Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kutana na Uber Movement

Kutumia data ili kusaidia katika mchakato wa kupanga, kuboresha na kutatua foleni

Kupanga miji bora kunahitaji data nzuri. Uber hukusanya data ya safari katika zaidi ya miji 10,000 kote ulimwenguni. Kwa nini usitoe maoni yako? Jiunge katika Uber Movement, inayowapa wasanifu wa miji uwezo wa kufikia data iliyojumlishwa ya Uber ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu miji yetu.

MCHANGO WETU

Uber Movement hutoa nyenzo mpya kwa wasanifu wa miji

“Uber Movement is an important first step that demonstrates our commitment to the cities we serve, so that they can better plan and manage their streets and infrastructure.”

Shin-pei Tsay, Mkurugenzi wa Sera, Miji na Usafirishaji, Uber

Mkusanyiko wa data mpya ya usafiri

Kufanya data iweze kufikiwa na wasanifu wa miji husaidia kuwapa nyenzo zaidi ili kuboresha miundo ya miji baadaye. Na hilo linaweza kudumisha miji safi, bora na inayopendeza kila mtu.

Kazi za Uber Movement

Mpango wa kusaidia katika matukio yasiyotarajiwa

Data yetu inaweza kusaidia miji kupanga vizuri na kushughulikia masuala ya usafiri na dharura ili wasafiri waweze kusafiri kwa njia rahisi wakati tukio kama vile kufungwa kwa Metro DC linatokea.

Kutoa maarifa kuhusu huduma ya usafiri mijini

Mnamo Oktoba 2016, Uber na Infrastructure Partnerships Australia (IPA) zilifanya kazi kwa pamoja ili kuzindua Kipimo cha Usafiri cha IPA, ambacho hutoa data kuhusu jinsi usafiri hufanyika katika miji mikuu, inayohesabiwa kikamilifu kutoka kwenye data ya Uber Movement.

Kufuatilia ufikiaji wa chakula bora

The Cincinnati Mobility Lab huchunguza ufikiaji wa chakula bora katika eneo. Kwa kupima muda wa usafiri—kiashiria muhimu tunapochunguza ufikiaji wa chakula bora—data yetu inaweza kuchangia kwenye mijadala kuhusu ukosefu wa chakula na chaguo za ufikiaji wa chakula bora.