Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Matakwa ya Ankara ya Uber

Kila kitu kinachohitajika ili ankara yako ichakatwe kwa njia nzuri na kwa wakati.

Matakwa ya Ankara

Karibu kwenye matakwa ya ankara za Uber. Tumejitolea kufuata mchakato rahisi kutumia na sahihi wa ankara.

Ili kuhakikisha malipo kwa wakati unaofaa, tafadhali hakikisha unazingatia agizo la ununuzi la Uber na ankara zako zote lazima zikidhi matakwa mahususi ya nchi. Tafadhali chagua nchi ambayo unafanyia biashara kwa kubofya alama ya + ili kukunjua orodha.

Uwasilishaji wa Ankara

  • Tafadhali wasilisha ankara zako kupitia Tovuti ya uSupplier. Tembelea ukurasa wa Wagavi wetu wa Uber kwa taarifa zaidi.

  • Ankara zote zinazowasilishwa Uber lazima ziwe katika lugha ya eneo lako, katika faili la mfumo wa PDF. Ikiwa inatumika katika nchi yako, tafadhali pia ambatisha faili la mfumo wa XML la ankara ya kielektroniki. Ankara zitakazowasilishwa katika mafaili ambayo si PDF zitakataliwa.

  • Tafadhali wasilisha ankara 1 pekee kwa wakati mmoja, faili zilizobanwa zitakataliwa.

  • Ankara ambazo hazizingatii matakwa ya Ankara ya Uber zitakataliwa na zinaweza kusababisha ucheleweshaji wa malipo.

Faharasa

  • Maelezo: Maelezo ya kutosha kutambulisha bidhaa au huduma zinazotolewa. Tafadhali jumuisha tarehe za kipindi cha huduma ikiwa inatumika.
  • Idadi: Idadi ya bidhaa zilizotolewa
  • Bei ya Kila Bidhaa: Bei kwa kila bidhaa, bila kujumuisha VAT/GST (kwa mfano, bei ya kila saa/siku, bei kwa kila bidhaa, ada za kupangisha au kukodisha kwa kila kipindi)
  • Jina la taasiri ya Uber inayotozwa: Majina kamili ya biashara lazima yaandikwe kwa usahihi na yajumuishe vifupisho vya aina yoyote vya shirika katika jina la kampuni (yaani, Inc., Ltd., LLC). Majina kamili ya taasisi yanawekwa kwenye Agizo lako la Ununuzi.
  • Anwani ya kutuma bili ya taasisi ya Uber: Anwani ya taasisi ya Uber lazima ionekane sawasawa kama ilivyo kwenye Agizo lako la Ununuzi.

Usaidizi kwa wateja

Tafadhali wasiliana na mfanyakazi wa Uber ambaye unafanya kazi naye ili aunde agizo la ununuzi. Wahimize washirika wako wa biashara waunde agizo la ununuzi. Ikiwa wanahitaji usaidizi wowote, waambie wawasiliane na timu ya uendeshaji wa mnunuzi. Tafadhali angalia sehemu ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kama swali lako halijajibiwa hapa.