Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Mwongozo wa mtumiaji wa mnyama wa huduma

Kutumia teknolojia ili kuwezesha ufikiaji wa huduma za usafiri zinazotegemeka na zinazoweza kufikiwa kwa ajili ya wasafiri ambao ni vipofu au wenye uoni hafifu.

Faida za Uber

Teknolojia ya iOS VoiceOver na Android TalkBack

Kupitia iOS VoiceOver, Android TalkBack na mwonekano wa hiari wa Breli, Uber huwezesha kupata gari kwa kugusa kitufe. Ili kuwezesha VoiceOver kwenye iOS: Tumia njia za mkato za kugusa mara tatu au Siri kwa kubofya hadi kwenye chaguo la Mipangilio > Jumla > Ufikiaji > VoiceOver. VoiceOver inaweza kutumiwa kuhusiana na mwonekano wa Breli pasi waya na inapatikana katika majiji na lugha zote ambapo Uber inapatikana.

Malipo ya kielektroniki

Mfumo wa Uber wa malipo ya kielektroniki hurahisisha mchakato wa malipo, ukipunguza wasiwasi ya wasafiri kuhitaji kubeba pesa taslimu au kubadilishana noti na dereva.

Gharama rahisi

Kila safari hurekodiwa kielektroniki na risiti hutumwa kiotomatiki kwa wasafiri kupitia barua pepe, hivyo kufanya iwe rahisi kutayarisha ripoti za matumzi.

Inapatikana katika zaidi ya majiji 10,000

Kote ulimwenguni, mamilioni ya watu wanatumia Uber ili kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hakuna tena haja ya kusimamisha teksi barabarani au kungojea gari nje. Wasafiri wanaweza kuanzisha programu ya Uber wakiwa mahali popote na kusubiri kwa usalama gari lao lifike, hii ikitoa chaguo jingine la usafiri kwa watu ambao hawawezi kuendesha gari.

Ufikiaji sawa kwa wote

Kila ombi la safari unalotoa huoanishwa kiotomatiki na dereva aliye karibu kupitia programu ya Uber, hivyo ikipunguza fursa za ubaguzi, hali ambayo inaathiri huduma salama na nafuu za usafiri. Kwa wasafiri walio na ulemavu wa kuona au wasioona vizuri na huenda wanasafiri na wanyama wa huduma, Mwongozo wa Jumuiya wa Uber na Sera ya Mnyama wa Huduma inawahitaji waziwazi madereva kuzingatia sheria zote zinazohusu usafirishaji wa wanyama wa huduma.

Shiriki Muda Utakaowasili na eneo

Wasafiri ambao ni vipofu au wasioona vizuri wanaweza kushiriki maelezo yao ya usafiri kwa urahisi, ikijumuisha barabara mahususi na makadirio ya muda wa kuwasili na marafiki au familia kwa amani ya ziada ya akili. Wapendwa watapokea kiunganishi ambapo wanaweza kujua kwa wakati halisi jina na picha ya dereva, pamoja na taarifa za gari na wafuatilie mahali ulipo kwenye ramani hadi utakapowasili mahali unakoenda, yote haya bila kupakua programu ya Uber.

Kufuatilia kwa wakati halisi

Uber hutumia GPS ili kuweka kumbukumbu ya kila safari. Hii huwapa wasafiri amani ya akili kwa kujua kwamba barabara bora zinatumiwa na huwapa njia ya kuuliza maswali yoyote na uwezo wa kushiriki maendeleo ya safari pamoja na familia au marafiki.

Mwongozo wa kupata Sera ya Uber ya Mnyama wa Huduma

Kwenye kompyuta

Kituo cha Msaada wa Ufikiaji

Kwenye programu ya Uber

Kituo cha Msaada wa Ufikiaji

  1. Bofya kitufe cha menyu kwenye kona ya juu kushoto.
  2. Chagua Msaada.
  3. Telezesha chini hadi sehemu ya Ufikiaji.
  4. Chagua Kusafiri pamoja na Wanyama wa Huduma, kisha Marekani Sera ya Mnyama wa Huduma.

