Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Usalama umeongezwa kwenye safari zako kwa kipengele cha Kurekodi Sauti

Rekodi safari zako zote au baadhi tu ili kuhimiza tabia za kiheshima na ujilinde jambo lisilotarajiwa linapotokea.

Ongeza safu ya usalama kwenye kila safari

Weka mapendeleo yako ya Usalama

Kitarekodi kiotomatiki kulingana na mapendeleo unayoweka, chagua safari zote au baadhi ya safari, kama vile safari za usiku sana.

Rekodi zilizosimbwa kwa njia fiche

Hizi ni rekodi zinazolindwa kwa ajili ya faragha ambazo haziwezi kufikiwa na wewe, dereva wako au Kituo cha Usaidizi cha Uber isipokuwa ziambatishwe kwenye ripoti ya tukio.

Weka mipangilio ya Kurekodi Sauti

Gusa ngao ya usalama ya bluu kisha uchague Weka mapendeleo ya usalama

Weka Rekodi sauti kwa mapendeleo yako na uiruhusu programu itumie maikrofoni ya kifaa chako

Kitarekodi kiotomatiki kulingana na mapendeleo unayoweka—chagua safari zote au baadhi ya safari, kama vile safari za usiku sana

Unaweza pia kuanza kurekodi wakati wowote kwa kuchagua Rekodi sauti katika Zana ya Usalama

Jinsi ya kuambatisha rekodi kwa ripoti

  1. Nenda kwenye sehemu ya Usaidizi katika programu yako ya Uber
  2. Chagua Usaidizi katika safari
  3. Chagua safari kisha Ripoti suala la kiusalama
  4. Kwa rekodi za simu, chagua Shiriki rekodi unapoulizwa

Maswali yanayoulizwa sana

  • Kipengele cha Kurekodi Sauti sasa kinapatikana katika zaidi ya nchi kumi na mbili kote barani Afrika, Asia, Amerika Kaskazini na Amerika Kusini.

  • Inapowezekana, wasafiri na madereva wanaweza kuanzisha rekodi kupitia kipengele cha Zana za Usalama kilicho ndani ya programu kwa kutumia simu yao maizi. Msafiri mwingine aliye kwenye gari hataarifiwa wakati wa kurekodiwa, ingawa ilani imetolewa kwa watumiaji wote kwamba uwezo huu unapatikana na wasafiri wataona ujumbe kwenye programu yao ukiwajulisha kwamba sauti inaweza kurekodiwa kwenye safari yao.

    Je, huoni Rekodi ya Sauti kwenye Zana yako ya Usalama? Hakikisha kwamba una toleo jipya zaidi la programu.

  • Uber imejizatiti kuunda teknolojia zinazosaidia kufanya huduma yako ya Uber iwe salama zaidi. Kipengele cha Kurekodi Sauti kimekusudiwa kusaidia kuhimiza mawasiliano salama na ya starehe ukiwa safarini, kubaini kilichotokea na kutambua mwitikio bora baada ya tukio linalohusiana na usalama.

Kurekodi Sauti

Tumejitolea kubuni teknolojia mpya zinazosaidia kuimarisha usalama wa huduma yako ya Uber, kwa hivyo unaweza kusafiri na kuendesha gari bila wasiwasi.

Ikiwa unahisi hauko salama wakati wa safari, sasa unaweza kurekodi sauti ya safari kwenye programu.

Bofya tu ngao ya bluu ili ufungue kipengele cha Zana za Usalama na ufikie chaguo la Rekodi Sauti. Safari itarekodiwa kwenye programu na unaweza kuchagua kuishiriki na Uber baada ya safari kukamilika.

Kwa usalama wa kila mtu

Wasafiri na madereva wanaweza kurekodi sauti kupitia programu yao ili kuhimiza mawasiliano salama na ya kuridhisha wakiwa kwenye safari. Kwa kuwapa udhibiti huu, Uber inawawezesha watumiaji wake kufuatilia na kuripoti hali zisizoridhisha.

Imebuniwa kulinda faragha yako

Msafiri au dereva anapotumia kipengele hiki wakati wa safari, rekodi ya sauti itahifadhiwa na kusimbwa kwenye simu ili mtu yeyote —hata mtu aliyeanzisha kurekodi—asiweze kufikia. Uber inaweza tu kuifikia ikiwa mtumiaji atafungua ripoti ya tukio kwenye Uber na ajumuishe faili ya sauti. Isipokuwa hilo lifanyike, Uber haiwezi kufikia yaliyomo.

Saidia Uber katika uchunguzi

Tunachukulia ripoti za usalama kwa makini sana. Ikiwa mtumiaji atatuma ripoti kupitia faili la sauti, timu ya usalama italikagua. Uber itachukua hatua inayofaa kwa mujibu wa sera zetu.

  • Audio Recording is currently available in more than a dozen countries throughout Africa, Asia, Australia, Europe, New Zealand, North America, and South America.

  • Inapowezekana, wasafiri na madereva wanaweza kuanzisha rekodi kupitia kipengele cha Zana za Usalama kilicho ndani ya programu kwa kutumia simu yao mahiri. Msafiri mwingine aliye kwenye gari hataarifiwa wakati wa kurekodiwa, ingawa ilani imetolewa kwa watumiaji wote kwamba uwezo huu unapatikana na wasafiri wataona ujumbe kwenye programu yao ukiwajulisha kwamba sauti inaweza kurekodiwa kwenye safari yao.

    Je, huoni Rekodi ya Sauti kwenye Zana yako ya Usalama? Hakikisha kwamba una toleo jipya zaidi la programu.

  • Uber imejizatiti kuunda teknolojia zinazosaidia kufanya huduma yako ya Uber iwe salama zaidi. Kipengele cha Kurekodi Sauti kimekusudiwa kusaidia kuhimiza mawasiliano salama na ya starehe ukiwa safarini, kubaini kilichotokea na kutambua mwitikio bora baada ya tukio linalohusiana na usalama.

Maelezo zaidi kuhusu usalama kwenye mfumo wa Uber

Pata usaidizi wa saa 24 na wa dharura wakati wowote. Onyesha safari yako kwa wapendwa wako. Tumeweka kipaumbele kwenye usalama wako, ili ulenge fursa za kujipatia pesa.

Mamilioni ya watu huomba safari kila siku. Kila msafiri anaweza kufikia vipengele vya usalama vilivyo kwenye programu. Na kila safari ina timu ya usaidizi kwa wateja inayopatikana wakati wowote.