Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kutuhusu

Kutembea kwingi ni kuona mengi, bila shaka utapata mambo mazuri iwe unasafiri mtaani au kufanikisha ndoto zako maishani. Fursa zinajitokeza, kuwa tayari ili uanze kujitengenezea pesa. Kilichoanza kama njia ya kubonyeza kitufe ili kuita usafiri sasa kimerahisisha harakati za mabilioni ya watu kukutana katika sehemu zote ulimwenguni kwa njia mbalimbali kupitia teknolojia yetu.

Barua kutoka kwa Afisa Mkuu Mtendaji

Soma kuhusu ahadi ya timu yetu ya kumpa kila mtu kwenye mfumo wetu kote duniani teknolojia inayoweza kumsaidia afanikiwe.

Uber imejitolea kuwa mfumo wenye magari yanayotumia umeme na yasiyochafua mazingira kufikia 2040, na 100% ya safari zitafanyika katika magari ya umeme, kwenye usafiri wa umma au kwa kutumia magari madogo. Ni jukumu letu kama mfumo mkubwa zaidi wa usafiri duniani kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. Tutafanya hivyo kwa kuwapa wasafiri njia zaidi za kusafiri bila kuchafua mazingira, kuwasaidia madereva kutumia magari ya umeme na kushirikiana na NGO na sekta binafsi ili kusaidia kuharakisha mabadiliko katika matumizi ya nishati bila kuchafua mazingira.

Mbali na kukusaidia usafiri kutoka eneo moja hadi jingine, tunajitahidi kupiga hatua zaidi kupitia teknolojia ya magari ya kujiendesha na usafiri wa ndege mijini; kuwasaidia watu waagize chakula haraka na kwa bei nafuu, kuondoa vizuizi vya kufikia huduma za afya; kuunda vipengele vipya vya kuweka nafasi ya shehena; na kusaidia kampuni zitoe huduma rahisi za usafiri kwa wafanyakazi.

Tunathamini sana usalama wa wasafiri na madereva. Tumejitolea kutimiza wajibu wetu na tunaipa teknolojia kipaumbele. Tunashirikiana na watetezi wa usalama na tunabuni teknolojia na mifumo mipya ili kuboresha usalama na kusaidia kurahisisha safari za kila mtu.

Wanaoendeleza Uber

Tunabuni utaratibu ndani ya Uber unaosisitiza kufanya jambo linalofaa kwa wakati unaofaa kwa manufaa ya wasafiri, madereva na wafanyakazi. Pata maelezo zaidi kuhusu timu inayotuongoza.

Kufahamu uanuwai

Tungependa kudumisha mazingira ya kazi ambayo ni jumuishi na yanayoonesha uanuwai wa miji tunakotoa huduma zetu—ambapo kila mtu anaweza kufurahia jinsi alivyo na ambako uhalisia wa kila mtu unathaminiwa na kuchukuliwa kuwa uthabiti. Kwa kudumisha mazingira ambapo watu kutoka matabaka yote wanaweza kufaulu, tutaifanya Uber iwe kampuni bora zaidi—kwa wafanyakazi na wateja wetu.

Kutenda kwa uadilifu

Hati ya Mpango wa Maadili na Uzingatiaji ya Uber inaelezea ahadi yetu ya kudumisha uadilifu wa viwango vya juu kabisa ndani ya kampuni. Uwazi ni muhimu katika utamaduni wa kimaadili; tunafanikisha hili kupitia Nambari yetu ya Simu ya Msaada ya Uadilifu na miradi kadhaa ya uzingatiaji inayokua na yenye ufanisi.

Habari

Pata matangazo kuhusu ushirikiano, taarifa za App, mipango na habari zaidi za kitaifa na kimataifa.

Blogu

Pata maeneo mapya ya kugundua na kujifunza kuhusu bidhaa za Uber, ushirika na mengine mengi.

Mahusiano ya wawekezaji

Pakua ripoti za kifedha, angalia mipango ya robo ijayo ya mwaka na usome kuhusu mipango ya ushirika katika jamii.

Una haja. Tuna kazi.