani ya siku?
Usiwe na wasiwasi! Hakutakuwa na mabadiliko katika malipo ya kila wiki. Malipo ya kila wiki yameratibiwa kufanyika Jumatatu saa 10:00 asubuhi, saa za eneo husika.
Je, nitaona wapi taarifa inayohusiana na malipo kwenye kiwango cha dereva?
Unaweza kwenda kwenye Malipo na kuweka sehemu ya Lipa madereva wako au ubofye Ripoti kisha uangalie ripoti ya Malipo ya Dereva.
Kuhusu
Kuhusu