Kuripoti malalamiko kuhusu kunyimwa huduma ya mnyama wa huduma

Timu yetu mahususi ya usaidizi hushughulikia malalamiko yote yanayohusu wanyama wa huduma ili kuhakikisha kuwa matukio yanachunguzwa, kuandikwa na kutatuliwa ifaavyo. Ripoti hizi zinaweza kuandikishwa kwenye Kituo chetu cha Msaada wa Ufikiaji.

Kuna njia kadhaa za kuripoti malalamiko ya kunyimwa huduma ya mnyama wa huduma:

Kwenye kompyuta kwa ajili ya watumiaji walio na akaunti za Uber

Kituo cha Msaada wa Ufikiaji

  1. Ingia kwenye help.uber.com ukitumia maelezo yako ya kuingia kwenye akaunti ya Uber.
  2. Telezesha chini kisha ubofye Ufikiaji.
  3. Tafuta "sera ya mnyama wa huduma" kisha uchague Sera ya Mnyama wa Huduma ya Marekani.
  4. Telezesha chini hadi sehemu ya Ninataka kuripoti tatizo la mnyama wa huduma.

Safari zilizokamilika

  1. Ingia kwenyehelp.uber.com ukitumia maelezo yako ya kuingia kwenye akaunti ya Uber.
  2. Kwenye ukurasa wa Matatizo ya Safari na Urejeshaji wa Fedha, chagua safari husika ukitumia menyu kunjuzi ya historia ya safari kwenye ramani.
  3. Bofya Zaidi chini ya maelezo ya safari kwa ajili ya safari iliyochaguliwa.
  4. Chagua Ninataka kuripoti tatizo la mnyama wa huduma katika sehemu ya Matatizo ya Jumla.

Kwenye kompyuta kwa ajili ya watumiaji wasio na akaunti za Uber

Tafuta fomu ya malalamiko kuhusu mnyama wa huduma hapa.

Kwenye programu ya Uber

Kituo cha Msaada wa Ufikiaji

  1. Bofya menyu kwenye kona ya juu kushoto.
  2. Chagua Msaada.
  3. Kisha uchague Ufikiaji.
  4. Bofya Ninataka kuripoti tatizo la mnyama wa huduma.

Safari zilizokamilika

  1. Bofya menyu kwenye kona ya juu kushoto.
  2. Chagua Msaada.
  3. Kisha uchague Tazama Matatizo Yote.
  4. Bofya Ninataka kuripoti tatizo ya mnyama wa huduma.

Ada na kurejesha fedha

Tozo ya kughairi

Ikiwa utatozwa ada ya kughairi kwa sababu ya kunyimwa huduma, malipo haya yatarejeshwa na timu yetu ya usaidizi ikiwa utatoa taarifa Uber kuhusu suala hilo. Tafadhali kumbuka kwamba fedha zilizorejeshwa zinaweza kuchukua hadi siku 5 za kazi hadi zikufikie kwenye mbinu yako ya malipo.

Urejeshaji fedha wa Uber wa kiti cha pili

Ikiwa unasafiri na mnyama wa huduma kwenye safari ya UberPool na huenda ukahitaji nafasi ya ziada kwa sababu ya ukubwa wa mnyama wako wa huduma, unapaswa kuchagua viti 2 ili kuhakikisha kuwa wewe, mnyama wako wa huduma na wasafiri wengine wote mnaweza kutosha kwenye safari ya pamoja. Unaweza kuandikia Uber hapa na unaweza kurejeshewa fedha kwa ajili ya gharama ya ziada ya kiti cha pili.

Sera ya Mnyama wa Huduma

Sheria za jimbo na za serikali kuu zinapiga marufuku madereva wanaotumia programu ya Dereva wa Uber kuwanyima huduma au kuwabagua wasafiri walio na wanyama wa huduma. Kama ilivyoelezwa kwenye Mwongozo wa Jumuiya wa Uber na Sera ya Mnyama wa Huduma, madereva wanaohusika katika tabia ya ubaguzi kwa kukiuka jukumu hili la kisheria watazuiwa kutumia programu ya Dereva.

Je, una maswali yoyote?

Tuko hapa kukusaidia

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu akaunti yako ya Uber, vinjari maswali yanayoulizwa mara nyingi au utoe maoni kuhusu safari yako ya hivi karibuni.

Toa huduma nzuri

Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu kusafirisha wasafiri wenye ulemavu, angalia nyenzo hizi kwa ajili ya madereva.

*Haitumiki nchini Ufaransa.