Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Jumuiya salama zaidi

Kwa kushirikiana na mashirika maarufu, tunajitahidi kusaidia kurahisisha uendeshaji wa magari kwa usalama na kuzuia ajali barabarani.

Kusimamisha usafirishaji haramu wa binadamu

Linapokuja suala la matatizo ya kimataifa kama vile usafirishaji haramu wa binadamu, tumejitolea kutekeleza jukumu letu.

Kama kampuni inayojikita katika usafiri, tungependa kutekeleza jukumu letu ili kukomesha biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Ushirikiano wa kulinda watoto

Uber inajivunia kushirikiana na ECPAT, shirika maarufu la sera ambalo linalenga kuangamiza unyanyasaji wa watoto unaofanywa kupitia biashara ya ngono. Harakati zinazofanywa na shirika hili ili kutekeleza lengo hili ni uhamasishaji, utetezi, kutunga sera na sheria.

Madereva wanaotoa huduma bora

Kila mtu anayejisajili kuendesha gari huhamasishwa kuhusu viashiria vya biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa nyumbani

Tunatumia wigo na umaarufu wa Uber ili kusaidia katika kuhamasisha, kuelimisha na kuzuia unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa kinyumbani wanaofanyiwa mamilioni ya watu duniani.

Tunatazamia maisha mema ya baadaye

Juhudi zimeanzishwa, kama vile ziara kimataifa za kusikiliza, msururu wa wazungumzaji wa ndani na kujitolea kwa wafanyakazi.