Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Go―Get Zero

Tukio letu la kimataifa la tabianchi

Ni lengo letu kuwa mfumo usiotoa hewa chafu na unaopunguza uchafu unaotokana na upakiaji kufikia 2040.* Ndiyo maana katika Go-Get Zero, hafla yetu ya kila mwaka ya hali ya hewa, tulitangaza vipengele na masasisho mapya ili kuhimiza utumiaji wa magari ya kielekitroniki na kufanya iwe rahisi kwa madereva, wasafirishaji, wateja na wafanyabiashara kufanya chaguo zinazoweza kuwawezesha kutunza hali ya hewa. Ingawa bado tunahitaji juhudi zaidi, hatua hizo zinashika kasi. Angalia matangazo yetu yote na utazame hafla hiyo.

Tunahimiza madereva na wasafirishaji zaidi watumie magari ya kielekitroniki

Msaidizi wa Akiliunde

Kipengele hiki kipya cha Akiliunde, kinachokuja kwenye programu ya Dereva hivi karibuni, kitasaidia madereva na wasafirishaji kupata majibu ya haraka na ya binafsi kwa kila swali kuhusu Magari ya Kielektroniki.

EV Mentors

Tutawaunganisha wateja walio na hamu ya kujua mengi kuhusu magari ya kielekitroniki na madereva na wasafirishaji walio na uzoefu wa magari hayo, ili wajibu maswali ya wateja moja kwa moja na washiriki hali zao za utumiaji.


Kusaidia kufanya utunzaji wa mazingira kuwa rahisi


Onyesha uokoaji wa uchafuzi

Endelea kufuatilia kiwango cha hewa chafu unachopunguza unapochagua chaguo za safari za Uber zinazotunza mazingira. Dashibodi sasa inajumuisha safari zako za baiskeli ya kielekitroniki ya Lime na skuta ya kielekitroniki pamoja na safari za UberX Share. Tunakuletea baiskeli za Tembici hivi karibuni.

Mapendeleo ya Magari ya Kielektroniki

Kipengele hiki kipya kitawaruhusu wasafiri kuweka mapendeleo katika mipangilio ya programu yao ya Uber ili waunganishwe na Magari ya Kielekitroniki wakati wowote magari hayo yako karibu.

Bidhaa za Utunzaji wa Hali ya Hewa

Kagua na ununue kutoka kwa chapa zinazotunza hali ya hewa, unapohitaji. Mkusanyiko wa bidhaa zinazotunza Hali ya Hewa ni uteuzi ulioratibiwa wa chapa zenye nia moja kama vile Allbirds, Credo Beauty, Cuyana, L'Occitane na zaidi.** Nenda kwenye programu ya Uber Eats ili uanze kununua na ufuatilie chapa na ofa mpya, ambazo tutakuletea hivi karibuni.

Masoko ya wakulima kwenye Uber Eats

Tunakuletea huduma za kusafirisha bidhaa kutoka kwa wakulima hadi uliko Katika Jiji la New York na Los Angeles, sasa unaweza kuweka oda ya mazao ya msimu na bidhaa mpya moja kwa moja kutoka kwa masoko ya wakulima wa eneo lako.


Kuwapa wauzaji ruhusa


Soko Linalozingatia Mbinu za Upakiaji Zinaotunza Mazingira

Soko letu la kimataifa la Upakiaji Unaotunza Hali ya Hewa linasaidia kufanya upakiaji unaotunza hali ya hewa kupatikana kwa kila mgahawa wa Uber Eats. Tunatoa promosheni kwa migahawa ili ijaribu upakiaji endelevu.

Green Ambassadors

Tutawatuza wafanyabiashara kwenye jukwaa letu, ambao wanaonyesha juhudi endelevu zenye manufaa kwa ruzuku na ofa zenye thamani ya hadi USD 50,000 ili kusaidia kufikia malengo yao ya uendelevu. Watatumika kama Mabalozi wa Utunzaji wa Hali ya Hewa na kushiriki ushuhuda wao na wafanyabiashara wengine wanaotaka kubadili ili kutumia mbinu za upakiaji zinazotunza mazingira zaidi.

Ushirikiano wa Tuzo ya Earthshot

Tumejiunga na Tuzo la Earthshot kama mshirika mwanzilishi wa kusaidia kuanzisha na kukuza mashirika ibuka yanayotunza hali ya hewa. Uzinduzi wao unafanya chaguo endelevu kuwa rahisi, nafuu na bora zaidi kwa ajili yetu sote.

Go–Get Zero logo

Usiache kutunza mazingira hadi tuondoe hewa yote chafu

Bidhaa au vipengele vinaweza kutofautiana kulingana na soko au eneo. Angalia programu yako ili uone upatikanaji.
*Ili upate maelezo zaidi kuhusu malengo ya Uber kuhusu hali ya hewa, soma ripoti yetu ya ESG ya 2024.
**Chapa huchaguliwa kulingana na kujitolea kwao katika kutunza mazingira na kujitolea kwa uzalishaji endelevu zaidi. Uber haiwajibikii madai yanayowahusu wahusika wengine, huduma au bidhaa zao.